Wachezaji wa nje wanafeli kwa sababu hawajui uzito na historia ya vilabu wanavyokuja kuchezea

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,130
7,900
Kwa historia za vilabu vya Simba na Yanga, ni rahisi sana kuchukua mchezaji kutoa pembe yoyote ya Tanzania na atakuwa anajua moja kwa moja uzito wa nafasi aliyopewa.

Hii ni tofauti kwa wachezaji wa nje. Mchezaji wa nje anaweza kuwa ameisikia sikia timu fulani ikisumbua sumbua ila ule uzito wa kuichezea Simba au Yanga hauwezi kumuingia moja kwa moja.

Nadhani hizi timu inahitaji kutoa pindi la kama wiki moja kwa mchezaji mpya wanayemsajili toka nje. Apitishwe kwa wazee huko wampe mastori ya kitambo, wajue watu wanakufaga kwa hizi timu.

Hawa kina Babakar, Jobe na Freddy wanakuja asubuhi, jioni wanapewa jezi wanaambiwa ingia uwanjani uipambanie timu, watajuaje machungu ya mashabiki? Naamini hili ndiyo lilikuwa linamsumbua Baleke, hakuwahi kujua ukubwa wa Simba.

Nakumbuka Pacome Zouzoua alipokuja Yanga hakucheza moja kwa moja, tofauti na wengine aliokuja nao kipindi kimoja hadi zikaanza tetesi kuwa wamepigwa, leo hii anakwenda sambamba na aliowakuta katika kuipigania timu. Unadhani walikuwa wanamfanya nini kina Mzee Mpili?

Hivyo hivyo kwa timu ya Taifa, unachukua mchezaji huko Ulaya unasema ana vinasaba vya Tanzania, hujawahi hata kumlisha ugali dagaa au ugali harage ukamwambia hiki ndiyo chakula cha asilimia kubwa ya Watanzania, wewe unampa tu posho yake na jezi akaipambanie bendera, unategemea nini? TFF walishindwa kuwafanyia hata media tour ya siku moja wachezaji wapya katika vyombo vya ndani ili Watanzania wawajue, unawapeleka tu katika mashindano makubwa kama AFCON waiwakilishe nchi. Bibi yangu aliyeko kule Namtumbo atamuombeaje mchezaji ambaye hamjui hata jina?
 
Back
Top Bottom