Wafanyakazi wa Leopard Tours kuandamana mpaka kwa mbunge Lema

malcom2

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
301
67
Kutokana na manyanyaso makubwa na mateso wanayoyapata pasipo msaada wafanyakazi hao wa Leopard tours wameamua kuandamana mpaka ofisini kwa mbunge wa Arusha mh. G. Lema kumfikishia kilio chao.

Chanzo: wafanyakazi.
 
Kutokana na manyanyaso makubwa na mateso wanayoyapata pasipo msaada wafanyakazi hao wa leopard tours wameamua kuandamana mpaka ofisini kwa mbunge wa arusha mh g.lema kumfikishia kilio chao.

Chanzo wafanyakazi.

Lema kwani kawaajiri cha msingi waende mahakamani maana lema naye ni mtumishi hajaingia mkataba na leopard tours
 
Mkuu, watu wa Arusha wamekuwa kama mazezeta vile. wanafanana na vijana wa kinondoni, makao makuu ya chadema. wanajitoa ufahamu kila kukicha
 
Mkuu ahsante kwa tetesi, ila ile ni kampuni binafsi wangekuwa na busara badala ya kuandamana wangeacha kazi; kwani ni lazima wafanye kazi hapo?

Washauri bure kuwa waache kazi ujumbe utaeleweka.

ONYO:

Usije ukawa wakala wa upumbavu dhidi ya kampuni hiyo usiyojua undani wake.
 
Mkuu, watu wa Arusha wamekuwa kama mazezeta vile. wanafanana na vijana wa kinondoni, makao makuu ya Tchadema. wanajitoa ufahamu kila kukicha
Kuwa mstaarabu, huo uzezeta uliwapachika wewe watu wa Arusha? Changia mada na sio kutukana watu
 
wako sahihi kabisa name hii inaonyesha ni jinsi gain wali yo na imani na mbunge wao manager waeacha viongozi wrote na kwenda KWA mbunge wao safi sana
 
LEOPARD TOURS ORDERS TANZANIAN GOVERNMENT.
ZUHER FAZAL maarufu kama FAZAL mmiliki wa LEOPARD TOURS mtanzania mwenye asili ya kiasia ajigamba kuipakata serikali ya Tanzania, aliyatamka kwa kinywa chake hivi majuzi alipokuwa akiwafokea wafanyakazi wake. Alisema hakuna wa kunifanya chochote nchi hii serikali. Kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binahadamu anavyowafanyia wafanyakazi wake ni dhahiri ameipakata serikali ya Tanzania.
Kutokana na vitendo hivyo na kauli hiyo ilituhuzunisha sana na kutukumbushia Mr.FAZAL alipomtukana waziri wetu wa ulinzi wa kipindi cha nyuma Prf. PHILIMON SARUNGI pale IMPALA HOTEL. Haikuwa siri waliokuwa eneo la tukio walishuhudia na habari hizi ziliandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari. Aliwekwa lokapu kwa masaa machache na kutoka. Alifanya alilojua(HELA) prf,waziri tena baba yetu akajifedhehesha kwa kukanusha kwenye vyombo vya habari. Tulikuwepo pale kikazi siku hiyo waziri akitukanwa,wahudumu wa hoteli nao walisikia, PROFESA akakanusha, leo hii akija Arusha ataiweka wapi sura yake? Inawezekana wale wahudumu wa hoteli hawajui Mr. Fazal alitoa nini ili ufuta ile kesi lakini sisi wafanyakazi wa Leopard Tours tunajua nini alitoa kwa familia ya PREFESA ili kuyamaliza. Mr.Fazal kama walivyo wahindi wengine hawana siri huropoka. Wahudumu wa hoteli ya Impala nao walisikia akitukanwa nao pia tulishawaambia ukweli jinsi kesi ilivyomalizwa na Mr. Fazal, hivi PROFESA utalala wapi, au kuja ARUSHA,IMPALA HOTEL hautokuja?
Hajaishia hapo kuwavua viongozi wetu nguo mbele ya wafanyakazi wake: Huropoka kuwa ana mkono mrefu na serikali hata Hotel yake mpya iliyopo Ndutu kuwa ni yake na KAGASHEKI aliyekuwa waziri wa utalii,tena alimuendesha kwenda kupewa hilo eneo.
Hujigamba kuwa hakuna wa kumfanya jambo lolote kwani wakuu wa serikali wengi ndiyo wameficha hela kwenye kampuni yake, kama vile LOWASA, OLENAIKO na wengine wengi.
Husema yeye ndiye anayekipa hela nyingi chama tawala. LOWASA bado hajawa rais wa nchi hii huyu Mr. Fazal anajitanua hivyi, je LOWASA akiingia IKULU? Si Mr Fazal utachinja watu!!.
Hakuna wa kufanya chochote kwa yeye ndiye anayeyatengeneza kwa gharama zake magari yote ya POLISI Arusha pamoja na kuyanunulia vipuli na magurudumu.

NYADHIFA ZAKE

1) MMILIKI WA LEOPADR TOURS
Ni kampuni ya kupeleka WATALII katika vivutio mbalimbali vya utalii nchini.
Ndiyo kampuni Arusha inayoongoza kwa unyanyasaji na ukiukwaji wa utu na haki za binadamu.
Kampuni pekee nchini iliyoajiri WANAJESHI WA KINEPAL( NEPOL ARMY) kama walinzi katika kampuni hiyo.
Ndiyo kampuni pekee isiyofuata sheria za nchi kama vile (a) Sheria za uhamiaji. (b) Sheria za Kodi. (c) Sheria za kazi. (d) Na sheria nyingine nyingi.
Kampuni hii inaongoza kwa kuiibia serikali mapato yake ikiwemo la mishahara ya wafanyakazi wake kutokatwa kodi sawia na malipo halali wanayolipwa, Mfanyakazi analipwa dola 700 isiyoonyesha kwenye document yoyote hicho kiasi bali kitakachoonyesha kwenye document ni Laki moja na nusu (150000)TSH.
Kampuni pekee inayotumika kama kichaka cha kuficha wageni wanaofanyakazi bila kufuata taratibu za uhamiaji. Hakuna Afisa Uhamiaji Arusha kwa Fazal – WANAJESH WA NEPAL,WAHINDI hawana working permit.
Wabunge wetu mmiliyo WAZALENDO na nchi yenu,mlioonyesha UZALENDO WA KWELI kwenye UFISADI MKUBWA na mzito kama ule wa ESCROW,EPA na mwingine wingi.
Wabunge Wazalendo na Kituo cha Haki za Binadamu tunawaomba sana kutofumbia macho UFISADI ULIOPO LEOPARD TOURS.

2) KATIBU WA TATO.
TANZANIA ASSOCIATION TOURISM OPERATORS – TATO
Mr.Fazal ndiye Katibu wa TATO, ni chama cha magwiji wa makampuni makubwa ya utalii nchini. Chama hiki kipo kwa ajili ya kutunga mbinu za kandamizi na za kinyonyaji katika Taifa hili. Kila serikali inapokuja na mbinu au sheria za kukusanya mapato kwenye sekta hii huwa TATO hupinga na kuwa wakali sana kwa wao huendesha biashara kwa faida kidogo.
TATO kipo kuhakikisha wao tu ndiyo watakaofaidi utalii nchini.
Magwiji hawa wameishauri serikali vibaya sana kwa manufaa yao binafsi; Suala la kulipia leseni ya utalii(TALA) kwanini TATO hupinga daima TALA kulipiwa kwa gari kama Kenya na siyo kwa kampuni?. Ilipiwe kwa gari ili serikali ipate mapato na kuweka usawa katika malipo siyo mwenye gari mbili analipa TALA sawa na mwenye gari mia.
Wameishauri vibaya serikali na kuwekwa sheria za kuanzisha kampuni kumgandamiza anayeanza ili waendelee kubaki wao tu. Mfano anatokea mfadhili anataka kumsaidia mtanzania nae aendeshe biashara ya utalii,atashindwa kutokana na sheria zilizopo siyo rafiki. Hawa magwiji walianza na gari moja alafu mbili na kuendelea, lakini leo wameishauri serikali na kuwekwa sheria ya kuanzisha kampuni ya utalii lazima uwe na gari zisizopungua tano.
Hawataki watanzania kuinuka na kufaidi mema ya nchi yao. Tunasema kuwa wao ndiyo chanzo cha sheria hizo kandamizi kwa Mr. Fazal kama Katibu wa TATO ndiyo eti mshauri wa rais kuhusu mambo ya utalii. Atamshauri nini zaidi ya kufutia kwao ili kuendelea kuinyonya serikali na watanzania kwa ujumla.

3) MSHAURI WA RAIS MAMBO YA UTALII.
Ni mshauri wa rais katika mambo ya utalii, hivi tumekosa washauri mpaka kuwaomba wakwepa kodi kumshauri rais? Atashauri nini kulipatia taifa pato?

[h=1]UKIUKWAJI WA UTU NA HAKI ZA BINADAMU NDANI LEOPARD TOURS:[/h] Sisi ni wanayakazi wa Leopard Tours tunakabiliwa na unyanyashaji na ukiukwaji mkubwa haki za binadamu toka kwa mmiliki wa kampuni hii.
Kutokana na kupungua kwa watalii nchini,pia na ma-group mengi ya watalii kutoendelea kufanya safari na LEOPARD TOURS,mmiliki wa kampuni hii aliamua kupunguza wanyakazi wake haswa WAONGOZA WATALII(SAFARI GUIDES). Akabuni mbinu na vitisho ili aweze kupunguza wanafanyakazi pasipo kutotulipa haki zetu akiwatumia wanajeshi wake wa NEPOLI na baadae jeshi la polisi(RPC ARUSHA) pamoja na watumishi wengine wa umma.
Unyanyasaji na ukiukwaji wa waziwazi wa haki za binadamu ulianza pale tulipoanza kuhoji kuhusu itakuaje kuhusu haki na malipo. Mfano NSSF zetu kwani zimekua hazipelekwi sawia kama inavyotakika kisheria. Tulihoji mambo mengi ikiwemo kutokatwa P.A.Y.E katika mishahara yetu ndipo alipokuwa mkali sana mmiliki huyu na kusema tuende popote hakuna wa kumfanya chochote katika nchi hii kwani serikali kaiweka kiganjani.
Tuliendelea kujadiliana la kufanya pasipo kufikia muafaka kati yetu(Wafanyakazi). Kutokana na uwoga wetu tulishindwa kabisa tutafanya nini kama serikali tunayoitegemea ndiyo kaiweka kiganjani. Baadhi yetu tuliamini kuna suluhu,wakati tukiwa bado hatujafikia la kufanya;kwa nyakati tofauti wenzetu(wale wenye misimamo) walianza kuitwa oficini kuhojiwa kwani wanahamasisha wafanyakazi kudai haki zao.Wiki hiyohiyo walianza kufungiwa kule geriji Chini (Njiro) na kupewa mateso makali kutoka kwa (wanajeshi wa NEPOL ambao ni walinzi wake LEOPARD TOURS ) wakiwalazimisha waandike UONGO kuwa katika makaratasi ya SAFARI RETIREMENT za miezi ya nyuma kulikuwa na risiti za kugushi(Zikiwemo za Malipo ya Oldupai Gorge).
Baada ya ndugu na jamaa kulijua hili na kuhoji kama kuna masuala ya kugushi kwanini asilipeleke polisi ndipo mateso yalihamia ofici ya huku juu Kijenge. Alisema hakuna wa kumtisha na polisi kwani hata RPC wetu anamwita yeye Boss.
Alinyanyua simu akampigia RPC ARUSHA huku akituringia serikali yenu ipo hapa akituonyesha kiganja chake. Ni ajabu alimuita RPC aje, na alikuja dakika zilezile hapa oficini (LEOPARD TOURS) akamuamuru RPC awaweke ndani(LOKAPU) baadhi yetu mpaka pale yeye(Fazal) atakapuamua. Waliwekwa LOKAPU zaidi ya siku tano pasipo dhamana wala kufunguliwa dalaja la mashtaka.
Ndugu na jamaa pamoja na wanasheria tulilifuatilia kwa karibu ndipo RPC akajigundua anatumiwa vibaya na huyu tajiri,siku iliyofuata walipandishwa mahakamani na kupelekwa magereza pasipo dhamana. Tulijiuliza ni kosa gani hilo lililosababisha wasipewe dhamana.
Baada ya hili suala kuwa kubwa na kuvuta Public awareness dhamana iliachiwa ila kwa masharti magumu sana(Dhamana ya Mali ya milioni 400), akidai walimsababishia hasara ya million 800 kwa mwezi. Ndugu na jamaa tulifanikiwa kutimiza masharti hayo.
Tunajiuliza ni kosa gani kubwa hilo lao la kunyimwa DHAMANA na baadae MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA? (Hawa wachahe kujua haki zao na kuhoji ndiyo itumike nguvu kubwa kiasi hicho ili kuwaziba midomo na kuwaonya wengine wasijaribu kuhoji!!)
Bado twajiuliza ni nani mwenye kosa hapa? Ni Fazal anayekwepa kuwawekea wanfanyakazi wake NSSF asilimia sawia na misahara yao au ni mfanyakazi anayehoji kwanini?
Bado maswali hayapati majibu ni kosa sisi kuhoji kwanini MSHAHARA wetu haukatwi kodi (P.A.Y.E).
Bado twahoji nani alistahili kuwa LOKAPU ni aliyeajiri WANAJESHI WANEPALI au ni hawa wafanyakazi?
Bado tunajiuliza aliyestahili kuwa LOKAPU huyu mfanyakazi aliyekabidhi SAFARI RETIREMENT yake ikiwa sawa miezi iliyopita,wakakaguwa na kuafiki,leo kabadili na kuweka anazodai ni za kugushi,ni nani hapa alistahili LOKAPU aliyebadili au?.Kweli serikali kaiweka kiganjani.

WATUMISHI WA UMMA WALIHAMISHIA OFIC ZA UMMA LEOPARS TOURS
Na hili alitudhibitishia kuiweka serikali yetu kiganjani kama siyo mfukoni kwa kuwapigia na kuwaamuru waja oficini kwake(LEOPARD TOURS).
i. Mkuu wa mkoa Arusha – RC,DC.
ii. Wakuu wa jeshi la polisi – RPC, OCD, Na wengine tulioshindwa kujua vyeo vyao.
iii. Mkurugenzi wa Tanzania National Park(TANAPA) ALLAN KIJAZI.
iv. Wakuu kutoka Ngorongoro Conservation Area – Melita
v. Wakuu kutoka Olduvai Gorge.
WATUMISHI HAWA WA UMMA walifika japo kwa nyakati tofauti kutegemea na umbali waliotoka ili kulitii amri ya Mr.Fazal ya kumfuat(a Mr.Fazal) ofisini kwake LEOPARD TOURS kushughulikia masuala binafsi ya kampuni hiyo.
Jeshi la police ndilo lililotia aibu kabisa kwa kuwa wao ndiyo walipewa ofisi hapa Leopard Tours kututisha na kutushinikiza kukubali kuwa tulikuwa tukigushi malipo ya kiingilio cha Oldupai Gorge. Kulikuwa hakuna mjadala katika hili aidha uchague kukubali usamehewe au kukikataa kuna gari ya polisi nje ya geti la Leopard Tours linakungoja. Hakuna anaeyependa mazingira ya kule polisi kila mmoja wetu alijikuta akikimbilia kusaini kukubaliana na anavyotaka Mr.Fazal. Haya yote yalikuwa yanafanyika mbela ya RPC-ARUSHA chini ya polisi wenye silaha. Matisho yalikuwa makubwa kutoka kwa Mr.Fazal & Kamal kuwa atakayekataa kusaini atamfunga mpaka pale atakapoamua yeyemwenyewe(FAZAL) ndipo atatolewa.

Haya yote alikuwa akiyafanya ili kutuonyesha alivyo na nguvu kubwa na kusikilizwa na watumishi wetu wa umma(Serikali yetu). Tuligundua Mr.Fazal anao uwezo wa kuwaagiza watumishi wetu wa umma chochote pasipo kujali anavunja sheria(LEOPARD TOURS ORDER TANZANIA GOVERNMENT).

ALIKUWA KADHAMIRIA KUPUNGUZA MISHAHARA NA WAFANYAKAZI PASIPO KULIWALIPA STAHIKI ZAO.
Baada ya kutumia nguvu kubwa sana kufanya udhalimu wake wa kulazimisha wafanyakazi wake kusaini kukubaliana na matakwa yake yeye kwa manufaa yake binafsi baada ya kuyumba kwa biashara ya utalii kutokana na Ebola. Haya hapa chini ndiyo yaliyotokea baada ya kutimia lengo lake la kuhakikisha wafanyakazi wote wamesaini na kukubaliana na njama zake kuwa waliibia Leopard Tours.
i. Wote tulilazimishwa bila usimamizi wa polisi awamu hii, kuandika barua ya kuacha kazi(RESIGNATION LETTER).
ii. Kuomba kazi upya kwa malipo atakayotaka yeye ili kufidia hasara aliyopata.
iii. Mshahara wa December na January tulikuwa hatujalipwa kwa hiyo tutapewa nusu mshahara.
iv. Kuanzia February mshahara tutakuwa tunakata kiasi Fulani cha hela mpaka pale atakapokuwa amemaliza kufidia hasara ya million 800 aliyokuwa akipata kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.
v. Kwa wale atakaoendelea kuwahitaji kazi hawaruhusiwi kuacha kazi na kuenda kufanya kazi pengine,kwa wale asiyowahitaji tayari hawapo kazi. Hivi majuzi mwenzetu alikaza roho na kwenda kurizaini aliwekwa ndani(LOKAPU) mpaka atakaporuhusu aachiwe.
Unyanyasaji na ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu ni mkubwa sana hapa LEOPARD TOURS
Tunaomba msaada wabunge wetu na wanasheria kwa ujumla ili sheria ichukue mkondo wake anayestahili kuwajibika awajibike VIONGOZI WA UMMA wanatumiwa vibaya kwa maslahi binafsi dhidi ya unyanyasaji,uvunjivu wa sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kuna uvunjivu mkubwa sana hapa Leopard Tours ikiwepo Matusi mazito ya nguoni, kulipishwa vipuli na magurudumu ya magari,na mengine mengi sana

Tutashukuru sana kama tutusaidika.
Wafanyakazi wa Leopard Tours,
Asanteni.
 
Mbona umesema lowasa akichukua nchi hivi hamuwezi kucommet kitu bila kumtaja lowasa..!? na kwanini mkimbilie kwa lema kama sio umbumbumbu??! idara ya kazi hakuna? au mnapenda umbea, lema kashindwa kutekeleza ahadi zake alizozitoa huko ndio ataweza..!?
 
Wewe acha use***nge kwenye Ishu serious. Nini alishawahi kusaidiwa na Idara ya Kazi. Lema ni mbunge na hakuna ubishi kwamba lema ndio mwakilishi na ndio mtu wa kuwasemea wananchi matatizo yao kwenye hii serikali kuziwi
 
Wacha kutoa mbwa mtoni wewe kilaza, kuandika yenyewe hujui, unajua idara ya kazi ina maana gani?! kama hujui uliza boya wewe, mwambie na yale matatizo ya nyumbani kwako!
 
LEMA anahusikaje hapa?

Nendeni mahakamani au idara ya Kazi.

Acheni kuyafanyia maisha yenu siasa!
 
Wacha kutoa mbwa mtoni wewe kilaza, kuandika yenyewe hujui, unajua idara ya kazi ina maana gani?! kama hujui uliza boya wewe, mwambie na yale matatizo ya nyumbani kwako!

Nadhani una kaufinyu tu ka uelewa ndo mana unataka kuchanganya siasa na uhalisia, jumbo lililokuwa sio mambo ya lema ni kwamba waongoza utalii Hawa wana madai yao na yanaonekana ni ya mwingine ndo maana wamemchagua mbunge wako awe mwakilishi wao.
 
Wewe ndio mwenye uelewa mdogo, aliyesema tumeteua lema ni nani kama sio wewe? mimi nimekwambia kuna idara ya kazi mwende pale mkatoe malalamiko yenu, acha mambo ya siasa kwenye kazi..!!
 
Nadhani una kaufinyu tu ka uelewa ndo mana unataka kuchanganya siasa na uhalisia, jumbo lililokuwa sio mambo ya lema ni kwamba waongoza utalii Hawa wana madai yao na yanaonekana ni ya mwingine ndo maana wamemchagua mbunge wako awe mwakilishi wao.

Wafanyakazi wa makampuni ya utalii kwa kawaida ni wazito kujiunga na vyama vya wafanyakazi kama CHODAWU ndiyo maana wanakosa watetezi.
 
Ila nyie si mlitengezeneza vitabu bandia vya risiti mkala hela yake sasa mbona mnalalamika jf badala muende mahakamani. Lema hatawasaidia
 
Wafanyakazi wa makampuni ya utalii kwa kawaida ni wazito kujiunga na vyama vya wafanyakazi kama CHODAWU ndiyo maana wanakosa watetezi.

Hivi wafanyakazi ndiyo wanatakiwa kujiunga na chama cha wafanyakazi au chama ndiyo kinatakiwa kuwa na tawi sehemu ya kazi? Ujue waajiri hua awajengi mazingira rafiki kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi. Na ukikuta sehemu zenye tawi la chama cha wafanyakazi, basi baada ya kutetea masilai ya wafanyakazi, uongozi wa chama unatetea utalawa. Viongozi wachache wa vyama vya wafanyakazi wenye kujitambua ndiyo wanatetea wafanyakazi.
 
Choma mali zake zote.... gari weka chumvi
Kwenye engine...vunja vioo mahali popote
Gari la leopard likionekana..fazal kiburi kiburi kitakuponza subiri
 
Back
Top Bottom