Wadada nisaidieni hapa.

Jana kuna mtu alisema hawezi divorce sababu ya stigma inayo wakumba divorcees. No matter how unhappy the marriage gets, people have to hang on :(

Sijui nielezeeje hapa unipate vizuri, kuna ugumu sana kumwacha mtu mliyeishi naye let say miaka 10, ni tofauti na kuacha bf/gf

Khaaa! Hivi huwa kuna stigma eeh?...

Hawa ndio wale wanaishi watu wapendavyo na sio wao wapendavyo...chakufia kwenye ndoa ni nini?

Waulize mama zetu na baba zetu cha kufia kwenye ndoa nini watakuelewesha labda. Hasa kwa mwana mke akiolewa anabeba bendera ya ukoo. Akiachika utasikia, watoto wa Mzee X huwa wanaachika. Utakuwa umedrag down the whole family, unadhani Mzee gani atakubali hili? Achia mbali watu wa mbali, shughuli kubwa huanzia kwenye familia yako mwenyewe.

Sasa hapo ndo utagundua vile wengi wetu hatuishi maisha yetu bali ya watu wengine...
Tunafikiria tu hivi jamii itanielewaje mimi nikiachana na mume wangu? Yaani hujIjali binafsi unapitia mangapi kwenye hiyo ndoa na maumivu mangapi unayapata.....

Oh well...in that case one has to hang on in there!

Refer nilivyomjibu Sweetlady
Lakini on top of that hasa kwa mwanamke anakuwa na hofu ya kuacha watoto wake maana by default setting watoto wanabaki na baba. Akifikiria kuwaacha waje walelewe na mama wa kambo kuna hof inaingia inabidi kubaki na kuvumilia tu.

Stigma ipo. Na bora hata ukipewa wewe talaka watu wanaweza kukuonea huruma, lakini uidai wewe!

Utaambiwa "mwanamke mpumbavu......."

Na inawezekana watu wa familia yako ndio wakakusulubu zaidi.
Hebu fikiria kwenye jamii zinazopokea mahari kubwa, ukiachika maana yake ile mahari yote irudishwe.
Let say ulitolewa mahari ng'ombe 50, ni mzazi gani anataka zirudishwe eti kisa umeshindwa kuvumilia mume Kacheat?
Na unaweza kuta polygamy is allowed.

But somehow ni bora tabu ya stigma, inaisha as soon as you live a happy life again. Tabu ya ndoa mbaya is for life!
Ni kweli, lakini sio rahisi kihivyo, labda generation ya watoto wetu, lakini kwa sasa bado % kubwa haiwezi vunja ndoa kirahisi hivi.
 
HAPO MIMI NAKATAA. USIMGEUZE MWANAUME ATM machine. Na huu ndo udhaifu wa wanawake, wanahisi wao ni wa kupewa tu, nawapongeza wale wanaotoa

Aaaa mwanamme bakhili apigwe na chini tu, manake wengine ni wabakhili hata kwa pesa yako mwanamke! Ukiitumia anakufanyia bughdha
 
Do you think men cheat because they don't like their wives?

What do you mean 'mambo yote yanaenda sawa'? ni mambo gani yanawaweka pamoja kama sio mapenzi? na akisha gawa penzi huko nje what is left? If you man material things I believe you can have your own, if you mean time spent together you can have that from friends and family. sasa hayo 'mambo yote' ni nini tena kama sio trust, respect, love and all the things he has just blown up kwa ku-cheat? Na hapa hatujasema vya magonjwa.
 
@ Konnie, I understand sio rahisi kabisa, na sifagilii divorce. Ila naamini kuna kitu kilicho sababisha uingie ndani ya ndoa. kwangu mimi ni mapenzi. nikiona yameisha basi ni bora tuachane. Sasa kama kwako hicho kitu kilibadilika mkiwa ndani ya ndoa, na leo unagundua macho ya watu, mazowea na watoto ndio msingi wa ndoa yenu, basi baki tu sababu hata akicheat hajaharibu hivyo vitu. Ila mimi kama mimi nadhani siwezi kubali.
 
russian, kama ananicheat ila nakuwa nae ninapomuhitaji, hana ukorofi ndani ya nyumba na anawajibika vizuri kama mume au baba wa watoto. Sina tatizo hapo.
Nimekusoma. I don't agree but I get it. Kumbuka kuna magonjwa pia... huogopi kufa?
 
Katika maisha ya ndoa, ni vitu vingapi mwenza anaweza akavunja ahadi?

Mfano umeugua kwa muda mrefu, mume akakurudisha kwenu kwa sababu tu anaona usumbufu kukuuguza, na ukiangalia resources zote anazo lakini anaendelea kuwa mwaminifu utaachana naye?

Men like women cheat for all sort of reasons, but by cheating you dishonour your promise (to be faithful). You are no longer trustworthy and you have disrespected your partner.
 
Nimekusoma. I don't agree but I get it. Kumbuka kuna magonjwa pia... huogopi kufa?

naogopa kufa ila kufa kupo tu, matokeo mabaya yatakayotokana na kucheat sitoyavumilia.
Kwanza nikuulize, ni wanandoa wangapi wenye utaratibu wa kucheki afya mara kwa mara? Kwani ukimuacha wakati kashakuambukiza inakuwaje hapo?
 
Katika maisha ya ndoa, ni vitu vingapi mwenza anaweza akavunja ahadi?
Mfano umeugua kwa muda mrefu, mume akakurudisha kwenu kwa sababu tu anaona usumbufu kukuuguza, na ukiangalia resources zote anazo lakini anaendelea kuwa mwaminifu utaachana naye?
Ataonaje usumbufu kuniuguza? Hivi ndoa maana yake nini?
 
naogopa kufa ila kufa kupo tu, matokeo mabaya yatakayotokana na kucheat sitoyavumilia.
Kwanza nikuulize, ni wanandoa wangapi wenye utaratibu wa kucheki afya mara kwa mara? Kwani ukimuacha wakati kashakuambukiza inakuwaje hapo?
Mi ninavoishi naamini he doesn't cheat, so we live faithfully wote. Bahati nzuri tunafanya kazi in the same company na tunapima regularly (and publicly) as a couple to promote the culture in the company. Maybe nje ya mazingira haya ningekua sipimi as often, who knows? Halafu ukisha ambukizwa, you increase your chances of having aids by recontaminating yourself mara kwa mara. bora uondoke tu, it is never too late.
 
katika mahusiano ni bora kuamini kuwa mwenzio hafanyi, itasaidia hata wewe kuwa mwaminifu. Ukikosekana uaminifu ndio mambo ya usaliti yanaanza. Hii mitazamo yetu hutegemea sana na mazingira tuliyoishi na tunayoishi. Kwa wapenzi ambao huishi mazingira yaliyojaa cheating hujikuta wanaona ni kawaida.
 
Hii mitazamo yetu hutegemea sana na mazingira tuliyoishi na tunayoishi. Kwa wapenzi ambao huishi mazingira yaliyojaa cheating hujikuta wanaona ni kawaida.

Kwa hiyo mtazamo wako wa kutokumuacha mwanaume wako endapo atakusaliti unatokana na mazingira uliyoishi?
 
Back
Top Bottom