Wahusika shughulikieni suala la chemba za maji taka kujaa kariakoo

kangesa

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
551
1,048
Mwezi wa 11 nilienda Kariakoo kwenye mitaa ya Agrey na karibu mitaa yote chemba za maji taka zilikuwa zinatoa maji machafu kuashiria karo linalohofadhi maji taka hayo kuwa yamejaa.

Lakini cha kushangaza jana nimeenda tena nakutana na shida ileile, kwa maana kwamba tatizo nililolikuta mwaka jana mwezi tajwa hapo juu bado halijashughulikiwa.

Kwa sasaivi ni kama hata wafanyabiashara wenyewe wamezoea hiyo hali kwasababu maji yanatiririka tu ni kama kuna chanzo asili cha maji ya mto lakini harufu yake na particles za vinyesi kwa mbalii ni tatizo sana kwa watu wanaotumia maeneo hayo kupata magonjwa ya mlipuko

Wananchi hasa wateja wanaopita mitaa ile wanapata kero kubwa ya kuruka maji machafu yenye harufu ya kinyesi kwa mbaliii hasa wanawake wanapata shida sana.

Shugulikieni tatizo, mbona lipo ndani ya uwezo wenu viongozi wa maeneo hayo?
 
Hiyo ndio kariakoo.Mvua zikinyesha ni lazima ukute vinyesi barabarani maana mifereji yote ya maji taka na vyoo vitatapishwa siku hiyo
 
Back
Top Bottom