Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,623
DPP Atumie Nolle.jpg

Wanabodi,

Jumatatu ya leo, naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili, makala ya leo ni swali la ushauri wa Bure kwa DPP, kwa vile Rais Samia, ameishaonyesha nia njema ya kutaka Watanzania watendewe haki, Jee sasa tumshinikize DPP, kuzifuta kwa kutumia Nolle, zile kesi zote zinazo sua sua, ikiwemo kesi ya Masheikh wa Uamsho.

Huu ni mwaka wa 8, watu wako mahabusu, kesi ya Rugemalila, huu ni mwaka wa 4, haijaanza kusikilizwa, usikute kuna mahabusu wako ndani kwa miaka 10 sasa lakini hatuwajui, ikitokea watu hawa wakakutwa hawana hatia, hakuna kiwango chochote cha fidia kinaweza kuwafidia muda wao zaidi ya karma.

Hii ndio Makala yenyewe in full.

KWA MASLAHI YA TAIFA, KILIO CHA HAKI TANZANIA- DPP. TUMIA NOLLE KUTIMIZA NIA NJEMA NA ADHMA YA RAIS SAMIA KUTENDA HAKI.

Na Pascal Mayalla
Karibuni tena kwenye makala nyingine ya Kwa Maslahi ya Taifa kuhusu Kilio cha Haki Tanzania, leo ikiwa ni mfululizo wa makala za Kilio cha Haki Tanzania, tukiiangazia ofisi ya DPP, mada zinazotokana na uwepo wa kilio cha haki kwa Watanzania kutokana na kutotendewa haki na vyombo vya utoaji haki, Ujio wa rais SSH, umefufua upya dhima, ari na kasi ya haki kwa kauli zake na matendo ili kuwafuta machozi Watanzania na kuliponya taifa kwenye suala zima la utoaji haki.

Makala ya leo, ni ushauri wa bure kwa DPP afanye nini ili kuwatendea haki Watanzania, ila kabla sijatoa ushauri, naomba niwatembeze kidogo kwenye ofisi ya DPP, kuangalia Dira, Dhima na Maadili ya Msingi ya ofisi ya DPP.​

DIRA: Haki, amani na usalama kwa maendeleo ya Taifa, Je ofisi ya DPP inatenda haki?, pasipo haki kuna amani?, pasipo amani kuna usalama?, pasipo usalama kuna maendeleo?. Uchunguzi unaendeleo miaka 4, bila kesi kusikilizwa, huku watuhumiwa wakisota gerezani, hii ni haki gani?

DHIMA
Kushirikiana na wadau na kuendesha kesi bila woga, upendeleo ili kuhakikisha uwepo wa haki, amani, na usalama katika jamii. Jee ni ushirikiano gani ambao DPP anafanya na wadau, ili kesi ziendeshwe bila woga, na upendeleo?

MAADILI YA MSINGI
(i)Uwajibikaji: kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu kwa wakati, magereza zimefurika mahabusu, wengine ni zaidi ya miaka 4, uchunguzi unaendelea bila kesi kuanza kusikilizwa?, huu ni uwajibikaji gani?.

(ii) Kukubalika: uthabiti na uwezo wa kuaminika na kuthaminiwa;kukubalika gani, kwa udhabiti gani na kwa uwezo gani wa kuaminika, kama kuna kesi, all transactions zimefanywa kwenye benki tatu zote ziko jijini Dar es Salaam, uchungunguzi haujakamilika, huu ni zaidi ya mwaka wanne!, huu ndio uwezo gani wa kuaminika?

(iii) Uadilifu: kwa maadili na uaminifu bila kuvumilia vitendo vya rushwa na ubadhirifu;Hili la rushwa kwenye vyombo vya utoaji haki, naomba nisilizungumze sasa, maana makala za Jaji Mkuu ndizo zinafuta, hili nitalizunguza mbele.

(iv)Weledi: kwa kujituma,kujitoa,umahili na utaalamu ndani na nje ya ofisi;

Huduma bora:kwa kutoa huduma bora kwa kufanya kazi pamoja ,heshima na adabu, hili pia naomba nisilizungunze leo, linahitaji data journalism, kwa kuonyesha kesi ngapi serikali imeshindwa kwa aibu, ndipo tutazungumzia weledi, kujituma na umahiri wa ofisi ya DPP, hii itakuja kuwa na makala yake.
Hitimisho na Mapendekezo.
  1. Mheshimiwa Rais, Mama Samia ameisha onyesha nia ya dhati kwa kauli na matendo kutaka Watanzania watendewe haki, mpira sasa uko uwanjani, mezani kuanzia Jeshi la Polisi, IGP, DCI, DPP, na Mahamama, kujipanga kucheza huu mchezo kwa mujibu wa Kifungu cha 26 (1) ambacho kinatoa "Kila mtu ana jukumu la kuzingatia na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ”. Kitendo cha Jeshi letu la polisi, ofisi ya DCI, DPP, na mfumo mzima wa utoaji kutokutenda haki, ni kwenda kinyume cha Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977.
  2. DPP haipaswi kuanzisha, mashitaka bila kuwa na ushahidi wa kutosha, na badala yake atumie wakati wake wote kufanya uchunguzi, ili kesi inapopelekwa mahakamani ni kwenda kusikilizwa tuu. Kifungu cha 8 cha sheria ya NPSA kinatoa mwongozo mzuri kwa DPP juu ya vigezo vya kuzingatia anapofanya uamuzi wa aidha ashitaki au la, DPP aliyetangulia, hili hakulizingatia, DPP mpya ukizingatia mwongozo huu kwa weledi tutaona mabadiliko.
  3. Kama ilivyo kwa haki ni stahiki ya mtuhumiwa na sio hisani, dhamana pia ni haki ya mshitakiwa na sio hisani, tunapaswa kubadilisha sheria zetu, ili kila kosa liwe linadhaminika, isipokuwa makosa ya mauaji ya kukusudia, ujambazi kutumia silaha na kadhalika, au kama mtuhumiwa ni hatari na anaweza kuhatarisha uchunguzi au upelelezi, lakini Tanzania lazima tufike mahali, mpaka mtuhumiwa anafikishwa mahakamani , lazima kuwe ushahidi wa kutosha, sio mtu anatiwa mahabusu miaka 8!.
  4. Serikali isione sifa au raha kuwasweka watu mahabusu, bila kujiridhisha kwanza kwa ushahidi usiotia shaka kuwa ni wahusika wa jinai husika, inapotokea wakakutwa hawana hatia, hakuna kiwango chochote cha fidia kinaweza kuwafidia muda waliopoteza magerezani. Nchi za wenzetu, DPP hawezi kuwakamata watu na kuwasweka tuu mahabusu kabla hajakamilisha uchunguzi. Hivyo DPP, asikamate watuhumiwa wa kesi ambazo sio hatarishi kwa amani na usalama, kabla ya kukamilisha uchunguzi, just imagine, Mzee Rugemalila ana miaka zaidi ya 80, unamsweka mahabusu kwa zaidi ya miaka 4, mtu huyu anahatarisha vipi amani au ataingilia vipi uchunguzi wakati kila kilichofanyika, kimefanyika , kimefanyika kwa maandishi na kumbukumbu zote zipo kidigitali?.
  5. Ni wakati sasa wa DPP kutumia kikamilifu mamlaka yake ya Nolle Prosequi na kuondoa mashtaka dhidi ya watuhumiwa wote, katika kesi zote ambazo zina zaidi ya muda mrefu zinazo sua sua bila uchunguzi kukamika, au bila kusikilizwa kwa sababu ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha, iikiwemo kesi ya Rugemaliza, kesi ya wizi “Milioni Kwa Sekunde” , Kesi ya Masheikh wa Uamsho na kesi nyingine zote, halafu watafute ushahidi taratibu, wakiupata, ndio wazifungue tena.
  6. Lengo la kumsweka mtu mahabusu kwa makosa ya kudhaminika ni ili kumzuia asitoroke, Kitambulisho cha Taifa kina taarifa zote muhimu, hivyo kwa makosa madogo madogo, Polisi wafanye uthibitisho wa taarifa hizo, kitambulisho cha taifa kitambuliwe kama hati rasmi ya dhamana kujidhamini wenyewe kwa makosa madogo, hakuna haja ya kuwaweka watuhumiwa mahabusu kwa kesi ya kuiba kuku.
  7. Paia naelewa jinsi mifumo ya maisha na baadhi ya miundombinu ya makazi haswa maeneo ya uswazi, siyo rafiki kuwezesha mtuhumiwa anayepata dhamana kujulikana mahali alipo endapo ataruka dhamana na kujificha. Mfano mtuhumiwa anayeishi squatter area kama Mbagala rangi tatu au Manzese uwanja wa Fisi ambako hakuna mitaa wa anwani za makazi. National ID pekee haitoshi kumtambua mtu na makazi yake akiamua kubadilisha makazi, kwa watu hawa, serikali za mitaa ndizo zitumike kama dhamana, japo ni kweli kuna baadhi ya vibaka, kukaa mahabusu au kufungwa jela ndio salama yao, tumeshuhudia wakiachiwa hawadumu uraiani.
  8. Kuna watuhumiwa wako mahabusu kwa makosa yanayodhaminika, bali DPP ameiamuru mahakama kuzuia dhamana zao. Hapa kuna mambo 3.Moja ni masuala ya weledi,haki na uwajibikaji wakati wa kutekeleza mamlaka kwa mujibu wa kifungu hiki.Mbili,ni uhalali wa kifungu hiki kikatiba ambacho kwa kweli hakitoi uwajibikaji kabisa ndio maana kilifutwa kwenye CPA baada ya mahakama kujiridhisha kifungu hiki kinakwenda kinyume cha katiba, lakini kitu cha ajabu sana, kifungu hiki bado kipo kwenye EOCCA!. Kinafanya nini?. Mahakama inapofuta kifungu Fulani kwa kwenda kinyume cha katiba, kifungu hicho kifutwe kwenye sharia zote.
  9. Hata kwa makosa yanayohitaji mtu kusweka mahabusu, Tanzania tutumie nafuu za kidigitali, kwa kuanzisha digital cells, mtuhumiwa kuzuiliwa nyumbani kwake, hata kutumikia kifungo nyumbani kwa anafungwa GPS inayofungwa kwa lakiri ya kidigitali, na kuwa confined nyumbani kwake, nyumba hiyo inafungwa IP Camera, hivyo polisi wanaona nyendo zote za mtuhumiwa, akivuka tuu ile IP camera, inapiga alarm, mtuhumiwa anakuwa amekiuka masharti hivyo kustahili kuzuiliwa mahabusu. Utaratibu huu unaruhusu mke anapata haki zake za ndoa, watoto wanapata mapenzi ya baba, na baba kuendelea na shughuli za kuingiza kipato cha kuendesha familia.
  10. Hebu wafikirie Masheikh wa Uamsho, huu ni mwaka wa 8 wako mahabusu!, fikiria madhara ya kijamii na kiuchumi ambayo humpata mtu kwa kuswekwa ndani muda mrefu bila dhamana, kwanza unawatesa kisaikolojia, unatesa wake zao na familia zao, baadhi yao wake za masheikh hawa, wameachika bila kupenda kwa kushindwa kuvumilia maisha ya kukaa miaka 8 bila haki ya ndoa kwa vile hawa ni washika dini wa swala 5, siyo wanawake wazinifu kwamba wafanye tu uzinzi huku wakisubili waume zao, hata madaktari wanashauri, viungo vile kukaa miaka 8 bila kutumika sio afya.
  11. Baadhi ya watuhumiwa wamefiwa ndugu zao, wazazi wao na wapendwa wao bila kupewa haki ya kushiriki mazishi yao, akiwemo mwanafani mwenzetu Erick Kabendera, ambaye mama yake alitoa kilio mahali kuwa uhai wake unamtegemea mwanae. Mama huyo alipoteza maisha na mwanae hakuruhusiwa kumzika, Sisi watu wa karma, tulitoa angalizo la karma ya huyu mama, wanaojua karma ilikuja kufanya nini, wanajua!. Wapo baadhi ya mahabusu ambao wamepata matatizo ya kiafya permanently kwa kurundikana mahabusu bila huduma za msingi ambapo wangeweza kujihudumia wenyewe wawapo nje. DPP anapata faida gani kuswekwa watu rumande na kuzuia dhamana?!.
  12. Hivi karibuni kuna video imetrend kwenye mitandao ya kijamii jamaa aliswekwa lupango akiwa ndo kwanza ameoa na hajapata mtoto na mkewe. Kaswekwa jela miaka 8 bila hatia, karudi anakuta mkewe ana watoto wanne, ila mke akamwambia alikuwa anamsubiri, hivyo sasa ndoa inaendelea.
  13. Kwenye hili la dhamana kwa kila kesi lifanyike kwa washitakiwa wasio hatarishi, lakini kwa kesi za mauaji ya kukusudia, unyanganyi wa kutumia silaha na uhaini, kuzuiliwa mahabusu kuendelee mtu akijua kuwa kutoka ni ngumu possibility ya kujump bail ni kubwa au kuwadhuru key witness.
  14. Japo hapa natetea haki za watuhumiwa , pia naomba kuzingatia haki za wahanga wa uhalifu. Katika ulimwengu wa uhalifu kuna watu wabaya kupita kipimo. Just imagine unakuta mtu mzima umembaka mtoto wa miaka 2 na kumharibu vibaya sehemu zake za siri na pengine akamwambukiza HIV, mauaji ya kutisha , vitendo vya vikundi vya kihalifu kama panya road na mapanga yao wanapokuingilia na kukucharanga mapanga bila huruma na kumbaka binti yako au mkeo mbele yako na visa vingine vingi. Hao nao wasipate dhamana kwa vile wamepoteza sifa za haki yao kuwa huru.
  15. Ule utaratibu wa notification kwa makosa ya usalama barabarani, na kulipa faini za papo kwa papo, utumike pia kwenye vituo vya polisi, mwizi wa kuku akiri kuiba kuku, akubali kumlipa aliyemuibia na kulipa faini, kesi hiyo inaishia hapo hapo kituoni wala haina haja na kufikishwa mahakamani.
  16. Majaji wetu, kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana, nao wanapaswa kufanya kazi kama vituo vya polisi, mahospitali na dharura nyingine kwa saa 24. Kama ilivyo kwa madaktari wa zamu anapigiwa simu kukitokea dharura, kuwe na majaji wazamu saa 24/7. Nimeshuhudia hii Afrika Kusini, kila mtuhumiwa anapelekwa kwa hakimu wakati wowote hadi usiku wa manane, kama vile madaktari au vituo vya polisi.
  17. Criminal Justice System inahitaji kufanyiwa reform ili kuendana na wakati. Duniani kote magereza yako kwa ajili ya kutenga watu wabaya na jamii. Tujiulize toka kupata uhuru magereza mangapi yamejengwa ili yakidhi haja ya ongezeko la uhalifu. Wahalifu na uhalifu hatari kwa jamii unapoongezeka wahalifu lazima wataonekana wanajazana magereza
  18. Kwa upande wa sociological jurisprudence jamii yetu bado ina kisasi kingi. Kibaka tu wanawachoma moto. Je wale ndugu wataweza kumuacha salama mtuhumiwa anayedhaniwa kukatisha uhai wa mpendwa wao aidha kwa armed robbery au murder. Bado naamini reform ya jamii ianzie kwenye social justice system other than legal or criminal justice system. Malezi ya jamii, mfumo wa elimu juu ya haki jamii ili kuepuka visasi tuwafundishe waha, wajita na wakurya etc waache visasi vyao ya asili ili tuweze kupunguza mlundikano wa mahabusu ambao wengine wanahifadhiwa kuepusha kuthuriwa na wanajamii wanakoishi.
  19. Makosa kama ya economic offences kwanza watuhumiwa wanaweka tangible security wakiruka dhamana serikali itarecover kutoka kwenye security/bond. Pia wahujumu uchumi wengi ni active economic drivers wa wanajamii wao so kuwahold is an economic distortion kwa wao wenyewe na serikali inaua ile mifumo ya uchumi wao.
  20. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, Taifa litaponywa, haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami, tukianza na Mahakama.

pascomayalla@gmail.com

0754270403
 
Ni hoja nzuri sana, hasa ikizingatiwa nolle prosequi haizuii DPP kufungua kesi upya atakapopata ushahidi muafaka.

Kuweka watu miaka rumande kwa kigezo cha ushahidi kutokamilika ni mateso makubwa.

Aidha katika mazingira kama haya ya kupiga danadana haki za watu mahakamani, huwa najiuliza, uhuru wa mahakama uko wapi?
 
Kwa ujumla tuna sheria za ajabu sana na ushetani ndani yake. Sheria zetu zinatoa mwanya, mkiwa na utawala wa kishetani, kama awamu iliyopita, kuwatendea uovu bila kulazimishwa na chombo chochote kutenda haki.

Tunahitaji katiba mpya, tunahitaji marekebisho makubwa ya sheria zetu:

1) Makosa yote yawe na dhamana isipokuwa pale tu inapothibitika kuwa mtuhumiwa ni hatari kwa usalama wa watu wengine na yeye mwenyewe. Ikiwezekana, jambo hilo lithibitishwe na chombo kingine na siyo na DPP.

2) Hata inapothibitika mtuhumiwa ni vema akawekwa mahabusu, kuwa na muda wa mwisho wa mtuhumiwa kukaa mahabusu kama hakuna ushahidi uliopatikana.

3) Kuwe na chombo kingine huru kitakachokuwa na uwezo wa kuchunguza mashtaka yote ambaye yana harufu ya kumbambikizia makusudi mtuhumiwa. Na ikithibitika, waliotenda hivyo wapelekwa mahakamani kujibu mashtaka, na ikithibitika walimbambikizia mtuhumiwa, kuwe na adhabu ya watu waliofanya kosa hilo kwa makusudi kwenda jela, angalao siyo chini ya miezi 6.

Ni lazima tujenge Taifa la watu wastaarabu. Tusiishi kama wanyama wa Serengeti ambapo mwenye nguvu anamkamata na kumwua aliye dhaifu, wakati wowote anaotaka.
 
Nakala nzuri sana brother keep it up.

DPP mpya akifanyia kazi Hoja zako jamii itamwelewa kwa kweli.

inasikitisha sana kuona mtu anasekwa lupango zaidi ya miaka 4.

Pia DPP aangalie na baadhi ya sheri a zinazonyima zamana ni sheria kandamizi sana .
 
Hii mada ukiita kwa maslahi ya taifa nakuelewa kabisa.Ila zile zingine zingine hapana aise.brother kuna muda uko viziri kichwani.Hebu tumia kichwa chako kwa upande huu zaidi badala ya ule wakujipendekeza uone kama neema haitakushukia.nchi hii bado inachangamoto nyingi sana zakusema na kuweka sawa ila hili litawezekana pale ambapo nyie ambao mmesoma na mna uwanja mpana wakutoa mawazo yenu mtakapo amua kutumia muda wenu sawasawa kwa manufaa ya jamii nzima.Naunga mkono hoja.Hiyo ni namba ya simu au cheque no.
 
Kwa ujumla tuna sheria za ajabu sana na ushetani ndani yake. Sheria zetu zinatoa mwanya, mkiwa na utawala wa kishetani, kama awamu iliyopita, kuwatendea uovu bila kulazimishwa na chombo chochote kutenda haki.

Tunahitaji katiba mpya, tunahitaji marekebisho makubwa ya sheria zetu:

1) Makosa yote yawe na dhamana isipokuwa pale tu inapothibitika kuwa mtuhumiwa ni hatari kwa usalama wa watu wengine na yeye mwenyewe. Ikiwezekana, jambo hilo lithibitishwe na chombo kingine na siyo na DPP.

2) Hata inapothibitika mtuhumiwa ni vema akawekwa mahabusu, kuwa na muda wa mwisho wa mtuhumiwa kukaa mahabusu kama hakuna ushahidi uliopatikana.

3) Kuwe na chombo kingine huru kitakachokuwa na uwezo wa kuchunguza mashtaka yote ambaye yana harufu ya kumbambikizia makusudi mtuhumiwa. Na ikithibitika, waliotenda hivyo wapelekwa mahakamani kujibu mashtaka, na ikithibitika walimbambikizia mtuhumiwa, kuwe na adhabu ya watu waliofanya kosa hilo kwa makusudi kwenda jela, angalao siyo chini ya miezi 6.

Ni lazima tujenge Taifa la watu wastaarabu. Tusiishi kama wanyama wa Serengeti ambapo mwenye nguvu anamkamata na kumwua aliye dhaifu, wakati wowote anaotaka.
Hiyo na 1 yako unaposema "dhamana isipkuwa itakapothibitishwa na chombo huru" ndio mwanya wenyewe wa kuendelea kuwekwa ndani. Uwazacho ni utopia isiyotekelezeka hata kwa formulation yako mwenyewe bado imeacha loophole ya watu kuwekwa ndani.
 
Katiba yetu inatueleza kuwa Mahakama ndio chombo pekee cha kutoa HAKI, sasa inakuwaje inashuhudia na kuacha ukiukwaji wa haki za watuhumiwa ukifanyika kwa watuhumiwa kwa muda mrefu?!

watuhumiwa wanasota rumande zaidi ya miaka 8?! na mahakama ipo tu inaaangalia haina nguvu ya kisheria zaidi ya kusikitika na kulalama kwa mtuhumiwa/watuhumiwa,Jaji au Hakimu akidai kuwa mahakama haina cha kufanya, inabanwa na sheria!!!!! hiki ni kichekesho!!

Katiba inaipa Mahakama nguvu ya utoaji haki lkn sheria zingine zina kwaza utendaji wa mahakama!!

kama kuna sheria zinazo ibana mahakama isitende haki basi kweli ni bora sheria hizo zibainishwe na kisha zirekebishwe na pia ziongezwe sheria za kuipa nguvu mahakama ktk utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya utoaji Haki.

kwa sheria zilizopo inaonekana DPP ana nguvu kubwa kuliko hata mahakama!!! hii inaondoa maaana na malengo ya mahakama kuwa chombo cha kusimamia na kutoa Haki.

sio suala la kutekeleza nia njema ya Rais bali ni suala la kusimamia sheria kwa uadilifu bila kuonea.

leo tuna Rais mwenye nia njema asiye penda uonevu, mpenda haki, kesho tutakuwa na Rais wa ina nyingine, kesho kutwa wa aina nyingine!!! je, unadhani tutakuwa tumetatua tatizo?
jambo la msingi ni kuzirekebisha sheria zote ambazo zinaonekana wazi zinakandamiza haki za mtuhumiwa, lkn pia sheria zote ambazo zina ipa nguvu kubwa ofisi ya DPP kufanya atakavyo bila Mahakama kufanya chochote au bila Mahakama kulinda haki za Mtuhumiwa.
 
View attachment 1818080

Wanabodi,

Jumatatu ya leo, naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili, makala ya leo ni swali la ushauri wa Bure kwa DPP, kwa vile Rais Samia, ameishaonyesha nia njema ya kutaka Watanzania watendewe haki, Jee sasa tumshinikize DPP, kuzifuta kwa kutumia Nolle, zile kesi zote zinazo sua sua, ikiwemo kesi ya Masheikh wa Uamsho.

Huu ni mwaka wa 8, watu wako mahabusu, kesi ya Rugemalila, huu ni mwaka wa 4, haijaanza kusikilizwa, usikute kuna mahabusu wako ndani kwa miaka 10 sasa lakini hatuwajui, ikitokea watu hawa wakakutwa hawana hatia, hakuna kiwango chochote cha fidia kinaweza kuwafidia muda wao zaidi ya karma.

Hii ndio Makala yenyewe in full.

KWA MASLAHI YA TAIFA, KILIO CHA HAKI TANZANIA- DPP. TUMIA NOLLE KUTIMIZA NIA NJEMA NA ADHMA YA RAIS SAMIA KUTENDA HAKI.

Na Pascal Mayalla
Karibuni tena kwenye makala nyingine ya Kwa Maslahi ya Taifa kuhusu Kilio cha Haki Tanzania, leo ikiwa ni mfululizo wa makala za Kilio cha Haki Tanzania, tukiiangazia ofisi ya DPP, mada zinazotokana na uwepo wa kilio cha haki kwa Watanzania kutokana na kutotendewa haki na vyombo vya utoaji haki, Ujio wa rais SSH, umefufua upya dhima, ari na kasi ya haki kwa kauli zake na matendo ili kuwafuta machozi Watanzania na kuliponya taifa kwenye suala zima la utoaji haki.

Makala ya leo, ni ushauri wa bure kwa DPP afanye nini ili kuwatendea haki Watanzania, ila kabla sijatoa ushauri, naomba niwatembeze kidogo kwenye ofisi ya DPP, kuangalia Dira, Dhima na Maadili ya Msingi ya ofisi ya DPP.​

DIRA: Haki, amani na usalama kwa maendeleo ya Taifa, Je ofisi ya DPP inatenda haki?, pasipo haki kuna amani?, pasipo amani kuna usalama?, pasipo usalama kuna maendeleo?. Uchunguzi unaendeleo miaka 4, bila kesi kusikilizwa, huku watuhumiwa wakisota gerezani, hii ni haki gani?

DHIMA
Kushirikiana na wadau na kuendesha kesi bila woga, upendeleo ili kuhakikisha uwepo wa haki, amani, na usalama katika jamii. Jee ni ushirikiano gani ambao DPP anafanya na wadau, ili kesi ziendeshwe bila woga, na upendeleo?

MAADILI YA MSINGI
(i)Uwajibikaji: kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu kwa wakati, magereza zimefurika mahabusu, wengine ni zaidi ya miaka 4, uchunguzi unaendelea bila kesi kuanza kusikilizwa?, huu ni uwajibikaji gani?.

(ii) Kukubalika: uthabiti na uwezo wa kuaminika na kuthaminiwa;kukubalika gani, kwa udhabiti gani na kwa uwezo gani wa kuaminika, kama kuna kesi, all transactions zimefanywa kwenye benki tatu zote ziko jijini Dar es Salaam, uchungunguzi haujakamilika, huu ni zaidi ya mwaka wanne!, huu ndio uwezo gani wa kuaminika?

(iii) Uadilifu: kwa maadili na uaminifu bila kuvumilia vitendo vya rushwa na ubadhirifu;Hili la rushwa kwenye vyombo vya utoaji haki, naomba nisilizungumze sasa, maana makala za Jaji Mkuu ndizo zinafuta, hili nitalizunguza mbele.

(iv)Weledi: kwa kujituma,kujitoa,umahili na utaalamu ndani na nje ya ofisi;

Huduma bora:kwa kutoa huduma bora kwa kufanya kazi pamoja ,heshima na adabu, hili pia naomba nisilizungunze leo, linahitaji data journalism, kwa kuonyesha kesi ngapi serikali imeshindwa kwa aibu, ndipo tutazungumzia weledi, kujituma na umahiri wa ofisi ya DPP, hii itakuja kuwa na makala yake.
Hitimisho na Mapendekezo.
  1. Mheshimiwa Rais, Mama Samia ameisha onyesha nia ya dhati kwa kauli na matendo kutaka Watanzania watendewe haki, mpira sasa uko uwanjani, mezani kuanzia Jeshi la Polisi, IGP, DCI, DPP, na Mahamama, kujipanga kucheza huu mchezo kwa mujibu wa Kifungu cha 26 (1) ambacho kinatoa "Kila mtu ana jukumu la kuzingatia na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ”. Kitendo cha Jeshi letu la polisi, ofisi ya DCI, DPP, na mfumo mzima wa utoaji kutokutenda haki, ni kwenda kinyume cha Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977.
  2. DPP haipaswi kuanzisha, mashitaka bila kuwa na ushahidi wa kutosha, na badala yake atumie wakati wake wote kufanya uchunguzi, ili kesi inapopelekwa mahakamani ni kwenda kusikilizwa tuu. Kifungu cha 8 cha sheria ya NPSA kinatoa mwongozo mzuri kwa DPP juu ya vigezo vya kuzingatia anapofanya uamuzi wa aidha ashitaki au la, DPP aliyetangulia, hili hakulizingatia, DPP mpya ukizingatia mwongozo huu kwa weledi tutaona mabadiliko.
  3. Kama ilivyo kwa haki ni stahiki ya mtuhumiwa na sio hisani, dhamana pia ni haki ya mshitakiwa na sio hisani, tunapaswa kubadilisha sheria zetu, ili kila kosa liwe linadhaminika, isipokuwa makosa ya mauaji ya kukusudia, ujambazi kutumia silaha na kadhalika, au kama mtuhumiwa ni hatari na anaweza kuhatarisha uchunguzi au upelelezi, lakini Tanzania lazima tufike mahali, mpaka mtuhumiwa anafikishwa mahakamani , lazima kuwe ushahidi wa kutosha, sio mtu anatiwa mahabusu miaka 8!.
  4. Serikali isione sifa au raha kuwasweka watu mahabusu, bila kujiridhisha kwanza kwa ushahidi usiotia shaka kuwa ni wahusika wa jinai husika, inapotokea wakakutwa hawana hatia, hakuna kiwango chochote cha fidia kinaweza kuwafidia muda waliopoteza magerezani. Nchi za wenzetu, DPP hawezi kuwakamata watu na kuwasweka tuu mahabusu kabla hajakamilisha uchunguzi. Hivyo DPP, asikamate watuhumiwa wa kesi ambazo sio hatarishi kwa amani na usalama, kabla ya kukamilisha uchunguzi, just imagine, Mzee Rugemalila ana miaka zaidi ya 80, unamsweka mahabusu kwa zaidi ya miaka 4, mtu huyu anahatarisha vipi amani au ataingilia vipi uchunguzi wakati kila kilichofanyika, kimefanyika , kimefanyika kwa maandishi na kumbukumbu zote zipo kidigitali?.
  5. Ni wakati sasa wa DPP kutumia kikamilifu mamlaka yake ya Nolle Prosequi na kuondoa mashtaka dhidi ya watuhumiwa wote, katika kesi zote ambazo zina zaidi ya muda mrefu zinazo sua sua bila uchunguzi kukamika, au bila kusikilizwa kwa sababu ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha, iikiwemo kesi ya Rugemaliza, kesi ya wizi “Milioni Kwa Sekunde” , Kesi ya Masheikh wa Uamsho na kesi nyingine zote, halafu watafute ushahidi taratibu, wakiupata, ndio wazifungue tena.
  6. Lengo la kumsweka mtu mahabusu kwa makosa ya kudhaminika ni ili kumzuia asitoroke, Kitambulisho cha Taifa kina taarifa zote muhimu, hivyo kwa makosa madogo madogo, Polisi wafanye uthibitisho wa taarifa hizo, kitambulisho cha taifa kitambuliwe kama hati rasmi ya dhamana kujidhamini wenyewe kwa makosa madogo, hakuna haja ya kuwaweka watuhumiwa mahabusu kwa kesi ya kuiba kuku.
  7. Paia naelewa jinsi mifumo ya maisha na baadhi ya miundombinu ya makazi haswa maeneo ya uswazi, siyo rafiki kuwezesha mtuhumiwa anayepata dhamana kujulikana mahali alipo endapo ataruka dhamana na kujificha. Mfano mtuhumiwa anayeishi squatter area kama Mbagala rangi tatu au Manzese uwanja wa Fisi ambako hakuna mitaa wa anwani za makazi. National ID pekee haitoshi kumtambua mtu na makazi yake akiamua kubadilisha makazi, kwa watu hawa, serikali za mitaa ndizo zitumike kama dhamana, japo ni kweli kuna baadhi ya vibaka, kukaa mahabusu au kufungwa jela ndio salama yao, tumeshuhudia wakiachiwa hawadumu uraiani.
  8. Kuna watuhumiwa wako mahabusu kwa makosa yanayodhaminika, bali DPP ameiamuru mahakama kuzuia dhamana zao. Hapa kuna mambo 3.Moja ni masuala ya weledi,haki na uwajibikaji wakati wa kutekeleza mamlaka kwa mujibu wa kifungu hiki.Mbili,ni uhalali wa kifungu hiki kikatiba ambacho kwa kweli hakitoi uwajibikaji kabisa ndio maana kilifutwa kwenye CPA baada ya mahakama kujiridhisha kifungu hiki kinakwenda kinyume cha katiba, lakini kitu cha ajabu sana, kifungu hiki bado kipo kwenye EOCCA!. Kinafanya nini?. Mahakama inapofuta kifungu Fulani kwa kwenda kinyume cha katiba, kifungu hicho kifutwe kwenye sharia zote.
  9. Hata kwa makosa yanayohitaji mtu kusweka mahabusu, Tanzania tutumie nafuu za kidigitali, kwa kuanzisha digital cells, mtuhumiwa kuzuiliwa nyumbani kwake, hata kutumikia kifungo nyumbani kwa anafungwa GPS inayofungwa kwa lakiri ya kidigitali, na kuwa confined nyumbani kwake, nyumba hiyo inafungwa IP Camera, hivyo polisi wanaona nyendo zote za mtuhumiwa, akivuka tuu ile IP camera, inapiga alarm, mtuhumiwa anakuwa amekiuka masharti hivyo kustahili kuzuiliwa mahabusu. Utaratibu huu unaruhusu mke anapata haki zake za ndoa, watoto wanapata mapenzi ya baba, na baba kuendelea na shughuli za kuingiza kipato cha kuendesha familia.
  10. Hebu wafikirie Masheikh wa Uamsho, huu ni mwaka wa 8 wako mahabusu!, fikiria madhara ya kijamii na kiuchumi ambayo humpata mtu kwa kuswekwa ndani muda mrefu bila dhamana, kwanza unawatesa kisaikolojia, unatesa wake zao na familia zao, baadhi yao wake za masheikh hawa, wameachika bila kupenda kwa kushindwa kuvumilia maisha ya kukaa miaka 8 bila haki ya ndoa kwa vile hawa ni washika dini wa swala 5, siyo wanawake wazinifu kwamba wafanye tu uzinzi huku wakisubili waume zao, hata madaktari wanashauri, viungo vile kukaa miaka 8 bila kutumika sio afya.
  11. Baadhi ya watuhumiwa wamefiwa ndugu zao, wazazi wao na wapendwa wao bila kupewa haki ya kushiriki mazishi yao, akiwemo mwanafani mwenzetu Erick Kabendera, ambaye mama yake alitoa kilio mahali kuwa uhai wake unamtegemea mwanae. Mama huyo alipoteza maisha na mwanae hakuruhusiwa kumzika, Sisi watu wa karma, tulitoa angalizo la karma ya huyu mama, wanaojua karma ilikuja kufanya nini, wanajua!. Wapo baadhi ya mahabusu ambao wamepata matatizo ya kiafya permanently kwa kurundikana mahabusu bila huduma za msingi ambapo wangeweza kujihudumia wenyewe wawapo nje. DPP anapata faida gani kuswekwa watu rumande na kuzuia dhamana?!.
  12. Hivi karibuni kuna video imetrend kwenye mitandao ya kijamii jamaa aliswekwa lupango akiwa ndo kwanza ameoa na hajapata mtoto na mkewe. Kaswekwa jela miaka 8 bila hatia, karudi anakuta mkewe ana watoto wanne, ila mke akamwambia alikuwa anamsubiri, hivyo sasa ndoa inaendelea.
  13. Kwenye hili la dhamana kwa kila kesi lifanyike kwa washitakiwa wasio hatarishi, lakini kwa kesi za mauaji ya kukusudia, unyanganyi wa kutumia silaha na uhaini, kuzuiliwa mahabusu kuendelee mtu akijua kuwa kutoka ni ngumu possibility ya kujump bail ni kubwa au kuwadhuru key witness.
  14. Japo hapa natetea haki za watuhumiwa , pia naomba kuzingatia haki za wahanga wa uhalifu. Katika ulimwengu wa uhalifu kuna watu wabaya kupita kipimo. Just imagine unakuta mtu mzima umembaka mtoto wa miaka 2 na kumharibu vibaya sehemu zake za siri na pengine akamwambukiza HIV, mauaji ya kutisha , vitendo vya vikundi vya kihalifu kama panya road na mapanga yao wanapokuingilia na kukucharanga mapanga bila huruma na kumbaka binti yako au mkeo mbele yako na visa vingine vingi. Hao nao wasipate dhamana kwa vile wamepoteza sifa za haki yao kuwa huru.
  15. Ule utaratibu wa notification kwa makosa ya usalama barabarani, na kulipa faini za papo kwa papo, utumike pia kwenye vituo vya polisi, mwizi wa kuku akiri kuiba kuku, akubali kumlipa aliyemuibia na kulipa faini, kesi hiyo inaishia hapo hapo kituoni wala haina haja na kufikishwa mahakamani.
  16. Majaji wetu, kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana, nao wanapaswa kufanya kazi kama vituo vya polisi, mahospitali na dharura nyingine kwa saa 24. Kama ilivyo kwa madaktari wa zamu anapigiwa simu kukitokea dharura, kuwe na majaji wazamu saa 24/7. Nimeshuhudia hii Afrika Kusini, kila mtuhumiwa anapelekwa kwa hakimu wakati wowote hadi usiku wa manane, kama vile madaktari au vituo vya polisi.
  17. Criminal Justice System inahitaji kufanyiwa reform ili kuendana na wakati. Duniani kote magereza yako kwa ajili ya kutenga watu wabaya na jamii. Tujiulize toka kupata uhuru magereza mangapi yamejengwa ili yakidhi haja ya ongezeko la uhalifu. Wahalifu na uhalifu hatari kwa jamii unapoongezeka wahalifu lazima wataonekana wanajazana magereza
  18. Kwa upande wa sociological jurisprudence jamii yetu bado ina kisasi kingi. Kibaka tu wanawachoma moto. Je wale ndugu wataweza kumuacha salama mtuhumiwa anayedhaniwa kukatisha uhai wa mpendwa wao aidha kwa armed robbery au murder. Bado naamini reform ya jamii ianzie kwenye social justice system other than legal or criminal justice system. Malezi ya jamii, mfumo wa elimu juu ya haki jamii ili kuepuka visasi tuwafundishe waha, wajita na wakurya etc waache visasi vyao ya asili ili tuweze kupunguza mlundikano wa mahabusu ambao wengine wanahifadhiwa kuepusha kuthuriwa na wanajamii wanakoishi.
  19. Makosa kama ya economic offences kwanza watuhumiwa wanaweka tangible security wakiruka dhamana serikali itarecover kutoka kwenye security/bond. Pia wahujumu uchumi wengi ni active economic drivers wa wanajamii wao so kuwahold is an economic distortion kwa wao wenyewe na serikali inaua ile mifumo ya uchumi wao.
  20. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, Taifa litaponywa, haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami, tukianza na Mahakama.

pascomayalla@gmail.com

075427040
View attachment 1818080
  1. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, Taifa litaponywa, haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami, tukianza na Mahakama.

pascomayalla@gmail.com

075427040
View attachment 1825109

Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
View attachment 1825142
View attachment 1825139
View attachment 1825143
Hili jambo, tumelipigia Sana kelele, tumepandisha ma thread na mathreads, makala na makala hatimaye Leo kimefanyika kitu.

wa kilichofanyika leo, Ile Nolle ya Mbowe, hongera Sana DPP, utabarikiwa, aliyekutuma atabarikiwa, Tanzania tutabarikiwa. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana na haki ikaonekana imetendeka.

Mungu ibariki Tanzania,
Pasco
 
2. Heshimi Haki za binadamu ambazo zimeainishwa kwenye Katiba. Kuna uvunjifu wa haki za binadamu mdogo mdogo
Kwenye eneo hili la haki za binaadamu, Mama Samia, apewe kongole sana, huyu ni mpenda haki, muwaza haki, msema haki, mtenda haki.
Ameonyesha kwa kauli na matendo!.
Mifano iko mingi tuu ya kumwaga hapa nakupa mifano mitano tuu!, ukitaka 10, nakupa, ukitaka 20 nakupa
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Kwenye eneo la haki, so far Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendo, is the best of the best... ila sasa kwa kwa kadri siku zinavyokwenda, naona kama na yeye anaanza... itaendelea!, nitamalizia ...

P
 
TOKA MAKTABA :

6 February 2020

Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli, rais wa TLS atoa nondo kali:

Mfumo wa sheria za jinai ulioko sasa nchini Tanzania , hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji.

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

Dk. Rugemeleza Nshala ameishauri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo Haki Jinai, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.

18 September 2021
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu .

Azungumzia mazito kuhusu

  • Nolle prosequi / kufutiwa mashtaka bila kuelezwa sababu za msingi zaidi ya ofisi ya DPP kusema imeamua kutoendelea na mashtaka
  • Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP
  • Makubaliano kati ya raia na kitu kinachotisha kikubwa yaani raia asiishitaki serikali akiachiwa pia asidai fidia
  • Marekebisho ya sheria yanahitajika ili mahakama iweze kusikiliza haki ya dhamana na ikiwa inafaa mahakama ipewe mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa wakati Polisi na waendesha mashtaka wakiwa wanaendelea kusaka ushahidi
  • Watuhumiwa wengi wanaozea ndani ya mahabusu gerezani kwa muda mrefu wakati inadaiwa vyombo vinaendelea na upelelezi
  • Mtuhumiwa siyo mhalifu mpaka hapo atakapo pata haki yake kwa kuhukumiwa na Mahakama.
  • Hii ya mtuhumiwa kuhukumiwa na Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka au kiongozi yeyote ni uvunjifu wa haki za raia na katiba.
  • Wenye jukumu la kurekebisha mfumo huu Jinai Haki, ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake na bahati kuna wasomi bobezi waliopo ofisini , ni kama Mwanasheria Mkuu Jaji Dr. Feleshi, Waziri wa Sheria Prof. Palamagamba na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Wadau wengine kama TLS, Kituo cha Haki za Binadamu, Vyombo vya Habari na wananchi ni kupaza sauti na kupigia kelele mfumo huu mbovu wa Haki Jinai uliopo sasa hivi.
  • Polisi hawawezi kulaumiwa, wao Polisi hawana jukumu lolote bali kupiga saluti na kutekeleza amri na sheria hii mbovu inayoendesha Mfumo Haki Jamii ( Criminal Justice System) kama wanavyoelekezwa na viongozi wanaowaongoza jeshini na wanasiasa serikalini.
  • Watanzania tuamke toka dhamira zetu zilizo mfu, tupiganie haki hii wote kabisa bila kujali vyeo vyetu, vyama vya kisiasa, itikadi n.k

Rugemeleza Nshala, holds Doctor of Juridical Studies (S.J.D) from the Ivy league Harvard Law School. He holds a Bachelors of Laws Degree (LL.B) from the University of Dar es Salaam, Tanzania (his home country), which he obtained in 1993; the Masters of Laws Degree (LL.M) from Harvard Law School and Masters of Environmental Management (MEM) from Yale School of Forestry and Environmental Studies that he obtained in 1997 and 2007, respectively. Source : Harvard African Development Conference

Haki Jinai / Criminal Justice System

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI​

Imewekwa: Wednesday 15, June 2022

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
View attachment 2471512
Serikali imejipanga kuboresha Mfumo wa Haki Jinai nchini kwa kubaini changamoto na kupendekeza maboresho katika mnyororo mzima wa haki jinai. Hayo yamebainishwa katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau wa Haki jinai nchini. Kikao kazi hicho cha siku tano kimefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu leo tarehe 13 Juni, 2022 Jijini Dodoma.

Dkt. Kazungu amewataka Wadau wa haki jinai kujadili changamoto zinazoukabili mnyororo mzima wa haki jinai na kupendekeza namna bora ya kuboresha mfumo huo ili kujenga mfumo madhubuti wa sheria unaoaminika na jamii katika utoaji haki.

Maoni yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yatatumika kuboresha Andiko la Mapendekezo ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai Nchini kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi 2026/27.

Aidha, Dkt. Kazungu amesema mabadiliko ya mfumo wa haki jinai yamekuja wakati muafaka kwani hayo yamekuwa moja ya maono ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo

Source : https://www.sheria.go.tz/news/serikali-yajipanga-kuboresha-mfumo-wa-haki-jinai

Mkuu bagamoyo, asante kwa hii post, kwa ruhusa yako, naomba kuitumia kama mbolea kuboreshea baadhi ya mabandiko yangu ya kilio cha haki.

Natanguliza shukrani.

Paskali
 
Na Pascal Mayalla
Karibuni tena kwenye makala nyingine ya Kwa Maslahi ya Taifa kuhusu Kilio cha Haki Tanzania, leo ikiwa ni mfululizo wa makala za Kilio cha Haki Tanzania, tukiiangazia ofisi ya DPP, mada zinazotokana na uwepo wa kilio cha haki kwa Watanzania kutokana na kutotendewa haki na vyombo vya utoaji haki, Ujio wa rais SSH, umefufua upya dhima, ari na kasi ya haki kwa kauli zake na matendo ili kuwafuta machozi Watanzania na kuliponya taifa kwenye suala zima la utoaji haki.

Makala ya leo, ni ushauri wa bure kwa DPP afanye nini ili kuwatendea haki Watanzania,​

Ujumbe mkubwa ambao Samia anautuma Kwa vichwa ngumu ni

Ushauri kama huu wa changing the mindset ya watoa haki ili kuwatendea haki Watanzania, tuliutoa.
P
 
Back
Top Bottom