Wadau hii imekaaje?

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Habari wana Jf, kuna jambo kidogo naombeni mawazo yenu, Mimi ni mwajiriwa wa taasisi moja, mwaka jana serikali ilivyopandisha mishahara mwezi wa saba, taasisi yetu na yenyewe ikatupandishia (mimi ni mwajiriwa wa mkataba) sasa mkataba umeisha wananipa mwingine wa 2yrs ila eti wanasema hakutakuwa na changes zozote kwenye salary yangu coz walishanipandishia mwaka jana, Je hii ni sahihi? nikubali mkataba mwingine kwa mshahara wa mwaka jana?
 
nduguyangu hata kama wanakudhurumu wewe endelea kufanya kazi hiyo huku ukitafuta nyingine inayolipa zaidi ila usije ukaacha ajira yako kwani kuacha ajira yako ujue unaihujumu familia yako! pata kwanza ndipo utafute ajira nyingine!
kumbuka ukipata ajira nyingine hata kama unamkataba ukitaka kuacha unaandika barua ya kuacha kazi ndani ya masaa 24 halafu unawapa mshahara mmoja!
mie nakushauri jaza hata kama unaona unaonewa! lakini uendelee kutafuta ajira nyingine huku unafanya hiyo kazi!
huo ndiyo ushauri wangu (kumbuka ushauri si maamuzi unaweza kuufuata au kuacha na hata ukinijurisha kuwa hukuufuata mimi siwezi kujisikia vibaya)
 
Mkuu, Waswahili wana misemo mingi na yenye maana. Haba na haba hujaza kibaba. Usiwache m,bachao kwa msala upitao.
 
Mkuu nchi yenyewe unaiona inavyoenda tena mimi naona kama umepata bahati kupandishiwa mshahara mwaka jana na kuongezewa mkataba wa miaka miwili, wewe endelea na kazi kaka kuna watu wamesoma mpaka leo awajapata kazi na wapo radhi kupokea mshahara mdogo lakini nafasi za kazi ni ngumu kupata
 
Back
Top Bottom