Waislam Tanga waomba watoto wa kike wasikae dawati moja na wakiume

Status
Not open for further replies.

Mbogo Junior

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
248
66
Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.

Source ni Nipashe radio one.
 
Rekebisha HEADING,HIYO HEADING TO NI ISHARA YA UNAFKI,
WEKA SAWA HEADING NTARUDI TENA

Unafiki hauna nafasi hapo. Ni suala la kupanua mawazo zaidi na kuona nini matokeo yake mbeleni. Heading ni makosa ya kawaida lakini ni vizuri umegundua hilo.
 
Hii in SHARIA naomba na waiombevsrikali kuwa wstoto watakaofeli wapigwe mawe hadi kufa?
 
Kwani wanasomea misikitini? Au wanataka wageuze madarasa yawe misikiti? Lakini nina shaka na chanzo cha habari hii, hata kama kila mtu ana haki ya kutoa maoni atatoaje maoni ya kijinga namna hii ilhali anajua nchi hii sio ya kiislam?
 
Watu wengine wameweka ngono mbele wivu mpaka kwa watoto.Kuna siku watasema wanaume wasifundishishwe na walimu wa kike
 
ikifika hapo itafikia waislam pekee wakristo pekee.alafu suni pekee na kuendelea mpaka hukoo...
 
Hivi wakiristo tumekuaje?
Kwani muislam akitoa rai yake lazima ajibiwe vibaya?
KWENYE MAWODI HOSPITALINI wanavyo lala wanawake mbali na wanaume ni sababu za waisilam?
Inawezekana mungu tunayemuabudu siyo YESU KIRISTO !kama kwetu sisi waisilam ni wagonjwa na sisi matabibu , mbona tunawachukia wagonjwa?
Kwa andiko lipi?
Tusome yohana 20:16-17 ili tuwe na uhakika wa mungu.ukisoma bible mambo ya kupiga mtu mawe hayapo?
 
vizuri sana, ni bora umeonesha uelewa na si mropokaji kama hao, asante ndugu
 
unajitahidi kusikiliza taarifa ya habari.usisahau kutuletea na habari za kimataifa
Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.

Source ni Nipashe radio one.
 
Kwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk.
Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.

Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.

Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.

Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.
 
Kwa kipindi cha sasa inabidi wavulana wakae kivyao na wasichana wakae kivyo. Hii ni kutokana na kuwa watoto wa siku hizi wanabalehe mapema na hivyo kupata mihemuko wanapokuwa wamebanana kwenye dawati moja.

Kama ni suala la kudiscuss kigroup watachangamana kwa muda. Bwt mimi sio muislam
Tukumbuke kizazi cha sasa hivi kinaharibika mapema
 
Kwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk.
Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.

Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.

Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.

Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.

Wewe hata kama ni muislam umechangia hoja vilivyo hujatukana!umeeleweka hata na walitoa rai hiyo.Lakini bwana mtoi hata kwenye group discussions uwezekano wa kutenganisha madawati upo , umbali wa Bluetooth !
Halafu suala hili ingawa limeletwa jf na waisilam wa tanga kwa itikadi,lakini kwenye jamii zetu za Leo ni muafaka ndio maana kuna michakato ya kujenga mabweni ya wasichana nchi nzima!
 
Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa. Source ni Nipashe radio one.
kuna watu wajinga jamani. Hawa ndo maandiko yalowataja kama ni mabubu, viziwi , na vipofu, wasiojua jema wala baya.
 
Wewe hata kama ni muislam umechangia hoja vilivyo hujatukana!umeeleweka hata na walitoa rai hiyo.Lakini bwana mtoi hata kwenye group discussions uwezekano wa kutenganisha madawati upo , umbali wa Bluetooth !
Halafu suala hili ingawa limeletwa jf na waisilam wa tanga kwa itikadi,lakini kwenye jamii zetu za Leo ni muafaka ndio maana kuna michakato ya kujenga mabweni ya wasichana nchi nzima!

kwani wanajenga mabweni kuwatenga wasichana na wavulana? kujenga mabweni ni kuwanusuru na wazeee wasiojiheshimu huko mtaaani. kwenye mabweni c pakusomea swala lilikuwa mkao wa darasani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom