Wahariri na Rais Kikwete: Yametimia yaliyotabiriwa?

yule mhariri wa mwananchi anaitwa bakari sijui,aliuliza maswali kama mtoto wa form two!sijui swaumu ilikuwa kali au ndo wale marafiki wa zitto ambao ni marafiki wa jk pia...shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit
 
Huyu muhariri akiwa anaongea kwenye TV kwa ukali lakini nashangaa sana jana kapata nafasi ya kumuuliza JK swali uso kwa macho lakini kauliza swali dhaifu sana...JK sijui aliwapa nini wahariri alikuwa akicheka na wenyewe wanacheka.

Wahariri walikuwa wanauliza maswali dhaifu sana utadhani wapo kwenye kipindi cha malumbano ya hoja.

Kaka nimecheka sana hapo eti akicheka na wenyewe wanacheka au walikuwa wanachekeana? nchi hii bhana imeingia kwenye tope na ina pancha tunazidi titia tu
 
Ukweli ni kwamba wahariri wa magazeti yetu hawako informed kama tunavyodhani...ndio maana ni wazuri kwa tu kwa KUHARIRI habari wanazoletetwa au kuagizwa kuandika... nje hapo hakuna kitu.
 
acheni unafiki. maswali a msingi yaliulizwa. EPA, richmond, ulimboka, mgomo wa madaktari, mgomo wa walimu, chenji ya rada pamoja na rushwa nyingine nini. msiwaonee wahariri. mwanahalisi ni gazeti la udaku na majungu. namshukuru JK kwa kuweka kila kitu wazi. ni hodari wa kujibu maswali
 
Wengi wapo after bahasha then bias.wana njaa mpaka wanadhalilisha taaluma.WAMUIGE KUBENEA.
 
Yana mwisho yote hayo mungu pamoja na taifa letu naamini tutafika tunapopataka siku sio nyingi wote walio watumwa wa wenye fedha watafunguliwa na ubora wa fani zao utakuwa chachu ya maendeleo.

Kwa mikakati ipi? Au kwakupiga goti na kumwomba MUNGU!
 
Uhuru wa vyombo vya habari umebakwa na wao wamekubali na kufurahia. Ni sawasawa na mtu kajifanya kalewa chakari anaamua kupita katikati ya kundi la wahuni (masela) majira ya usiku then akifika karibu nao anaamua kujiangusha na kulala kifudifudi na anabaki pale kwa muda kuwa amezidiwa hawezi kunyanyuka na hajitambui. Anafurahia kutendewa anachotendewa.
 
i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.

ALIULIZA HIVI.
Mh kuna baadhi ya Vyombo vya habari vinadai serekali imehusika
Ningalipata mimi nafasi ningaliuliza hivi.
Mh rais. hivi karibuni baadhi ya magazeti na yalimtaja mtumishi wa Ikulu (Ningalimtaja jina )ndio wahusika wa utekaji wa Dk Ulimboka. Swali. kwa kuwa Ikulu ni pahala patakatifu , Jee mh kweli mtumishi huyu alietajwa yupo kweli Ikulu? na kama yupo nini msimamo wa serekali yako kama hayupo Ikulu wala haimjui kwanini serekali imekaa kimya kukanusha habari hizo kupitia Msemaji wa Ikulu kama tulivyozoea kusikia kupitia Kurugenzi ya mawasiliano?

b)Kwanini Mh rais umeshindwa kuunda tume huru kuondoa wingu hili

............HAASWAAAAAAAAAAAA..................!!!!!!!!!!!!!:israel:
 
Wakuu tukumbuke Jk aliingia madarakani kwa kutumia wahariri na anatawala nchi kwa kutumia wahariri na mapepo!
 
Njaa Njaa kitu kibaya sana...hata Absaloom Kibanda yupo kimaslahi!Anajua siku Chadema ikichukua nchi nafasi ya Salva Rweyimamu itakuwa yake!Hakuna weledi,hakuna Uzalendo...pengne tungekuwa na "Freelencer Editors"
 
bila shaka yametimia!

The bottomline is that some of the journalists and other professions are taken through education institutions that are not really and contextually education institutions but a pretence of schools. Ama tatizo ni wakufunzi wao au ni wao wenyewe kwani inaonyesha hawawezi kufanya critical au critique analysis. They are either obfuscated of the two amidst ignorance flocking from reading divorce. The latter is a problem of the vasty majority of young generation of Tanzania supplemented by a kind of some higher education syllabuses that is higand highly specialised and disciplined based. Hii aina ya elimu haiwandai Watanzania kupanua wigo wa kuchambua issues. Haiyumkiniki waandishi wa habari wanashindwa kuwa paraphrase maswali yanayohakisi usomi na uelewa wa mambo. Wanaacha issues muhimu na kuuliza vitu amabavyo viko too general. Kwanza issues ya Ulimboka is a tip in the icerge of how people are psycholically and physically tortured. Swali lingelenga kuonyesha kuwa of the barbaric events and some alleged to have been plotted but somehow ended up aborting as they were known before ni kwanini State security agencies are zinahusishwa. Nikwanini zinakuja na utetezi usio na mashiko? Kama kashfa kama za Loliondo, Richmond, EPA, Meremeta na nyinginezo zimetokea wakati tunajidai kuwa kati ya nchi nchi zenye the best trained security agencies na hawakuzizuia mpaka zinaiburiw na wansiasa hasa wa upinzani what is the fundamenta role of our defence and security and intelligence agencies
 
Niliwadharau sana, kwamfano alipokuwa anajibu hoja ya kukunua CT SCAN akasema 'anayedhani gharama za ct scan ni sawa na bei shangingi aje tumpe hiyo fedha akatuletee', wao mnaowaita wahariri wakaitikia kwa kuunga mkono wakisema ninakukuu 'labda ya kichina' Ni watu wapuuzi sana, hovyo kabisa, wanaakisi aina ya jamii ya watu wasiojua matatizo na asili ya mazingira magumu yanayowazunguka, hali ambayo itawafanya kuendelea kuwa katika matatizo hayo kwa muda mreefu hadi watakapozinduka.
 
Kwanini kubenea mwenyewe hakwenda, yule jamaa namkubali angemchana laivu?


Next time Mkweree akiwaita wahariri wa magazeti, aende Ansbert Ngurumo badala ya Kabanda kutoka Tanzania Daima na wahariri wakatae kupeleka maswali kabla!! Pia waruhusiwe kuuliza follow up questions kama wataridhia kupeleka maswali kabla ,hapo wanaweza kumnasa mkwereee.
 
Mimi huwa nasoma Mwanahalisi tu la nisome Mwana Spoti sinunui Mwananchi wala upuuzi mwingine hakuna wahariri kabisa ila wanafiki tu
 
Bado mimi sielewi hili jambo lilivyokaa. Ninavyojua mimi maswali huulizwa mtu/msemaji baada ya kusikiliza anachokiongea. Sasa iweje utume maswali ya kumuuliza mtu ambaye bado hata hujakisikia anachokisema? Hili ni kosa la kiufundi. Na kama hilo limefanyika basi hatuna hata haja ya kuwa na sheria yoyote ya kutambua uwepo wa wanahabari nchini, kwakuwa hawapo kabisa. Hakuna mwanahabari yeyote anayeweza fanya hivi. Tuwatafutie jina jingine tu.
 
i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.

ALIULIZA HIVI.
Mh kuna baadhi ya Vyombo vya habari vinadai serekali imehusika
Ningalipata mimi nafasi ningaliuliza hivi.
Mh rais. hivi karibuni baadhi ya magazeti na yalimtaja mtumishi wa Ikulu (Ningalimtaja jina )ndio wahusika wa utekaji wa Dk Ulimboka. Swali. kwa kuwa Ikulu ni pahala patakatifu , Jee mh kweli mtumishi huyu alietajwa yupo kweli Ikulu? na kama yupo nini msimamo wa serekali yako kama hayupo Ikulu wala haimjui kwanini serekali imekaa kimya kukanusha habari hizo kupitia Msemaji wa Ikulu kama tulivyozoea kusikia kupitia Kurugenzi ya mawasiliano?

b)Kwanini Mh rais umeshindwa kuunda tume huru kuondoa wingu hili


Mimi ndiye Absalom Kibanda niliyezushiwa kuuliza swali hilo? Akutukanaye hakuchagulii tusi. Swali langu lilihusu mgomo wa madaktari na lililikuwa na sehemu zipatazo nne. Suala la Ulimboka lilikuwa ni kipengele cha nne na hayo yaliyoandikwa hapo si maneno yangu.

Niliuliza: "Mheshimiwa Rais, taifa bado linakabiliwa na mwangwi wa mgomo wa madaktari. Katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja sasa, madaktari wamegoma mara tatu na miongoni mwa sababu wanazotoa ni kutoridhishwa kwao na namna serikali inavyowajali kwa maana ya kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuzingatia maslahi yao mengine.

Jambo kubwa ambalo madaktari hao wanalisema ni namna serikali inavyoangalia vipaumbele vyake katika kuwahudumia wananchi. Moja wa hoja zao kwa mfano, madaktari wanashangazwa na kukosekana kwa mashine ya T scan katika hospitali zote za umma nchini wakati serikali hiyo hiyo ikitumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kununua mashangingi kwa maana ya V 8 ambazo wanasema gari moja la aina hiyo lina uwezo wa kununua mashine moja ya aina hiyo.

Mheshimiwa Rais mgomo wa mwisho wa madaktari hao ulifanyika miezi michache tu baada ya wewe mwenyewe kulihakikishia taifa mwezi Machi mwaka huu kupitia hotuba yake kwa taifa uliyoitoa kupitia mkutano wako na wazee wa Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine ulituahidi kwamba mgomo ule wa mwezi wa Pili ungekuwa ni wa mwisho.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba kile ulichokisema hakikuwa. Je serikali na wewe mmejifunza nini kutokana na madai hayo ya madaktari ikiwa hasa baada ya azma yako ya kuona migomo ikikoma kutotimia kama ulivyoahidi mwezi Machi?

Mheshimiwa Rais ukiyaacha hayo, mgomo huo wa madaktari ulizaa tukio la kutekwa nyara, kuteswa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka. Ingawa katika hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi Juni ulisema serikali haikuhusika na tukio hilo, taarifa ambazo zimeendelea kuripotiwa kupitia katika vyombo vya habari zimeendelea kuihusisha serikali yako katika tukio hilo. Je baada ya hali hiyo kutokea, ni nini kauli yako kuhusu kuendelea kwa taarifa hizo zinazoendelea kuihusisha serikali yako na kitendo hiki cha kinyama?"
 
Hapa nafikiri ni suala la kuelewa hasa nini maana ya hii mikutano ya habari au "press conference". Hili ni tukio muhimu kwa nchi maana mkuu wa nchi anazungumza na vioo vyetu vya jamii ambavyo vinawakilishwa na wahariri wake wakuu.

Wahariri ni watu muhimu sana kwenye fani ya uandishi na mawazo yao yanaheshimika sana. Wahariri wanaweza kugeuza upepo wa muelekeo wa kisiasa ama uwe unafuata upane huu au upande ule.

Mheshimiwa raisi kama anataka mikutano halisi na waandishi basi inabidi aamue kwamba ama iwe anasoma taarifa rasmi kuhusu tukio fulani au matukio mbalimbali na ambayo yatafuatiwa na maswali ya waandishi (wahariri), au anakuwa amewaita wahariri ili wamuulize maswali tu na yeye kujibu au anaweza kuwaita kwa yeye kuongea tu na yasiulizwe maswali.

Sasa hio sentensi ya mwisho (ambayo inahusu yeye kuongea tu bila kuulizwa maswali) ndio utaratibu ambao raisi anafanya kwa kuzungumza kwenye luninga na baada ya hapo anapotea.

Mikutano kati ya viongozi wakuu wa serikali kama raisi na wahariri inaeleweka kwamba maswali yatakuwa yanakusanywa na wahariri na maofisa wa habari wa raisi lakini tayari wahariri wakiwa wamewasili pale Ikulu na kama ni kuchambuliwa kutafanyika hapohapo na baadae itajulikana ni nani watauliza maswali ambayo yamo kwenye orodha na ni akina nani watauliza maswali yalio nje ya orodha na haya ndio yahahitaji uangalifu kuyajibu.

Nionavyo mimi binafsi ni kwamba hapakuwepo na mkutano wa maana katia ya wahariri na mheshimiwa raisi bali kulikuwana mazungumzo kati ya pande mbili ambazo hakikuwa na malengo yoyote.

Bado nalipa gazeti la Mwanahalisi na mhariri wake Saed Kubenea alama za juu kwa habari zake zenye kujaa uchunguzi wa kina na wenye ushahidi wote usio na chembechembe za uchakachuaji.

Uandishi wa kupokea hundi au "chequebook journalism" utokomezwe kwa nguvu zote.

Hawa wahariri walioenda Ikulu naona kwamba bado hawajaiva kwenye kazi zao.

I'm very disappointed indeed.
 
Back
Top Bottom