i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.
Huwa najiuliza sana. Kwanini tzdaima huwa linaandika mambo makubwa na ya kiuchokozi sana kuhusu Serekali ya JK . Lkn huwa nashangaa kila mara wakikutana uso kwa uso na JK huwa mdomo wa muhariri huyu huingia kitetemeshi . kazi wanayofanya huwa ni nyepesi sana na maswali yake hata Katibu tarafa wa CCM anaweza kuijibu tena huku akicheka
ALIULIZA HIVI JANA.
Mh kuna baadhi ya Vyombo vya habari vinadai serekali imehusika Kumteka Dk Ulimboka.
Ningalipata mimi nafasi ningaliuliza hivi.
Mh rais. hivi karibuni baadhi ya magazeti na yalimtaja mtumishi wa Ikulu (Ningalimtaja jina )ndio wahusika wa utekaji wa Dk Ulimboka. Swali. kwa kuwa Ikulu ni pahala patakatifu , Jee mh kweli mtumishi huyu alietajwa yupo kweli Ikulu? na kama yupo nini msimamo wa serekali yako kama hayupo Ikulu wala haimjui kwanini serekali imekaa kimya kukanusha habari hizo kupitia Msemaji wa Ikulu kama tulivyozoea kusikia kupitia Kurugenzi ya mawasiliano?
b)Kwanini Mh rais umeshindwa kuunda tume huru kuondoa wingu hili
Siyo huyu tu ila hata Bakari machumu pamoja na kuuliza swali ndefu ambalo mkulima viazi kule Mangola angeweza kuliuliza vizuri na kwa mpangilio zaidi. Maswali ya kweli yapo press conference za US na Ulaya. Hapa kwetu Wahariri wengi wanavizia kazi ya Rweyemamu na wanamwuuliza rais swali kwa mtindo wa jibu ili asijisikie vibaya
Mara nyingi wanaocheza nje ya uwanja huwa wanafunga magoli mengi sana.
Kwanini kubenea mwenyewe hakwenda, yule jamaa namkubali angemchana laivu?
Serikali imelifungia gazeti la MWANAHALISI. Wiki hiyo hiyo Rais Kikwete akawaalika wahariri kwenda kuongea nao Ikulu. Akawaagiza waandike maswali na kuyatuma mapema. Wakatii na kuyatuma. Orodha ya waalikwa ikachambuliwa. Ni sawa na kusema, ili uwe mhariri ni lazima ikulu ikubali kuwa wewe ndiye mhariri. Haya tuyaweke pembeni, tujikumbushe yaliyowahi au kutabiriwa/ kusemwa kuhusu waandishi wa Tanzania.
-Kwamba, ni wavivu wa kufikiri
-Kwamba, hawajui kuuliza maswali ya maana,
-Kwamba, hawajui kufanya uchunguzi na kuandika vizuri habari za uchunguzi,
-Kwamba, ni "vijibwa" vya watawala na wenye fedha,
-Kwamba, ni "makanjanja" wanaochafua tasnia ya habari, n.k.
Kwa kitendo cha wahariri kutii kwenda Ikulu na kukubali kuandaa maswali na kuyatuma mapema, wakati gazeti mojawapo limefungiwa kibabe, kimewadhalilisha sana wahariri wetu. Kimedhihirisha kwa dhati kuwa waandishi hawana umoja wala mshikamano na kwa hiyo ni ruksa kwa dola kuwafanyia itakavyo.
Hata katika nchi zilizoendelea, marais na viongozi wa nchi hizo, wakiitisha mikutano na wahariri au waandishi, huwapa uhuru wa kuulizwa maswali hata kama wanaweza kufanya mbinu ya kuwainua na kuwapa fursa ya kuuliza wale ambao hurusha "friendly fire" kwa watawala. Huu utaratibu wa wahariri wetu kukubali "kuandikiana barua za mapenzi" na rais ukome maana unaidhalilisha tasnia ya habari. Kama rais anataka maswali yaliyoandikwa, basi na yeye ajibu kwa maandishi na awatumie waliouliza.
Kukosekana kwa umoja na mshikamano miongoni mwenu, kunawafanya muishi kwa matumaini ya kuteuliwa ua kuingia katika siasa ili muendeleze michezo michafu mnayoipiga hivi sasa mkiwa mmevaa glovu. Jamani mnashindwa kumwuliza Rais, ikiwa serikali haikumteka Dr. Ulimboka kwa nini haichunguzi utekaji huo? Mnakubaliana na kujiumauma kwake kuwa "maneno yako mengi na yataendelea kuwapo"!
MMENISIKITISHA SANA.
i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.
Huwa najiuliza sana. Kwanini tzdaima huwa linaandika mambo makubwa na ya kiuchokozi sana kuhusu Serekali ya JK . Lkn huwa nashangaa kila mara wakikutana uso kwa uso na JK huwa mdomo wa muhariri huyu huingia kitetemeshi . kazi wanayofanya huwa ni nyepesi sana na maswali yake hata Katibu tarafa wa CCM anaweza kuijibu tena huku akicheka. Inaonekana baadhi ya habari za TZDAIMA zinaandikwa na watu makini kama wabunge wa Chadema na muhariri hupitishiwa. kibaya zaidi ndie mwenyekiti wa jukwa la wahahariri tz