Waislam Tanga waomba watoto wa kike wasikae dawati moja na wakiume

Status
Not open for further replies.
Wewe hata kama ni muislam umechangia hoja vilivyo hujatukana!umeeleweka hata na walitoa rai hiyo.Lakini bwana mtoi hata kwenye group discussions uwezekano wa kutenganisha madawati upo , umbali wa Bluetooth ! Halafu suala hili ingawa limeletwa jf na waisilam wa tanga kwa itikadi,lakini kwenye jamii zetu za Leo ni muafaka ndio maana kuna michakato ya kujenga mabweni ya wasichana nchi nzima!
kazi kweli kweli.
 
Kwani wanasomea misikitini? Au wanataka wageuze madarasa yawe misikiti? Lakini nina shaka na chanzo cha habari hii, hata kama kila mtu ana haki ya kutoa maoni atatoaje maoni ya kijinga namna hii ilhali anajua nchi hii sio ya kiislam?

Ni kweli bro ila nchi hii pia siyo ya kikiristo haki ya kutoa maoni ipo kikatiba kwa kila mwananchi
 
Hivi wakiristo tumekuaje?
Kwani muislam akitoa rai yake lazima ajibiwe vibaya?
KWENYE MAWODI HOSPITALINI wanavyo lala wanawake mbali na wanaume ni sababu za waisilam?
Inawezekana mungu tunayemuabudu siyo YESU KIRISTO !kama kwetu sisi waisilam ni wagonjwa na sisi matabibu , mbona tunawachukia wagonjwa?
Kwa andiko lipi?
Tusome yohana 20:16-17 ili tuwe na uhakika wa mungu.ukisoma bible mambo ya kupiga mtu mawe hayapo?

Utaitwa msaliti sasa hvi, kie kie kie


Sent from my EyePhone
 
Sharia imeanza kutumika Tanga? Subirini ije mahakama ya kadhi...vilema wataongezeka

Ikija mahakama ya kadhi vilema wataongezeka au uhalifu(forbidden deeds)...utapungua?..
Think beyond the average mind can see
 
Sharia imeanza kutumika Tanga? Subirini ije mahakama ya kadhi...vilema wataongezeka
Hivi umeangalia jinsi wanavyokaa hawa watoto kwenye madawati? Yaani ni mbanano wa hali ya juu wanatiana sana vidole hawa watoto. Mahakama ya kadhi haiwezi kuleta madhara ikiwa itawahusu waislam wenyewe sisi wakristo tusiwe na uwoga
 
Hivi wakiristo tumekuaje?
Kwani muislam akitoa rai yake lazima ajibiwe vibaya?
KWENYE MAWODI HOSPITALINI wanavyo lala wanawake mbali na wanaume ni sababu za waisilam?
Inawezekana mungu tunayemuabudu siyo YESU KIRISTO !kama kwetu sisi waisilam ni wagonjwa na sisi matabibu , mbona tunawachukia wagonjwa?
Kwa andiko lipi?
Tusome yohana 20:16-17 ili tuwe na uhakika wa mungu.ukisoma bible mambo ya kupiga mtu mawe hayapo?

Ndg, issue ya kutengwa wodi za wanawake na wanaume hospitali ni tofauti na watoto kuwa darasani. Fikiria uhalisia wa mambo haya mawili.
 
Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.

Source ni Nipashe radio one.

Tunaelekea mbali lakini ni hatua za awali kuelekea utekelezaji wa mahakama za kadhi na sharia lawa. niamini nikisemacho
 
kwani wanajenga mabweni kuwatenga wasichana na wavulana? kujenga mabweni ni kuwanusuru na wazeee wasiojiheshimu huko mtaaani. kwenye mabweni c pakusomea swala lilikuwa mkao wa darasani

mimba zote za wasichana wa shule ni za wazee?
Kwani wazee wa kike mitaani hawapati mimba za wavulana?
 
Ndg, issue ya kutengwa wodi za wanawake na wanaume hospitali ni tofauti na watoto kuwa darasani. Fikiria uhalisia wa mambo haya mawili.

Tueleze tofauti kimantic sio tofauti ya dawati na kitanda
 
mchakato wa mabweni ya wasichana nchi nzima wa nini sasa?

Wewe mbona akili yako ndogo na unakazana itumike na jamii. Hivi huwezi kuona tofauti ya BWENI na DARASA?

Amsha ubongo wako, bweni ni kwa ajili ya KULALA na darasa ni kwa ajili ya KUSOMEA. Kuna tofauti kubwa kati ya KUSOMA na KULALA na ndio maana kule nyumbani kwenu ulikuwa unaweza kula, kuongea, kufanya kazi na mama yako lkn hukuweza kulala naye.

Sasa sijui una akili gani ya kulinganisha kulala na kusoma. Amsha kichwa
 
Tueleze tofauti kimantic sio tofauti ya dawati na kitanda

Wewe jamaa umejiandaa kubisha au umetumwa kabla haujajipanga.Yaaani huoni tofauti ya darasa na wodi ya wagonjwa?

Wodini kunahitajika kuvua nguo kwa ajili ya uchunguzi au kukaa uchi kutokana na sehemu inayouma. Haiwezekani kuchanganya jinsi tofauti.

Hili la kutenga watoto ni fikra potofu
 
Psychologically...unachokiongea ndio unachokiwaza!
Ngono imekutawala!

Ngono imemtawala huyo anayetaka watoto watengwe. Yeye hakuweza kuona kuwa watoto wakikaa pamoja, wale wa kike walio wazito watasaidiwa na wa kiume na kwa kujumuika mmoja atafaidika na mwenzake. Walichokiona wao ni kwamba wataingiliana kimwili. Sasa labda nikueleze kwa nini watu wa Tanga na pwani kwa ujumla wana mawazo ya namna hiyo:

Mawazo yao yanatokana na maisha yao. Watu wa Pwani wanaongoza kwa kuwaza ngono. Mwanamke wa Pwani hatizamiki kama ana faida nyingine zaidi ya ngono. Baba mtu mzima akimtazama binti mdogo anawaza kumuoa awe mke wa tatu, yaani biashara kuu ni NDOA na NGONO na mitaala hakuna cha zaidi.

Hao waliokaa chini wakawaza kuwa watoto watajamiiana wakikaa pamoja wanajua kuwa watoto wao wa kike tayari wana mawazo ya kuwa mwanaume kazi yake ni kuoa na mwanamke kazi yake ni kuolewa kwa hiyo wanajua ukiwaacha na wanaume tu, alichokisema Rais Kikwete kitatokea (Kiherehere)

Najua ubishi utakuwepo, lkn sikiliza miziki ya taarab itakwambia watu wa pwani wanawaza nini zaidi ya kuolewa ukewenza na kushindania waume
 
Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.

Source ni Nipashe radio one.

Hii kitu ipo very simple and clear!...sioni sababu ya kucomplicate!
In reality watoto wanaharibika kiasi fulan....movie/tamthilia wanazoangalia makwao wanazileta darasani..hivyo kama wakitengwa wakiwa individual iatasaidia uwepo wa righteousness and respect at all!...hii inaonekana hata majumbani dada yako ukicheza nae sn heshima inapungua,,,,,hata mavyuoni inafika kipindi kujitenga na itreractions zisizo za lazima ili kujijengea heshima..hivyo hili swala likianzia ngazi ya chini(primary)..tz gud coz heshima inaongezeka!
Na tukija kitaalam hilo wala halizuii intreraction kama theory ya cognitivism inavyoeleza ni swala la kuform group for certain goals only not something else!
Au kama mwalimu akitumiabehaviorism theory pia haitaaffect kabisa coz mwalimu atakuwa source of evrythin and inview watakuwa passive recpient of knowladge delivered!..aint see negative effects kwa hili!
Tukija kikatiba wananchi hawajavunja katiba...
Wito...ifike stage kama mawazo ya dini nyingine yanaletaa maendeleo basi tuyaheshimu na yatumike!...
 
Kwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk.
Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.

Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.

Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.
Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.
kweli Mtoi umejibu vyema kabisa bila kupendelea upande wowote na kama wewe ni muislam basi wewe ni Bold Spirit.Watanzania na waafrika kwa ujumla tunahitaji kutumia busara ya hali ya juu kuhusu dini hizi kubwa ambazo zimetokea ughaibuni. Ni suala lisilopingika kuwa dini hizi tulivyoletewa zilikuja pamoja na tamaduni husika .zingine zikiwa zimeandikwa kwenye vitabu hivyo vitakatifu ambavyo havina mwanya wa amendment na mengine yakiwa hayajaandikwa ila tunaiga jinsi hao mabwana waliotuletea dini hizo wanavyoishi. Kwenye suala hili la wanafunzi wa kike na wakiume kutokukaa pamoja ni wazi kuwa ni utamaduni wa kiarabu na kwa Muumini wa kiislamu mwenye imani kali au ambaye amesoma elimu ya dini tuu na hajasoma elimu ya kawaida anachukia sana mabinti wao sio tuu kukaa dawati moja na watoto wa kiume bali wanataka hata watenhanishwe kama ilivyo msikitini.Kwangu nadhani huu ni utamaduni tuu ambao sisi kama watanzania si lazima kuufuata sana kwani hata uko uharabuni ulipotokea sasahivi unapata changamoto kubwa sana kwa wanawake wapenda mabadiliko ambao baada ya kusoma wameona utamaduni huo gandamizi kwa haki za wanawake hauna nafasi kwa karne ya sasa na wanapigana usiku na mchana kujikomboa kutokana na mfumo dume uliowachukulia wanawake kama sio viumbe wa kawaida na wakichangamana na wanaume tuu basi kinachofuata ni hisia za kingono.Kwa Tanzania kuna faida kubwa sana kwa wanafunzi kusoma wakiwa wamechanganyikana za kijamii pamoja na kitaaluma.Ni vizuri wasomi kama wewe Mtoi na wapenda mabadiliko kuwaelimisha wazee waliobobea kwenye elimu ya dini tuu na wasiopenda mabadiliko kuachana na hizo mila potofu
 
Sasa mbona hizo shule zao za kidini wanatengwa madawati lakini bado wanaongoza kwa kupata Sifuri. Hawa watu ni wa kupuuzwa kabisa..
 
Jamani hebu tufikirie hili suala outside the box!Kwani sehemu gani kwenye Biblia wamesema ni lazima au imeshauri watoto wakiume na wakike wakae pamoja? Mbona kila kitu tunakipelekea katika masuala ya kidini tu? Na hiyo ilikuwa ni suggestion ambayo kuna sababu zimepelekea wazo hilo kutolewa so ni bora mtoa mada angekuwa specific zaidi kuwa kitu gani kimepelekea wazo hilo kutolewa na hao wazazi. Kama kuna umuhimu wa kufanyahivyo ikionekana basi na iwe kwa nia njema tu!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom