wachezaji wa taifa stars wavunja ukimya kupitia globu ya jamii
KILICHOTOKEA IVORY COAST KATI YETU (HARUNA, ATHUMAN, KEVIN, BONI, AMIR, NURDIN) NA KOCHA MARCIO MAXIMO
UTANGULIZI
Kwanza kabisa tunatoa pongezi kwa mtandao huu wa jamii na Tunaomba balozi utufikishie haya tulionayo kwa jamii ya watanzania wote.
Katika maelezo yetu haya tutaeleza kila mmoja ya walioandikwa hapo juu kilichomtokea kwa kituo kabla hatujaondoka na baada ya kuwa kwenye mashindano, tunafanya hivi kwa kuwa hatuna uwezo wa kuongea na waandishi wa habari ana na pia tunaogopa kama binadamu tusije tukatereza kitu ambacho kinaweza kikatuletea madhara katika shughuli zetu za kila siku (Kucheza Mpira).
Hivyo kwa ushauri wa ndugu na jamaa zetu tukaona ni bora tutumie tovuti yetu hii ya jamii kuwaomba msamaha watanzania wote na pia kuwapa haki ya kujua nini hasa kilichotokea na pia tunaomba wanahabari watumie ujumbe wetu huu kuwafikishia habari wananchi wote wa Tanzania ili waweze kuelewa undani wa sakata zima hili na tunaomba endapo tutakacho kieleza hapa kitakuwa sio kweli atoke mbele ya jamii na kutukosoa tuko tayari kwa hilo.
ATHUMAN IDD (Chuji)
Itakumbukwa kuwa wakati nikiwa na timu yangu ya Yanga niliumia nyama za paja kitu ambacho kilisababisha Dakitari wa timu kushauri kuwa nipumzike wakati nikiendelea na matibabu ili niweze kupona vizuri kitu ambacho nilikifanya na nikaamua kwenda kwa mama yangu Tanga kupumzika wakati nikiendelea na matibabu.
Siku chache baadae niliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambapo niliripoti lakini sikuweza kufanya mazoezi na timu kwa sababu ya tatizo langu la paja na hata Dakitari wa timu alithibitisha hilo, lakini baada ya muda mfupi nikaanza mazoezi mepesi pamoja na timu na mwisho nikawa sawasawa japo sio 100%.
Muda mfupi kabla ya kwenda kwenye mashindano Kocha mkuu akaniita na kuniambia kuwa ananichukua mimi kwenda Ivory Coast kwa kuogopa kelele za watu lakini sitocheza kitu ambacho sikukielewa lakini pia sikutaka kukubali kwani niliamini naendelea vizuri na baada ya siku chache nitakuwa sawasawa 100% kwahiyo kocha ataweza kunipanga.
Tulipofika kwenye mashindano niliongeza bidii ya mazoezi ili kumshawishi kocha kuwa niko sawasawa 100% lakini hilo halikueleweka nikaendelea kubaki benchi bila maelezo ya kujitosheleza kwanini niko benchi hasa mechi ya pili tuliocheza na Ivory coast nilikuwa niko tayari kimwili na hata kiakili kwa aslimia 100 kucheza mchezo ule lakini sikupangwa.
HARUNA MOSHI (Boban)
Kucheza kwenye mashindano makubwa kama yale imekuwa ni ndoto ya kila mchezaji duniani kwahiyo kupata nafasi kama ile huwa ni bahati na kila mtu huwa anajitahidi kuonyesha kiwango chake chote ili ikiwezekana apate nafasi ya kwenda kucheza mpira wa kulipwa popote duniani kwani kunakuwa na wawakilishi wa vilabu mbalimbali vya nje kuja kuangalia wachezaji wanaoweza kuwafaa.
Siku ya mechi ambayo tulicheza na Ivory Coast nilipangwa lakini nakiri nilicheza chini ya kiwango ila tu naomba watu waelewe kuwa haikuwa hivyo kwa makusudi kwani ilikuwa ni nafasi yangu ya kuonekana hivyo ilitokea kwa bahati mbaya sana na ninasikitika kwa hilo.
Baada ya mechi tukiwa kwenye mkutano wa wacheza kocha alinisema sana kupita kiasi (kwa karibu dk15 hivi) kitu ambacho hakikunifurahisha na kama hivyo haitoshi kwa muda wote toka siku hiyo nikawa hata nikimsalimia haitikii wala hataki kuniangalia machoni kwa kweli ni kitu ambacho kiliniumiza sana katika muda wote niliokuwa mashindanoni.
KEVIN YONDANI
Na mimi pia nakiri kuwa katika mechi ya kwanza nilicheza chini ya kiwango lakini kama alivyosema Boban kuwa ile ilikuwa ni jukwaa la sisi kuonekana duniani kwamba tunaweza endapo tukipewa nafasi.
Kwa hiyo kutokana na presha ambayo kwa kweli ilinizidi nikajikuta kuwa nimepania sana mpaka nashindwa kucheza kwa kiwango kile ambacho ninakifiria kichwani kwangu.
Baada ya mechi kwenye mkutano wa wachezaji kwa kweli hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa kocha wetu kiasi cha kushindwa hata kuvumilia na kunipa nafasi nyingi na hata kuongea au kusalimiana na mimi ilikuwa haiwezekani kitu ambacho nadhani haikuwa sawa nilistahili kupewa nafasi nyingine niweze kufanya kile ambacho kila mtu alikitarajia kutoka kwangu.
AMIR MAFTAH
Kwa upande wangu mimi kosa langu kubwa ni kuwa karibu na Athuman kwa hiyo na mimi nikajikuta nimeingizwa kwenye mkumbo huo, lakini ikumbukwe kuwa mimi na Athuman tumekuwa tukila na kulala pamoja toka wakati wa Serengeti Boys. Kwa hiyo n iwatu ambao yeye anapokuwa na matatizo kama haya mimi najisia angalau kumwambia neno hata moja ambalo litamfariji kwasababu ndie mtu ninemjua vizuri kuliko mtu mwingine kambini na siwezi kumtelekeza leo hasa wakati ambapo anahitaji kuwa na mtu wa karibu.
Kwangu mimi hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana kiasi cha kutopangwa na hata kuwekwa kwenye list ya wachezaji wa akiba.
NURDIN BAKAR
Kama ilivyokuwa kwa Amir na mimi kosa langu kubwa ni hilohilo la kuwa karibu na Athuman na mimi pia nikaingizwa kwenye mkumbo huo, lakini Mimi, Amir na Athuman tulikuwa kulala pamoja Serengeti Boys, Simba na hata sasa Yanga kwahiyo niwatu ambao mmoja wetu anapokuwa na matatizo tunakaa kama kitu kimoja kuongea na pia ifahamike kuwa hata wazazi wetu wanafahamiana kwahiyo tunapoongea ni kama watoto wa familia moja, lakini baada ya kuona kuwa kocha hafurahii uhusiano huo nikaona wacha nijitoe kwa muda na ndio angalau nikapata nafasi ya kucheza.
MWINGINE
Haya yaliyotokea pia yamumuhusisha Godfrey Boni ambaye sijui ni kwanini Kocha aliamua kumuingiza kwenye sakata hili labda anaweza kueleza vizuri (Kocha) endapo akiulizwa.
MATUKIO YA IVORY COAST
Sisi wachezaji ambao tulikuwa katikati ya sakata hili yalitukuta yafuatayo:
Tulitolewa kabisa kwenye Program ya mazoezi ya timu tukawa tunafanya mazoezi wenyewe pembeni (kwa wale waliokuwepo wanaweza kuwa mashahidi wa hili).
Tulitolewa kwenye mazungumzo ya timu kwa sababu kocha alisema anataka kuzungumza na wachezaji wake tu, ikabidi sie tutoke waongee.
Kocha alimwambia Katibu kuwa sisi asiotutaka turudshwe nyumbani ndege ya kwanza itakayopatikana kitu ambacho katibu hakukubali na hata Waziri alipoambiwa kasema yeye ndio kiongozi wa msafara kwahiyo ndie anaeamua ni nani anarudi na nani anabaki kwahiyo hakuna mtu atakae rudi nyumbani kabla ya mashindano kuisha.
UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM
Baada ya kufika uwanja wa ndege waziri Mkuchika alituita (Boban na Chuji) na kutuuliza kilichotokea tukamueleza yote bila kubakiza.
Baada ya hapo tukaamua kuondoka kurudi makwetu kitu ambacho watu wengi waliona kuwa sio sawa kwa hiyo kwa ajili yao tunawaomba radhi kwa hilo lakini ikumbukwe kuwa sisi ni binadamu na yote yaliyotokea Ivory Coast yalitutesa kwa kipindi chote tulichokuwa huko tukaona hatuna hata haja ya kuwa na watu ambao hawakutaka kuwa na sisi, kifupi ni kwamba hatukutaka kuwa wanafiki na kuvaa tabasamu la plastiki.
MWISHO
Tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Katibu wa TFF Frederick Makalebela na Mkuu wa msafara Mh. Muhammad Seif Khatibu wa kutumia busara ya hali ya juu wakati wote wa mtafaruku huu na tunawaambia kuwa huo ndio moyo wa kimichezo na kizalendo.
Tunaimani endapo wakiendelea hivi basi Nchi yetu itafika mbali kwa Tanzania ni Kubwa kuliko mtu binafsi awae yeyote Yule.
Hayo ndio yaliyotokea Ivory Coast na tunaomba mzee wa tovuti ya jamii uwasilishe kilio chetu kwa watanzania na tumeamua tutoe leo kabla ya wenzetu kuondoka kwenda mashindanoni Misri na kama kuna mtu yeyote anasema kuwa haya tuliyoandika sio kweli basi awasilishe maoni yake ili watanzania wajue mbivu na mbichi.
Unaweza kuwasiliana na sisi kuhusu hili kwa email (KAPUNI) Ila tunaomba usiichapishe hii email address kwenye mtandao wa jamii.
Asanteni sana
Haruna;
Athuman;
Kevin;
Amir;
Nurdin;