Wafungwa-Hatma ya Ndoa zao Ikoje?

Erickb52

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
18,539
11,442
Jamani nimekaa nikajiuliza inapotokea mtu akafungwa Jela, na alikuwa na mke/mume je hatma ya ndoa yao ikoje? Je anayebaki uraiani anatakiwa asipate unyumba hadi kifungo cha mwenzi wake kiishe mfano Miaka 15? Je kiubinadamu inawezekana kuvumilia kwa muda wote huo hata kama unajilinda? Haki ya wanaobaki uraiani ikoje? Na km akitoka nje kuna ubaya au afanyaje?
 
mambo kama haya hutokea pindi unapotupwa lupango
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana kabisa kuvumilia, vinginevo kile kiapo cha "Nitavumilia wakati wa shida na raha" kifutwe!.
 
Hata magereza ya bongo kulikuwa na vyumba maalumu vya wafungwa kukutana na wenza wao ila kwa sasa vimebomolewa na serekali imeongeza vyumba ya kulala wafungwa
 
hii kitu imekaa vibaya ila nafikiri kutakuwa na kautaratibu flani kwa wenye ndoa ila lazma utoe chochote kwa askari
 
hii kitu imekaa vibaya ila nafikiri kutakuwa na kautaratibu flani kwa wenye ndoa ila lazma utoe chochote kwa askari
Ila kwa hapo lazma aliyebaki nje awe na huo moyo wa kumpa mwenzake haki yake
 
Kwa nini kusiwekwe kachumba ili waliofungwa wawe wanapata haki zao kutoka kwa wenzi wao.Mbona USA wanazingatia haki za wafungwa.
 
Kuna haja ya kuangalia haki za wafungwa ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kukutana na wenzi wao wa ndoa. Kifungo hakijamuondolea haki hiyo.Kama tuna nia basi hili linawezekana. tatizo letu ni ukosefu wa ubunifu katika mfumo wa magereza yetu na ni moja ya majukumu ya tume ya haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom