WAHAYA na WANYAKYUSA hufilisika kwenye utu uzima

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856
Mimi ni Mhaya upande wa baba na Mnyakyusa upande wa mama.
Nia ya uzi huu ni kutafuta tiba ya kitabia.
Tabia za Wahaya na Wanyakyusa kwa kiasi kikubwa sana zinafanana.
Kinachoniuma na kuniumiza nafsini mwangu ni kuona Wahaya na Wanyakyusa wengi hufilisika kadiri wanavyo ongezeka umri mali nayo hupukutika.
Je tufanyeje ili tuwe kama Wachagga ambao mali hushamiri kadiri umri unavyoongezeka?
 
HTML:

Labda utoe mifano halisia, kabla hatujaijadili hoja yako
 
HTML:
Mfano mmoja ni mzee Mangomango wa Mwenge na Rwechungura wa Masaki. Hadi wanakufa wamekufa wakiwa makapuku

Lakini hao mbona ni wachache kati ya wahaya na wanyakyusa wengi? na kama hoja yako ina ukweli, inawezekana hawana hulka ya kurithisha au kuwafundisha watoto wao wangali bado wana nguvu.
 
Mimi ni Mhaya upande wa baba na Mnyakyusa upande wa mama.
Nia ya uzi huu ni kutafuta tiba ya kitabia.
Tabia za Wahaya na Wanyakyusa kwa kiasi kikubwa sana zinafanana.
Kinachoniuma na kuniumiza nafsini mwangu ni kuona Wahaya na Wanyakyusa wengi hufilisika kadiri wanavyo ongezeka umri mali nayo hupukutika.
Je tufanyeje ili tuwe kama Wachagga ambao mali hushamiri kadiri umri unavyoongezeka?

Napenda kuongeza na Wasukuma pia. Nimeishi na watu hawa Wahaya, Wanyakyusa na Wasukuma nimeona mengi yanayofanana niseme tu hawa jamaa wana tabia ya kusquander ie kutumia mali kwa fujo sana hasa kwenye vileo, vyakula na wanawake. Pengine hapo ndipo mchawi wao alipo.

Wahaya na Wasukuma wengi wakishatoka kwao basi hawaangalii nyuma tena. Ndio maana unaona Wahaya wengi wakijitutumua hapa mjini kwamba wamesoma lakini nenda Kashozi, Muleba, Mtukula n.k umaskini wa ajabu na kagera ni moja mikoa maskini zaidi Tz. Mimi nadhani idadi ya akina mangi waliosoma ni mara 3 ya wahaya lakini jamaa hawajitambulishi sana lakini wapo, wajanja sana hawa jamaa. Angalia vizuri vyuo vikuu utaona sijui wanamission gani, lakini no sweat ni wa kuigwa

Tofauti na akina Mangi ambao nimewaona ni watu makini sana kwenye matumizi ya jasho lao. Unaweza kumkuta mangi ana bilioni 3 lakini matumizi yake ni ya kawaida wala habweteki na pesa. Atafikiri kujenga nyumba hata kama tayari anazo nyumba 5. atasomesha watoto na kununua ardhi.

Na hii ndio inayowafanya akina mangi waonekane kama wabahili, kumbe sio ubahili ni kuweka kipaumbele (priority) kwenye mambo ya msingi kwanza na starehe baadaye.

Ushauri wangu ni kwamba badilika kitabia na kuwa na maono ya muda mrefu, fikiria kuinvest (kuwekeza unapopata hela) lakini weka hiyo mipango kabla hata ya kupata hela kwani kama huna hiyo mipango siku ukipata hela ghafla zitaishia kwenye mabinti, pombe, nk.

Akina mangi ni wanywaji lakini wanakunywa kwa step na wanapokaa baa hawakai tu ili kunywa bali utakuta ndio kikao chao cha kukutana na kupanga mipango ya biashara, (asilimia karibu 35% ya wanaokaa kwenye mabaa ni wao lakini bado hawafilisiki kihivyo) tofauti na wengi wetu ni kupiga mastori ya malaya tu

Ila wanapoteza sana kwenye masherehe ya kifahari ya harusi na mtu mmoja alipiga mahesabu na kugundua kuwa gharama za harusi zote za akina mangi kwa mwaka ni zaidi ya bilioni 100! Wangeweza kujenga chuo kikuu kimoja kila mwaka! Lakini bado hii haiwafilisi sana, ina pesa hii mijitu tukubali
 
Mikela,
Nimeishi kyela; kuna ukweli fulani kuhusu Wanyakyusa wanachacha sana uzeeni: Mfano; Marehemu Obasi Katule, Mwaituka, Mwakasumi, Mwakabumbe, Mtemi,
 
Kafara za kjihaya na kinyakyusa cum sukuma huisha nguvu kadri unavyotumbua, teheteheteheteheteheteheteheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!
 
Nafikiri ni vema pia kufahamu chanzo cha utajiri wa haya makabila. I mean ufahamu wa mchakato/namna/mbinu/ au njia wanazopita watu hawa kuusaka mpaka wakawa au wakaupata utajiri wao ndo utakao tupa pa kuanzia kujua ni kwanini wanafilisika mapema wafikapo uzeeni.
 
me nawapongeza kwa kuwa wanakula jasho lao, kila mtu atafute vya kwake sio kutegemea wazazi. ni mtazamo tu.
 
Ndugu hao wachaga uliowatolea mfano nao wana mambo yao ya ajabu sana!! Mali zinawafanya wake wengi kuua waume zao wakifika utu uzima! Wanyakyusa pia nao wana tabia hizi!!
 
Mimi ni Mhaya upande wa baba na Mnyakyusa upande wa mama.
Nia ya uzi huu ni kutafuta tiba ya kitabia.
Tabia za Wahaya na Wanyakyusa kwa kiasi kikubwa sana zinafanana.
Kinachoniuma na kuniumiza nafsini mwangu ni kuona Wahaya na Wanyakyusa wengi hufilisika kadiri wanavyo ongezeka umri mali nayo hupukutika.
Je tufanyeje ili tuwe kama Wachagga ambao mali hushamiri kadiri umri unavyoongezeka?

Punguzeni mbwembwe na kujikweza kwani ili ufanikishe mbwembwe hizo lazima kutakuwa na utumiaji mbaya wa pesa.Mnajitahidi kwenye kutafuta pesa lakini knowledge ya uchumi imewapiga chenga.Weka malengo,tafuta pesa(kihalali),na utaipata tuu!matumizi yasizidi uwezo,timiza malengo yako,save,fanya investment......utaona graph ya maendeleo inapanda kila kukicha!............Anza leo,hujachelewa kijana.
 
wewe uctake kumuingiza na former health minister prof david mwakyusa kwamba last tym alikuwa waziri tena wa afya lakini leo muda unazidi kwenda na uzee ndo huuooo!yupo 2 kapotoza direction!ila kwa upande wa pili 2nae dr harisson mwakyembe mbn yeye last tym alikuwa chini na leo yupo juu na muda unazidi kuyoyoma!!mkuu eh haya maisha bwana toa fikra mgando za miaka ile ya giza!komaa fanya kazi utakachokipata kula nusu nusu hifadhi.
 
Kuna kaukweli ndani yake. ila cku hizi vijana wanagitahidi kuenda na wakati, hakuna cha kabila wala nini...unaweza kuumkuta kijana wa kihaya anafanya mambo ya kutisha (maendeleo) na kijana wa kichagga kadorola.....so tusi-stereotype kabila/makabila kwa sasa...
 
unaweza kufikiria ivyo kwa sababu wachanga tokea zamani walikua na sifa yakua na noti. lakini kwa sasa kila mmoja nimtafutaji naomba toa fikira izo
unamaana unamanisha wahaya na wanyakyusa niwatu wanao jisahau? sikweli labda kizazi kile si chaleo,
 
Mimi ni Mhaya upande wa baba na Mnyakyusa upande wa mama.
Nia ya uzi huu ni kutafuta tiba ya kitabia.
Tabia za Wahaya na Wanyakyusa kwa kiasi kikubwa sana zinafanana.
Kinachoniuma na kuniumiza nafsini mwangu ni kuona Wahaya na Wanyakyusa wengi hufilisika kadiri wanavyo ongezeka umri mali nayo hupukutika.
Je tufanyeje ili tuwe kama Wachagga ambao mali hushamiri kadiri umri unavyoongezeka?

Ndg, nahisi wewe wala hutoki makabila hayo ila umeamua kwa sababu zako kuwadharau au kufanya hivo kwa sababu unazozijua. Mambo mengine ni magumu kujudge kwa sentensi moja tu.
Naamini hukuwa no.1 ktk shule zako, je tukuite mjinga, mpumbafu au vyovyote sababu wako waliokuzidi?
Au je utajisikiaje wazungu wakisema Waafrika wote ni wajinga, masikini, au tusi lolote lile baya maana wametuzidi kila kitu (in general)
Nadhani ktk mifano hiyo utajifunza kitu.
Kama unahisi mmefanikiwa sana au mna kipaji fulani, mshukuru Mungu tu na wala usiwadharau wengine.
Nakubali kuna challenges na mambo ya kujifunza toka kwa waliofanikiwa, lakini huwezi hukumu kuwa wale walioko hivi basi wote ni sababu hii.
 
Mimi ni Mhaya upande wa baba na Mnyakyusa upande wa mama.
Nia ya uzi huu ni kutafuta tiba ya kitabia.
Tabia za Wahaya na Wanyakyusa kwa kiasi kikubwa sana zinafanana.
Kinachoniuma na kuniumiza nafsini mwangu ni kuona Wahaya na Wanyakyusa wengi hufilisika kadiri wanavyo ongezeka umri mali nayo hupukutika.
Je tufanyeje ili tuwe kama Wachagga ambao mali hushamiri kadiri umri unavyoongezeka?
dah... Mkuu hiyo ni bonge ya combination... kama PCB, maana ukienda Mbeya balaa, Bukoba Balaa

aisee
 
Back
Top Bottom