BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Nimepita Kariakoo leo kwakweli hali ya Miundombinu zikiwemo Barabara za Mitaa na Chemba za Majitaka ni mbaya inatia kinyaa na Mamlaka zinaendelea kukusanya Kodi pale kama hazioni.
Mbaya zaidi Chemba zimepasuka katika maeneo ambayo watu wanalazimika kutembea kwenye uchafu unaotoka katika mitaro iliyopo chini ya Barabara.
Cha ajabu Mamlaka zinapita katika njia hizo kila wakati na hakuna hatua zinazochukuliwa ukizingatia wakat huu kuna mvua zinazoendelea kunyesha hali inayoweza kusababisha Mgaonjwa ya Mlipuko ikiwemo homa za matumbo.
Waziri wa Afya Wizara ya Afya Tanzania inapaswa kufika na kuangalia jinsi hali ya usalama wa afya za Watanzania ikiwa hatarini.