Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.
Source ni Nipashe radio one.
Sharia imeanza kutumika Tanga? Subirini ije mahakama ya kadhi...vilema wataongezeka
Ubaya uko wapi, watoto wa shule wanaobalehe wakikaa pamoja kuna kijimhemko ndio, na kama hawana nidhamu ndo wataanza kushikana-shikana, hapo kuna usikivu tena?
Au kwa vile waliosema ni waislamu?
Ubaya uko wapi, watoto wa shule wanaobalehe wakikaa pamoja kuna kijimhemko ndio, na kama hawana nidhamu ndo wataanza kushikana-shikana, hapo kuna usikivu tena?
Au kwa vile waliosema ni waislamu?
Wanawake na wanaume wote ni watu. Ni vema kuwaweka karibu tangu watoto ili wajifunze kushirikiana bila madhara. Hii concept ya kuwatenganisha inatokana na wenye imani kwamba wanawake ni kifaa kwa mwanaume. Serikali izibe masikio kwa watu kama hao.Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.
Source ni Nipashe radio one.
Hivi wakiristo tumekuaje?
Kwani muislam akitoa rai yake lazima ajibiwe vibaya?
KWENYE MAWODI HOSPITALINI wanavyo lala wanawake mbali na wanaume ni sababu za waisilam?
Inawezekana mungu tunayemuabudu siyo YESU KIRISTO !kama kwetu sisi waisilam ni wagonjwa na sisi matabibu , mbona tunawachukia wagonjwa?
Kwa andiko lipi?
Tusome yohana 20:16-17 ili tuwe na uhakika wa mungu.ukisoma bible mambo ya kupiga mtu mawe hayapo?
Kwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk.
Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.
Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.
Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.
Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.
wanawaka tamaa za mwili wakiwa wadogo?
kweli Mtoi umejibu vyema kabisa bila kupendelea upande wowote na kama wewe ni muislam basi wewe ni Bold Spirit.Watanzania na waafrika kwa ujumla tunahitaji kutumia busara ya hali ya juu kuhusu dini hizi kubwa ambazo zimetokea ughaibuni. Ni suala lisilopingika kuwa dini hizi tulivyoletewa zilikuja pamoja na tamaduni husika .zingine zikiwa zimeandikwa kwenye vitabu hivyo vitakatifu ambavyo havina mwanya wa amendment na mengine yakiwa hayajaandikwa ila tunaiga jinsi hao mabwana waliotuletea dini hizo wanavyoishi. Kwenye suala hili la wanafunzi wa kike na wakiume kutokukaa pamoja ni wazi kuwa ni utamaduni wa kiarabu na kwa Muumini wa kiislamu mwenye imani kali au ambaye amesoma elimu ya dini tuu na hajasoma elimu ya kawaida anachukia sana mabinti wao sio tuu kukaa dawati moja na watoto wa kiume bali wanataka hata watenhanishwe kama ilivyo msikitini.Kwangu nadhani huu ni utamaduni tuu ambao sisi kama watanzania si lazima kuufuata sana kwani hata uko uharabuni ulipotokea sasahivi unapata changamoto kubwa sana kwa wanawake wapenda mabadiliko ambao baada ya kusoma wameona utamaduni huo gandamizi kwa haki za wanawake hauna nafasi kwa karne ya sasa na wanapigana usiku na mchana kujikomboa kutokana na mfumo dume uliowachukulia wanawake kama sio viumbe wa kawaida na wakichangamana na wanaume tuu basi kinachofuata ni hisia za kingono.Kwa Tanzania kuna faida kubwa sana kwa wanafunzi kusoma wakiwa wamechanganyikana za kijamii pamoja na kitaaluma.Ni vizuri wasomi kama wewe Mtoi na wapenda mabadiliko kuwaelimisha wazee waliobobea kwenye elimu ya dini tuu na wasiopenda mabadiliko kuachana na hizo mila potofu
Unaposema wadogo unamaanisha nini ? Kwani balehe inaanzia miaka mingapi ?
bro huwa nakukubali sana your among of the jf great thinkersKwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk. Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.
Naona ukada wa CHADEMA unazidi kukuingia na hata kusahau dini yako....!
Umeambiwa watenganishwe kwenye madawati na sio vyumba vya masomo/darasa MBONA HAMSOMI MADA MKAIELEWAAAA ??