Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Jumuisho: Kikwete ndio kinara wa hilo zigo la Dowans

Hii haswaa ndiyo ukweli wenyewe na ndio maana kuna watu hata huko CCM wanaoeleweka kwa misimamo wanaogopa kuwa wazi kupinga malipo haya simply b'coz inaweza kuwa interprated ni kumpinga JK. Na hii pia inatuthibitishia kwamba JK ni dikteta huko kwenye vikao vyake na likely ni mtu wa visasi kama ilivyowahi kusemwa huko nyuma.
 
Labda wanaamini hiyo bil 94 wakiipata wanaweza kununua nguvu yote ya Umma, na kuusambaratisha upidhani kabla 2015
 
Jumuisho: Kikwete ndio kinara wa hilo zigo la Dowans. JK ndio Rais, Ngereja na Werema wasingekuja na kauli zao bila ya baraka za Ikulu. Pia JK ni mwenyekiti wa CC, kwa hiyo CC isingekuja na kauli ile ambayo inachimba kaburi la CCM na huku wakiona wazi kwamba wananchi hawataki kusikia habari hizo.
Keil hapo you can connect the dots easly. Nasisitiza RA is just the agent. Mtakapo jua who is really behind RA kwenye Kagoda ndipo mtakapo jua who is behind RA kwenye Dowans na mtashindwa kushangaa na kubaki midomo wazi!.
 
WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA UCHUNGUZI TANZANIA
TUTENDEENI HAKI KWA DOWANS HARAKA SANA!!!


Watanzania, inaelekea GUDUDU wa ajabu tena wa kutisha mno mpaka ikaifanya CCM, pamoja na hasira zetu hizi zote, ituone wa afadhali kidogo wa kukandamiza zaidi kuliko kusema kutokulipa GUDUDU Dowans.

Waandishi wetu wa habari za uchunguzi za uchunguzi wakatueleze kiundani zaidi kwamba ni kitu gani GUDUDU iliomo ndani ya huyu mdeni hewa Dowans inayomtisha saaana Dr Kikwete na bench zima ya CC ya CCM kiasi cha kuona ya kwamb wakiue Chama Cha Mapinduzi na au wananchi wa Tanzania wengi zaidi kusafirishwa kwenda kwenye umasikini wa kufa mtu kuliko kutokulipa Dowans??

Ndugu Said Kubenea, Ayub Rioba, Mbaraka Islam, Maggid Mjengwa na 'This Day' team, nyote hapo hamna haki ya kukalia na kutunyima haki yetu ya kujua GUDUDU kitu kinachotisha ajabu kiasi hicho ndani ya Dowans kwa CCM na serikali yake, kiasi kwamba hata kama ingelikua halali kulipwa, ni sharti malipo yake iwahishwe haraka hata kabla ya wadeni wetu wa zamani kama Wazee watumishi wa Afrika Mashariki.
 
WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA UCHUNGUZI TANZANIA
TUTENDEENI HAKI KWA DOWANS HARAKA SANA!!!


Watanzania, inaelekea GUDUDU wa ajabu tena wa kutisha mno mpaka ikaifanya CCM, pamoja na hasira zetu hizi zote, ituone wa afadhali kidogo wa kukandamiza zaidi kuliko kusema kutokulipa GUDUDU Dowans.

Waandishi wetu wa habari za uchunguzi za uchunguzi wakatueleze kiundani zaidi kwamba ni kitu gani GUDUDU iliomo ndani ya huyu mdeni hewa Dowans inayomtisha saaana Dr Kikwete na bench zima ya CC ya CCM kiasi cha kuona ya kwamb wakiue Chama Cha Mapinduzi na au wananchi wa Tanzania wengi zaidi kusafirishwa kwenda kwenye umasikini wa kufa mtu kuliko kutokulipa Dowans??

Ndugu Said Kubenea, Ayub Rioba, Mbaraka Islam, Maggid Mjengwa na 'This Day' team, nyote hapo hamna haki ya kukalia na kutunyima haki yetu ya kujua GUDUDU kitu kinachotisha ajabu kiasi hicho ndani ya Dowans kwa CCM na serikali yake, kiasi kwamba hata kama ingelikua halali kulipwa, ni sharti malipo yake iwahishwe haraka hata kabla ya wadeni wetu wa zamani kama Wazee watumishi wa Afrika Mashariki.
 
Hawawezi kuwa systematic kwa kuwa kila mtu anapalilia mraba wake, na wao pia wanasoma alama za nyakati.

Wapo wanajenga hoja kwa kuangalia Urais wa 2015 na Ubunge wa 2015.

Wapo wanaotetea malipo kwa kuwa walibebwa na mafisadi kwenye mbio za kuingia mjengoni kwenye uchaguzi wa 2010. Lakini hata ukiwa na mahela kiasi gani, bado huwezi kupambana na nguvu ya umma ambayo imepewa elimu ya uraia na imeelewa adui yao ni nani.

Ndiyo maana kila mtu anakuja na tamko la kivyake. Nape Nnaye anasema haamini kama lile tamko alilotoa Chiligati lilikuwa ni la CC anayoifahamu yeye, anahisi labda Bob Chiligati alijitengenezea version yake. Kwa lugha nyepesi ni kwamba Nape ametofautiana na CC.

UVCCM wanasema serikali isilipe mpaka kwanza RICHMOND ajulikane ni nani na ikiwezekana ashitakiwe.

Mwakyembe/Sitta wanasema hakuna kuilipa Dowans, kampuni ambayo ni ya kitapeli.

Wabunge wa CCM wanasema ikiwezekana serikali isikubali kulipa na watafute njia za kisheria za kumaliza kadhia hiyo.

Jumuisho: Kikwete ndio kinara wa hilo zigo la Dowans, maana hana mashaka ya kujipendekeza kwa wapiga kura kwa kuwa anajua huu ni muhula wake wa mwisho, so hata CCM ikipoteza uchaguzi wa 2015, yeye hatakuwepo. JK ndio Rais, Ngereja na Werema wasingekuja na kauli zao bila ya baraka za Ikulu. Pia JK ni mwenyekiti wa CC, kwa hiyo CC isingekuja na kauli ile ambayo inachimba kaburi la CCM na huku wakiona wazi kwamba wananchi hawataki kusikia habari hizo.

Tumshukuru Kikwete kwa kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, maana ametusaidia sana kuimrisha upinzani na pia kuimaliza CCM. Ile ndoto kwamba CCM inaweza kutawala kwa miaka 100 ijayo, inapotea taratibu na sasa life span ya CCM inazidi kuwa fupi sana.
Keil umetoa analysis nzuri, ni wachache sana ndani ya CCM wanaoona/jua faida ya kuilipa Dowans kwa hiyo wanaona kuliko kupoteza imani kwa wapiga kura wao kwa kitu wasichofaidika nacho ni bora isilipwe kabisa they have nothing to lose.
 
Hii haswaa ndiyo ukweli wenyewe na ndio maana kuna watu hata huko CCM wanaoeleweka kwa misimamo wanaogopa kuwa wazi kupinga malipo haya simply b'coz inaweza kuwa interprated ni kumpinga JK. Na hii pia inatuthibitishia kwamba JK ni dikteta huko kwenye vikao vyake na likely ni mtu wa visasi kama ilivyowahi kusemwa huko nyuma.
Nyambala, nakubaliana na wewe kwa kiasi. Kuwa mtu wa msimamo ni strength of character kusimamia kile unachoamini no matter what, kama walivyofanya Sitta na Dr. Mwakiembe. Sasa hao unaowaita wana misimamo lakini wanaogopa kumpinga JK kwa kuhofia visasi, ndio msimamo gani huo?!. Huu ni udhaifu, weakness na unafiki wa kisiasa kumuunga mkono mdomoni kwa kitu usichokiamini moyoni.
Niliufuatilia mjadala wa Richmond bungeni mwanzo hadi mwisho, nikakumbuka jinsi watu kama kina Ole Sendeka, Anne Kilango, Selelii na wale waliojiita makananda dhidi ya ufisadi walivyojipambanua kwa michango yao moto na yenye ncha kali na makali kama ya upanga wa makali kuwili!.

Lakini ile e siku Sitta anauhitimisha rasmi mjadala ule pale Bungeni, sikuamini hao makamanda walivyonywea kama vifaranga vya kuku vilivyo lowa maji! na Ole Sendeka aliposimama kuchangia nikajua huyu ndie mwanamume wa shoka, Morani wa Kimasai hawezi kukubali kufa kibudu, nikijua atatoa msimamo wa kupinga mambo hayawezi kumalizwa kirahisi hivyo, lakini alipochangia tuu ndipi alinichosha na kuniacha hoi kabisa alipounga mkono hoja!.

ilicomment humu humu kuwa ule ulikuwa ni utumbo mkubwa zaidi heri wenzake walioamua kujinyanazia kimya. Nilikumbushia lile swali la Mzee Mwanakijiji " Makamanda walioko CCM, wanapigania nini?".

Kwa misimamo hiyo kana wa Ole Sendeka, ndipo nikaelewa pia kuna wabunge machachari, kelele nyingi kumbe ni debe tupu tuu!.

Baada ya mbwembwe zote mle bungeni kwenye suala hili mbona wote wamenywea na kubaki Sitta tuu na Mwakiembe?!, ndio maana nasema, ukiondoa wachache wenye msimamo, wengi wa wabunge wa CCM hawana msimamo ni wanafiki tuu na waganga njaa kwa lengo la kichumia tumbo!.
 
Baada ya mbwembwe zote mle bungeni kwenye suala hili mbona wote wamenywea na kubaki Sitta tuu na Mwakiembe?!, ndio maana nasema, ukiondoa wachache wenye msimamo, wengi wa wabunge wa CCM hawana msimamo ni waganga njaa tuu wenye unafiki kwa lengo la kichumia tumbo tuu!.

Pasco, ondoa shaka kuna maendeleo fulani weekend hii iliiyopita ambayo itawarudisha watu kwenye mstari.
 
Pasco, ondoa shaka kuna maendeleo fulani weekend hii iliiyopita ambayo itawarudisha watu kwenye mstari.
Asante Mzee Mwanakijiji, wakati tukiwasubiria hao watakaorudi kwenye mstari, Nyambala kasema wana msimamo, bado nauliza wale waliojipambanua kama makamanda, leo hii wako wapi na hiyo misimamo ndio misimamo gani?.
 
Pamoja na jitihada za viongozi wa chama kuendelea kusisitiza mshikamano ndani ya chama, bado suala la dowans litaendelea kuwagawanya. Najua yaliyomo kwenye mioyo wa wabunge wa ccm siyo yanayotamkwa kwenye vinywa vyao hadharani. Nimekutana na kuongea na wabunge watatu wote wa ccm. Kila mmoja anapinga tena sana msimamo wa serikali wa kutaka kuilipa dowans lakini wanaogopa kutamka waziwazi wasije wakaanza kuandamwa na viongozi wao. Kwa hiyo, unaweza kushangaa asilimia zaidi ya 90 ya wabunge wanapinga suala hili lakini hawapo tayari kuonekana wanapinga waziwazi. Huo ndiyo unafiki wa viongozi wetu tuliowachagua kutuwakilisha kwenye masuala nyeti kama hayo yanayomgusa moja kwa moja mwananchi wa kawaida.
 
Wazee,
Kama kuna wakati ambapo watanzania wamepata fursa murua ya kupima udhati wa jk na serikali yake katika kupambana na ufisadi nchini, basi ni wakati huu wa sakata la dowans. Lakini vilevile, suala la dowans limetupatia sisi wapiga kura fursa ya kuwapima viongozi wetu hasa wabunge kama kweli ni wazalendo. Ngoja tusubiri hali itajavyojiri bungeni mwezi Februari, tuone ni nani atawasaliti wananchi na ni nani atawatetea wananchi dhidi ya ufisadi huu mkubwa katika historia ya nchi yetu.
 
Sasa hao unaowaita wana misimamo lakini wanaogopa kumpinga JK kwa kuhofia visasi, ndio msimamo gani huo?!. Huu ni udhaifu, weakness na unafiki wa kisiasa kumuunga mkono mdomoni kwa kitu usichokiamini moyoni.

Mkuu Pasco, have we forgotten kwamba tunazungumzia wanaCCM, na what u have said ndiyo haswaa mojawapo ya sifa ya mwanaccm these days.

Lakini mimi nnaowazungumzia ni watu kama Warioba forget about Ole Sendeka, mama Kilango and the likes.
 
I thank God for Dowans, it have helped us to get direction for next election (whether 2015 or before that), and the coming bunge will really easy selection. We will not need to hear campaign because we will know who sheeps are and who wolves in sheeo clothing are!

Thank you oh God for Richmond and Dowans!
 
CCM yanywea msimamo wa wabunge wake kuhusu Dowans Wednesday, 26 January 2011 20:18

Exuper Kachenje
SAKATA la kampuni ya kufua umeme ya Dowans limeishika pabaya CCM baada ya jana kueleza kuwa pamoja na maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho kutaka Dowans ilipwe, inakubaliana na msimamo wa mkutano wa wabunge wote wa CCM uliotaka sakata hilo lifuatiliwe ili kupunguza deni au kutolipa kabisa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alieleza hayo jijini Dar es Salaam jana alipoulizwa msimamo wa CCM kutokana na hoja ya wabunge wa chama hicho kutofautiana na msimamo wa Kamati Kuu ya CCM Iliyosema ipo haja ya kul;ipwa kwa deni lote.

Hivi karibuni, katika taarifa yake baada ya kikao chake, pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ya CCM (CC), ilisema kwa kuwa suala la Dowans ni la kisheria na inakubali Serikali kuilipa Dowans fidia ya Sh 94bilioni, lakini baada ya kesi zilizofunguliwa na wadau mbalimbali nchini kupinga kampuni hiyo kulipwa kusikilizwa.

Uamuzi huo wa CC ulikuja siku moja baada ya Umoja wa Vijana wa chama hicho UVCCM kuitaka serikali isiilipe Dowans ikipingana na CCM.

Lakini Jumamosi iliyopita, Kamati ya wabunge wote wa CCM iliyokutana chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, katika kikao chake mwishoni mwa wiki iliyopita ilipendekeza kuwa serikali isilipe kabisa fidia hiyo au deni lipunguzwe.

Kufuatia utofauti huo wa misimamo, jana Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliliambia gazeti hili kuwa uamuzi huo wa wabunge umetia msukumo maamuzi ya CC na kutaka vita hiyo ya Dowans ipiganwe mahakamani.

Chiligati alionekana kugeuka na kueleza kuwa uamuzi wa CC na ule wa wabunge yote yana lengo moja, akisema kuwa wanakubali maamuzi ya wabunge kwa kuwa yanaimarisha uamuzi wa CC.

"...'We must read between the lines', ninataka kusema kuwa lazima tukubali kuwa sote tunapigania jambo moja, lakini tukumbuke kuwa suala la Dowans ni la kisheria, lazima tuheshimu uamuzi wa mahakama ukikataa unafungwa,"alisema Chiligati.

Aliongeza kuwa:"Maamuzi ya wabunge yanatia msukumo uamuzi wa CC kwani yanataka kufuatwa kwa sheria na ndiyo sote tunavyosema hata CC na lengo letu ni moja ili kupunguza mzigo kwa Watanzania;
Lengo ni moja lazima tupigane vita ya Dowans mahakamani na hatuwezi kusema hatukubali kwani suala lenyewe ni la kisheria lazima uende mahakamani."

Alisema ni jambo jema kwa waliojitolea na kutaka kufuatilia suala hilo ili deni lipunguzwe au Dowans isilipwe kwani kimsingi deni hilo la Dowans ni mzigo mzito kwa Watanzania.

"Wabunge waliojitolea kufuatilia suala hilo hawakukosea kwani wanajua suala hilo ni la kisheria na wote tunakubali kwani kimsingi deni la Dowans ni mzigo mzito kwa wananchi," alisema.

Hata hivyo alieleza kuwa kimsingi hakuna anayefurahia deni hilo au kulilipa fedha hizo kwa kuwa ni mzigo mkubwa huku akisistiza kwamba 'vita ya Dowans' lazima ikapiganwe mahakamani.

"Hakuna anayefurahia kulipa fedha zote hizo (Sh94bilioni), hakuna anayesherehekea kuilipa Dowans," alisema Chiligati




Comments




0 #1 MR. ANZA 2011-01-27 07:34 JAMANI MBONA CHILIGATI NI KIGEUGEU? BAADA YA KUBANWA NA WABUNGE ANAJIDAI CC WALISEMA SUALA LA DOWANS LIPIGANIWE MAHAKANI WAKATI WOTE TUNAJUA CC WALIKUBALI DENI HILO LILIPWE LOTE..SHAME UPON YOU CHILIGATI..WATANZANIA HATUDANGANYIKI TENA..HAKUNA KUILIPA DOWANS..
 
TAMADA yatangaza maandamano


na Hellen Ngoromera


amka2.gif
SIKU chache baada ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunukuliwa wakitoa kauli zinazoashiria dhahiri kwamba serikali italipa fidia kwa Kampuni ya Dowans (T) Ltd, jana Chama cha Uzalishaji na Maendeleo nchini (TAMADA) kimetangaza kufanya maandamano ya amani ya wafanyabiashara ndogo ndogo hadi Ikulu ili kumshinikiza Rais Kikwete asitishe malipo ya fidia kwa kampuni hiyo.
Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara mwishoni mwa mwaka jana ililiamuru Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) lililo chini ya serikali, kulipa fidia ya sh bilioni 94 kwa Dowans baada ya kulitia hatiani kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu.
Wakitoa tamko lao kwa vyombo vya habari jana, viongozi hao wa TAMADA walisema kwa sasa wapo katika mchakato wa kuandaa taratibu za kisheria na wakishazikamilisha wataandamana kutoka jengo lao la Machinga Complex hadi Ikulu.
"Maandamano haya ni ya wafanyabiashara wadogo ambao ndio wako katika dimbwi la umaskini, tumepanga kuandamana mwezi mmoja kutoka sasa.
"Haiwezekani Dowans ilipwe wakati kuna watu wana hali mbaya na wanatia huzuni mahospitalini," alisema Mwenyekiti wa TAMADA, Abel Mwakabenga.
 
PHP:
"Maandamano haya ni ya wafanyabiashara wadogo ambao ndio wako katika dimbwi la umaskini, tumepanga kuandamana mwezi mmoja kutoka sasa. 
 "Haiwezekani Dowans ilipwe wakati kuna watu wana hali mbaya na wanatia huzuni mahospitalini," alisema Mwenyekiti wa TAMADA, Abel Mwakabenga.

Hizi siyo sababu za kupinga DOWANS ilsilipwe bali sababu halisi ni kuwa TZUO ya DOWANS inakiuka sheria za nchi hii na ilitolewa kwenye mazingira ya kifisadi tu..................
 
Back
Top Bottom