Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Pls posts zingine zinajirudia bila sababu! Pls kabla hujapost pitia angalau posts zilizo tangulia, otherwise it is becoming monotonous! Hii post ilikwepo humu asubuhi ya leo.
 
Wabunge wa CCM watakubali kupiga kura ya kutokuwa na Imani na RAISI na serikari ya chama chao? DOWANS is a tricky game, sijui watatoka vipi?
 
Hapakuwa na haja ya maneno marefu... Kuna kitufe cha kuripoti ambacho pamoja na mambo mengine kinawasaidia Mods kuunganisha mabandiko yanayojirudia!
 
Watakoma kulilia urais wakati uwezo wao mdogo na IQ pungufu kabisa....ikulu si pa kukimbilia ona sasa wanatafuta kulipa fedha za kampeni walizokopeshwa....EPA hii imegonga mwamba!!!halipwi mtu hapa...
 
Halipwi mtu hapa mpaka kieleweke. Tumechoka nchi yetu kufanywa shamba la bibi kila kukicha.

Tatizo kila mtu yupo anasema ''halipwi mtu hapa mpaka kieleweke''..mara..''issue hii haikuptia kwenye baraza la Mawaziri....''. Yaani ni vilio tuuuu na hakuna YEYOTE anayechukua hatua zaidi ya kulalamika kwenye vyombo vya habari.

DOWANS watalipwa and we will revert to our business....as usual! Very sad.
 
Tatizo kila mtu yupo anasema ''halipwi mtu hapa mpaka kieleweke''..mara..''issue hii haikuptia kwenye baraza la Mawaziri....''. Yaani ni vilio tuuuu na hakuna YEYOTE anayechukua hatua zaidi ya kulalamika kwenye vyombo vya habari.

DOWANS watalipwa and we will revert to our business....as usual! Very sad.

Mkuu u sounds like u got a lion share on DOWANS! very sad where is ur patriotism?
 
Bila maandamano nchi nzima kushinikiza JK na genge lake la mafisadi kuachia ngazi au Bunge kuwafungashia virago vyao ....................we are doomed.....................

Democracy is messy young man. Stick with it and it will deliver. Haya maandamano and blah blah will have a net negative effect on the ultimate goal. Which is Maisha bora kwa kila mtanzania ie Economic Development.

Acheni kujibu hoja kishabiki. Bungeni mko 40, halafu mnajifanya kutoa hoja za kutafuta umaarufu. Mwambie huyu Kafulira apeleke hoja bungeni to ban imported synthetic fibers and subsized pamba kutoka marikani ili wakulima wa kibondo wapate hela ya ukweli. Otherwise aache uhanithi wa kutafuta umaarufu kuleta hoja ambazo zitatupotezea muda with nothing in return.
 
Democracy is messy young man. Stick with it and it will deliver. Haya maandamano and blah blah will have a net negative effect on the ultimate goal. Which is Maisha bora kwa kila mtanzania ie Economic Development.

Acheni kujibu hoja kishabiki. Bungeni mko 40, halafu mnajifanya kutoa hoja za kutafuta umaarufu. Mwambie huyu Kafulira apeleke hoja bungeni to ban imported synthetic fibers and subsized pamba kutoka marikani ili wakulima wa kibondo wapate hela ya ukweli. Otherwise aache uhanithi wa kutafuta umaarufu kuleta hoja ambazo zitatupotezea muda with nothing in return.[/Q

Selemani, kwanza kabisa kuwa mwangalifu na lugha kaka, hapo kwenye nyekundu utata mtupu, But kubwa zaidi hata kama CCM wanawabunge wengi hili ni swala linalohusu National interest, hatuwezi kuweka tofauti zetu za itikadi and come together na bunge kuiwajibisha serikari? Ilitakiwa kuwa hivyo kwenye swala muhimu kama hili la DOWNS, lakini wabunge wa CCM wamekwisha anza kunyamazishwa na pinda amewapa semina juzi ya wao kuendelea kuwa rubber stamp wa serikari, this was to be expected kwani CCM sio wawakilishi wa wananchi hivyo kama wanapewa two sides to choose kati ya upande wwa serikari au wananchi basi wabunge wengi wa ccm watasimama na kuheesabiwa upande wa serikari na kumwacha mwananchi na mpiga kura wake akigagaa.

Hivyo basi hicho ndo tunataka kitokea, kwa kafulila kuwasilisha hoja ya kutokuwa na Imani na serikari then wabunge wa CCM wasimame upande wa serikari wahesabiwe hicho ndicho kitakachotokea hata kafulila analifahamu hilo na watu wote wanaojua siasa hiyo ni possition ambayo mwanasiasa yoyote hataki afikie hapo, then ikiwa hivyo CCM watakuwa wamepigwa bao kubwa sana, kwani watawapa rungu wapinzani la kuwatandika mpaka 2015. Kinachofanyika sasa hivi kuwapelekea mashambulizi na wao wanazuia goli lisiingia kwa kunawa mpira ndani ya penalt box.

Leo ndo nimeelewa Selemani hujui siasa kabisa unasema Kafulila anatafuta sifa wakati he is taking the fight to CCM! wewe hukuona Tea Party movement walivyomfanyia OBAMA na few months ago amepoteza Congress kwa Republican, Na kitendo cha Kafulila kutoa msimamo mkali unasaidia to sana for their base and party faithful to get FIRED UP! stay focusedand involved on the process, Sasa kama CCM wataleta mizengwe kuzima hoja isijadiliwe bungeni kwa ubabe basi kuwatoa nishai kwa Nguvu ya Umma ni muhimu.
 
Akisoma maazimio ya semina hiyo Kaimu Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama, amesema kamati yao imeishauri serikali kutafakari kwa makini hukumu hiyo na kutumia njia za kisheria kuangalia uwezekano wa kutolipa fidia hiyo.

"Kuhusu deni la Dowans kwa TANESCO la sh 94 bilioni kamati ya wabunge wa CCM wameitaka serikali kupitia njia za kisheria itazame upya suala hilo kwa nia ya kutafuta uwezekano wa kuwaepushia Watanzania mzigo huu," alisema Mhagama.

Source: Tanzania Daima.
 
Wabunge wa CCM walipata joto ya jiwe ya kueleweka kwenye uchaguzi ulioisha. Hoja kuu iliyokuwa inawatesa ni ufisadi na jinsi walivyoshindwa kutetea maslahi ya wananchi wakiwa Mjengoni. Kwa kuwa bado wana hamu ya kuendelea kuwa mjengoni, na kama wana akili timamu hawawezi kuunga mkono malipo hayo.
 
Inaonekana kuna watu wachache tu ndani ya CCM wanaoelewa faida za malipo kutoka Dowan, waliobaki wanaburuzwa tu ili kulinda itifaki ya chama
 
Kumbe sometimes kelele zinasaidia keep on keeping on Chadema matunda yenu yanaanza kuonekana hata kabla ya kuingia madarakani.
 
Kwa kweli siku hizi siwaelewi CCM wanavyoendesha mambo yao they are not systematic as it was used to be.

Hawawezi kuwa systematic kwa kuwa kila mtu anapalilia mraba wake, na wao pia wanasoma alama za nyakati.

Wapo wanajenga hoja kwa kuangalia Urais wa 2015 na Ubunge wa 2015.

Wapo wanaotetea malipo kwa kuwa walibebwa na mafisadi kwenye mbio za kuingia mjengoni kwenye uchaguzi wa 2010. Lakini hata ukiwa na mahela kiasi gani, bado huwezi kupambana na nguvu ya umma ambayo imepewa elimu ya uraia na imeelewa adui yao ni nani.

Ndiyo maana kila mtu anakuja na tamko la kivyake. Nape Nnaye anasema haamini kama lile tamko alilotoa Chiligati lilikuwa ni la CC anayoifahamu yeye, anahisi labda Bob Chiligati alijitengenezea version yake. Kwa lugha nyepesi ni kwamba Nape ametofautiana na CC.

UVCCM wanasema serikali isilipe mpaka kwanza RICHMOND ajulikane ni nani na ikiwezekana ashitakiwe.

Mwakyembe/Sitta wanasema hakuna kuilipa Dowans, kampuni ambayo ni ya kitapeli.

Wabunge wa CCM wanasema ikiwezekana serikali isikubali kulipa na watafute njia za kisheria za kumaliza kadhia hiyo.

Jumuisho: Kikwete ndio kinara wa hilo zigo la Dowans, maana hana mashaka ya kujipendekeza kwa wapiga kura kwa kuwa anajua huu ni muhula wake wa mwisho, so hata CCM ikipoteza uchaguzi wa 2015, yeye hatakuwepo. JK ndio Rais, Ngereja na Werema wasingekuja na kauli zao bila ya baraka za Ikulu. Pia JK ni mwenyekiti wa CC, kwa hiyo CC isingekuja na kauli ile ambayo inachimba kaburi la CCM na huku wakiona wazi kwamba wananchi hawataki kusikia habari hizo.

Tumshukuru Kikwete kwa kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, maana ametusaidia sana kuimrisha upinzani na pia kuimaliza CCM. Ile ndoto kwamba CCM inaweza kutawala kwa miaka 100 ijayo, inapotea taratibu na sasa life span ya CCM inazidi kuwa fupi sana.
 
WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA UCHUNGUZI TANZANIA
TUTENDEENI HAKI KWA DOWANS HARAKA SANA!!!


Watanzania, inaelekea GUDUDU wa ajabu tena wa kutisha mno mpaka ikaifanya CCM, pamoja na hasira zetu hizi zote, ituone wa afadhali kidogo wa kukandamiza zaidi kuliko kusema kutokulipa GUDUDU Dowans.

Waandishi wetu wa habari za uchunguzi za uchunguzi wakatueleze kiundani zaidi kwamba ni kitu gani GUDUDU iliomo ndani ya huyu mdeni hewa Dowans inayomtisha saaana Dr Kikwete na bench zima ya CC ya CCM kiasi cha kuona ya kwamb wakiue Chama Cha Mapinduzi na au wananchi wa Tanzania wengi zaidi kusafirishwa kwenda kwenye umasikini wa kufa mtu kuliko kutokulipa Dowans??

Ndugu Said Kubenea, Ayub Rioba, Mbaraka Islam, Maggid Mjengwa na 'This Day' team, nyote hapo hamna haki ya kukalia na kutunyima haki yetu ya kujua GUDUDU kitu kinachotisha ajabu kiasi hicho ndani ya Dowans kwa CCM na serikali yake, kiasi kwamba hata kama ingelikua halali kulipwa, ni sharti malipo yake iwahishwe haraka hata kabla ya wadeni wetu wa zamani kama Wazee watumishi wa Afrika Mashariki.
 
Inaonekana kuna watu wachache tu ndani ya CCM wanaoelewa faida za malipo kutoka Dowan, waliobaki wanaburuzwa tu ili kulinda itifaki ya chama

Wanaojua umuhimu wa hayo malipo ni hawa:
JK, Rostam Aziz, Ngereja, Werema, Nazir Karamagi aliyehamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans na Lowassa aliyehakikisha Richmond inapata mkataba japo haikuwa na uwezo wa ku-deliver.
 
Back
Top Bottom