Wachina 150 katika mradi wa barabara ya km 65 je wote hawa ni wataalamu au ni siasa?

Ndugu wana Jf, naomba niwasilishe hoja hii kwenu, nilfanikiwa kufika katika mradi huo nilichokiona, hata mhesabu trip za mchanga katoka china, wasimamizi wa vibarua ni wachina halafu waliowengi hawana elimu. Je, swali sasa wanaingiaje inchini hawa, kw vigezo gani. maana kazi wanazofanya watanzania wapo wengi sana naamini. Uhamiaji wanafanya nini au ni kugonga mihuri tu bila kujua kwa vile wachina hawa niliambiwa kwa rushwa wanaongoza, maana wamegundua sumu ya mtanzania ni rushwa. hawa wachina wapo mradi wa barabara tanga horohoro. naomba mulijadili hili la sivyo ajira zote zinaenda kwa wageni wakati wazawa wenye fani hizo wapo

Vitendo vya baadhi ya Watanzania wenzetu vimesababisha hasara kwa makampuni ya kigeni..tuendelee kulalamika kwa sababu ndicho pekee tunachomudu.
 
Swali hilo elekeza wizara ya kazi na uhamiaji wao ndio watoa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Pia waweza kuuliza kupitia website ya serikali utajibiwa

idara ya kazi ndo washenzi kabisa. jana nikiwa mtaani nilipata skendo yao nilichoka, sitaki hata kuwasikia. Wahindi huwa hawatoi mkataba kwa kukwepa kulipa michango ya mwajiri hifadhi za jamii. Sasa hawa idara ya kazi, wanajifanya kwenda kutaka kuwasaidia hao vibarua wa wahindi waliofanya kazi kwa mda hata wa mika 10. wanauliza maswali wanachukua contact zao na wanaahidi kumpelekea mhindi mahakani kwa kushindwa lkuwa na taarifa sahihi za wafanyakazi wao.

wanachokifanya baada ya kuchukua kila taarifa mhimu, wanapitia mlango mwingine, uso kwa uso na mhindi, wanaanza kumtishia na sheria yao hiyo huku wakionesha vitambulisho vyao, baada ya hapo mhindi hataki kufika mahakamana, anavuta dro, anaangusha hata milion moja, jamaa wanatoka kimyakimya.

Mhindi anaanza kumtafuta nani mchawi, anakusakizia kesdi ya wizi ili apate sababu ya kukufukuza bila hata kukulipa hata ile posho anayotoa, huku idara ya kazi wakiendelea kujenga nyumba na kununua magari tu. washenzi wakubwa kabisa
 
Samahani; hivi unajuaje kama hawana elimu?
Kwa mtazamo wangu, naona wameamua kufanya hivyo ili kulinda cement, mafuta nondo na vitu vingine visiibiwe. Maana waTZ tumezidi; twataka barabara nzuri lkn lzm tuifanyie ufisadi!

Wakandarasi wetu wakipewa kazi (maengeneer), hawakubali kupigwa jua matokeo yake kila kitu kinaenda hovyo hovyo!

Sipingi ulegelege wa serikali, lkn l think the Chinise r trying to keep their job by making sure that next time they will get contracts.
 
Mkuu hata mimi nilishangaa mradi wa barabara toka Korogwe hadi Handeni kila baada ya kilometa moja unakumbana na wachina 4 mpaka 10 nikajiuliza hivi Tanzania tuna kwenda wapi ?.

Vibarua wa kitz ni wezi na wachakachuaji.
Nilijionea mwenyewe wakati wa ujenzi wa barabara ya Senjele Tunduma.
 
Wiizi kwa wataalam mpaka vibarua Engineer anaanzia kwanza saa nne yuo break point anakunywa supu then anaenda ofisini site anaingia saa saba saa tisa anaenga angalia game au lunch mpaka kesho....Eng ana supervise kwa simu...wakipata kazi za mkoani
ndio hatoki kabisa dar anatuma vijana"kibarua" kwenda kuangalia site yeye kakaaa tu hapo dar....

Tufike wakati tupeane ukweli wizi wizi kwa watanzani umezidi na tamaa....Kijana kamaliza chuo kikuu anataka baada ya mwaka awe
anajenga na range anaendesha atafanyaje kazi huyu kama sio kuwaza kuiba na kupata extra cash isivyo halali...wizi wizi tu.
 
Hata mimi nisingeajiri Watanzania labda kwa kufagia barabara tu. Kwa kweli Watanzania wamezidi katika wizi. Juma lililopita tulisikia yule contractor wa Denmark anayejenga barabara Rukwa kuwa ameibiwa sana.
 
Ni kweli kwa hili inashangaza uwingi wa Chinese kwa kipande hicho cha barabara ,kwa haraka ina maana kwa suala la usimamizi kila mchina pale anasimamia si zaidi ya nusu km.
Hata hivyo uzalendo wa kutaka kuona tunapata vitu vizuri ikiwemo barabara bora ndiyo unatufikisha hapa,kwani wizi wa hata mafuta ya gari kwa wafanyakazi na vibarua kwa kisingizio kuwa malipo ni madogo,kama kazi unaona haikufai si ukatafute nyingine tu kama zinapatikana kirahisi na kwa malipo uanayotaka.
Leo hii wachina wamejaa kila mahali tena kwa wingi wakati hizo zingekuwa ni kazi za WATZ,na hakuna anayeongea kwa hili tutaishia kusema kuwa ni wezi je hao hawatuibii kwa kutunyima ujuzi,na kujazana hata katika fursa za WATZ wenyewe,ifike wakati kila MTZ ajue kuwa TUNATENGENEZA VYA KWETU ILI TUFAIDI WOTE NA SI KUFAIDI KABLA YA KAZI ILI WAFAIDI WACHACHE
 
Nasema hivi, Laiti Serikali ingekuwa makini, nchi hii tatizo la ajira ingekuwa ni ndoto.
Ajira nyingi zimeshikiliwa na wageni ambao wengi wao sio wataalamu, kazi hufundishwa na wabongo.

Nenda kiwanda cha nguo URAFIKI kuna Wachina mpaka wakulima bustani ya mboga mboga.Wakati walitakiwa kuwa na Wachina 5-8 lakini wapi kama 40 hivi.
 
sawa acha waje cha msingi ni kuhakikisha wanaondoka mradi ukikamilika,
pia serikali iongeze bei ya viza kwa wachina
 
Wanaona ni bora wasimamie wenyewe kwani sisi waswahili tukipewa kazi mara nyingi tunapiga bao na uvivu mwingi. Angalia sehemu ambazo waswahili wamepewa kazi ni vituo bubu/sheli za mikono za mafuta yaliyoibwa. Halafu usisahau china ni cheap labour
 
Back
Top Bottom