Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Watanzania wenzangu hembu tutafakari utendaji huu wa polisi.Hivi karibuni mh.Nassari na wanasisa wenzake wameripotiwa kuhojiwa na polisi juu ya matamshi waliyoyatoa kwenye mkutano wa hadhari mjini Arusha.Binafsi sipingi hatua hiyo kwani ni wajibu wa polisi.
Hata hivyo,najiuliza maswali mengi, kwa mfano, mh.Malima alipokutwa na silaha ya kivita aina ya SMG alihojiwa na file lake lilipelekwa kwa DPP?Wakwapuaji wa fedha za EPA kama Meremeta,kagoda na Deep green finance nao walihojiwa na polisi?Na kama waliohojiwa jambo hili linaloathiri umma wa watanzania liliwekwa wazi kama hili la Nasari na wenzake na kama jibu ni hapana ni kwa manufaa ya nani?
Wanasiasa wa upinzani hasa viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakikamatwa na kuhojiwa na polisi mara kwa mara tena kwa uharaka wa ajabu,lakini watuhumiwa wa ufisadi na mkosa mengine inakuwa nongwa kuwakamata na inachukua muda mrefu na pengine ni baada ya kelele nyingi kupigwa.Tujiulize ktk hii ripoti ya CAG nani amekamatwa na kuhojiwa na file lake kupelekwa kwa DPP mpaka leo hii.Je waliotajwa na CAG wana makosa ambayo hawastahili kuitwa na kuhojiwa mapema kama mh.Nassari na wenzake au makosa yao yana utaratibu tofauti?
Ni maswali ambayo mimi binafsi naona yanahitaji kutolewa ufafanuzi vinginevyo imani ya watanzania kwa jeshi la polisi itazidi kushuka na huenda ikaathiri zana nzima ya polisi jamii.