Waheshimiwa Wabunge kulala Bungeni: Je ni kutafakari au kusinzia?

Kunaumuhimu mkubwa kabisa wakupeleka vitanda na maneti bungeni.Tatizo uzee unawazidi,mawaziri lakini wazembe na wajinga tu
 
CCM hawajui kwamba huyu alishajivua gamba zamani akakimbilia NCCR Mageuzi, nako kukadoda akarudi chama cha magamba (ushauri wa Sumaye kwamba ukitaka kuwa tajiri njoo CCM ulimvuta)
Magamba wanamtumia kwa haiba yake, sijui kama inalipa.
 
Kusinzia maana yake ni kwamba hakupumzika vizuri jana yake(analipa madeni),hata hivo huu umri wa kina wasira uzee unasumbua,wabunge wanatakiwa vijana ambao damu inachemka
Wengine hata sio uzee ila manyama uzembe kama mzee wa TOT,sio rahisi mtu mwenye mwili wa kawaida tuseme uzito wa kg 70 na mwenye umri chini ya miaka 40 kusinzia sinzia ovyo kama hao wazee
 
kwa kuwa kazi za wabunge hafanyika wakiwa wamekaa katika viti na meza vinavyowekwa katika ukumbi maalum, ndio maana wabunge wa bunge la tanzania wakajitungia sheria ya kulipwa kiiitwacho "sitting allowance" yaani posho ya kukaa.

Kwa mtindo huu naoanzisha mhe stephen wassira mbunge wa ccm kuchapa usingizi kabisa ndani ya bunge, linatolewa pendekezo kuwa katika bajeti hii mhe mkulooo waziri wa fedha atenge shs bilioni 10 kwa ajili ya kuwalipa wabunge "sleeping allowance" posho ya kulala ili wakatatue matatizo ya wananchi wanayoyaota wakiwa usingizini ndani ya ukumbi wa bunge.

mhe spika naomba kuwasilisha!!!!
Usingizi Bungeni.jpg
 
Naunga mkono hoja. Bunge lianze kuwalipa waheshimiwa posho ya kulala maana wanalipwa posho ya kukaa tu wakati kuna wakati wanatakiwa kulala ukumbini huku wakitafakari
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia 100 na ikibidi viti viwe vinakunjuka kama vitanda ili wakisikia usingizi wanakunjua vitu vyao wanaendelea kuchapa usingizi kwani kila kitu kinaenda vizuri ktk nchi hii na wanatingwa na majukumu mengi bila kupata muda mzuri wa kupumzika.
Mheshimiwa Spika naunga mkono hoja
 
Naunga mkono hoja. Bunge lianze kuwalipa waheshimiwa posho ya kulala maana wanalipwa posho ya kukaa tu wakati kuna wakati wanatakiwa kulala ukumbini huku wakitafakari
Kama alivyosema Mhe Mizengo Pinda kuwa wabunge hutumia posho za kukaa wanazolipwa kutatua matatizo ya wananchi, inategemewa kuwa pindi watakapolipwa posho za kulaa watazitumia kutatua matatizo ya wananchi yanayowajia katika njizo wanakuwa wakikoroma katika ukumbi wa bunge.
 
Huyo wa kwanza ndio mbunge wa jimbo langu. Sijui anakesha wapi huyo mtu.
 
Wana jf tujadiliane sababu hasa inayopelekea wabunge kulala bungeni wakati wana mda wa kutosha wa kupumzika usiku,kitalaamu mtu inabidi alale kati ya masaa sita hadi saba mbona muda wanao,tatizo ni nini
 
Wana jf tujadiliane sababu hasa inayopelekea wabunge kulala bungeni wakati wana mda wa kutosha wa kupumzika usiku,kitalaamu mtu inabidi alale kati ya masaa sita hadi saba mbona muda wanao,tatizo ni nini

na michepuko nayo inachangia,naombeni kwa mwenye ile picha ya augustine mrema akiwa amelala mpaka udenda ukamtoka aniwekee hapa akumbuka ilitokaga kweny gazeti la mwananchi
 
Back
Top Bottom