Waheshimiwa Wabunge kulala Bungeni: Je ni kutafakari au kusinzia?

attachment.php



Duh! Mpaka udenda unamwagika!
 
Nyama za mnadani bia za baridi ,posho tele na dm zakutosha halafu uchangiaji hafifu mradi jioni posho imeingia,wengine ulabu mwingi,wengine uzee,wengine wanatunga uongo wa kesho kikao kijacho
 
hakuna kutafakari ukimwuliza kilikuwa kinazungumzwa nini wala hajui.........huko ni kuvimbiwa kutoka na mafweza wanayopata changanya na umri
 
Viyoyozi viachwe ila wawekewe magogo wakalie badala ya hivyo viti m'bonyeo na mneso! Tuone kama watalala! Tatizo ni hivyo vikalio vyao!!!
 
lugha ya picha,tunasubiri ya pinda, makinda, mkulo na wengineo pia kwani si huyu mwenye hiyo tabia pekee..
 
Hivyo vinaitwa vi Siesta. Lakini on wakati mwengine mtu anaweza kuonekana kama amelala kumbe anatazama chini au amefumba macho anatafakari. Picha inaweza kuongea maneno 1000 yakawa yote ya uongo.
 
Hivyo vinaitwa vi Siesta LOL. Lakini on a serious note wakati mwengine mtu anaweza kuonekana kama amelala kumbe anatazama chini au amefumba macho anatafakari. Picha inaweza kuongea maneno 1000 yakawa yote ya uongo.
 
Sasa na huyo mama amefuta mwongozo angalau ulikuwa unawamusha. sijui itakuwaje
 
attachment.php


huyu ni waziri wa nchi ofisi ya rais (mahusiano na uratibu) wa serikali ya jamhuri ya muungano ya tanzania akisikiliza bunge la bajeti ya serikali ya mwaka 2011/12.wassira ndie alieachiwa shughuri za serikali bungeni na waziri mkuu baada ya mh.waziri mkuu kupata uzuru kwa siku ya jana.
 

Attachments

  • IMAG0060.JPG
    IMAG0060.JPG
    806.5 KB · Views: 109
View attachment 32516

huyu ni waziri wa nchi ofisi ya rais (mahusiano na uratibu) wa serikali ya jamhuri ya muungano ya tanzania akisikiliza
bunge la bajeti ya serikali ya mwaka 2011/12.wassira ndie alieachiwa shughuri za serikali bungeni na waziri mkuu baada
ya mh.waziri mkuu kupata uzuru kwa siku ya jana.

Kama usikilizaji wenyewe ni wa aina hii ndo' maana kila siku tunaingia mikataba isiyoeleweka.
Mungu ibariki Tanzania
 
lugha ya picha,tunasubiri ya pinda, makinda, mkulo na wengineo pia
kwani si huyu mwenye hiyo tabia pekee..

Vipi kuhusu ya spika Ana, atakapobanwa na kujikuta akikurupuka kumshutumu Tundu Lissu kuwa aache
kuikosoa serikali wakati muongeaji ni waziri mkuu.
 
Huu ni wizi tu haijalishi chama wala itikadi. Wewe unalipwa utekeleze majukumu yako lakini badala yake unakwenda kulala bungeni. Akizinduka na kukuta meza zinagongwa, na yeye pia anagonga bila aibu huku akiwa hajui ni nini kinaongelewa. Wakizungumzia juu ya kuondoa posho ndiyo wa kwanza kupinga hiyo hoja.
 
Sasa hivi kuna lugha mpya imekuja tunapoona waheshimiwa wakiwa wamesinzia huku vikao vya bunge vikiendelea pale bungeni, kwa mfano gazeti moja la kilasiku kutoa picha ya muheshimiwa naibu waziri wa ushirikiano wa Africa Mashariki, Dk. Abdulla Juma Saadalla akiwa ameuchapa usingizi kabisa pale bungeni siku ya jumanne katika kikao cha kuchangia bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011 -2012 lakini lugha ilyotumika pale ni kua alikua ANATAFAKARI jambo! Haya tena siku ya jumatano gazeti hilohilo limetoa picha ya muheshimiwa waziri wa Nnchi,ofisi ya Raisi (Mahusiano na uratibu) Stephen Wassira naye kwenye picha gazeti la jumatano akiwa anaonekana ameuchapa usingizi kabisa, lakini lugha iliyotumika pale ni kua ANATAFAKARI! Jamani wanaJF wenzangu nisaidieni kuhusiana na hii lugha!
IHaya mwaya mwacheni waziri wetu anatafakari namna ya kuwabishia akina  Lissu,Zitto,Mnyika,Halima Mdee,David Kafulila na wengine walio active kutoka upinzani!Au anasikitika kwa nini upinzani wameanzisha hoja ya kufuta posho wakati yeye anajipanga tena kununua khanga,kofia ili akawadanganye watu wa Bunda
 
Back
Top Bottom