Wachawi wa elimu yetu ni hawa

malackN

Member
Jul 25, 2012
54
14
Naanza kwa kuwapa pole sana wahanga wa matokeo ya kidato cha4.

Kuna sababu kibao zilizo sababisha watoto kufeli ila mimi binafsi ninasababu kuu mbili ambazo naamini zaidi ya 90% zimesababisha matokeo mabovu;

1. Uwajibikaji wa viongozi wa selika na utekelezaji wa sela ya elimu, hili naona ndio tatizo kubwa ambaro linafanywa makusudi kwakua tu watoto wa vigogo wote hawasomi shule za selikali, ili kupunguza upinzani katika ukanda wa ajira na uongozi kwa ujumla, hivyo viongozi kuendelea kufisadi pesa za elimu bila hata shaka kwa kuwa viongozi wote wajuu haiwagusi sana kwa kuwa familia zao husomea inje au st.

2. Maslahi ya walimu hili ni tatizo kubwa mno tunapiga kelele maabala, maktaba, wingi wa wanafunzi darasani, nk lakini hizi zote hazifikii maslahi ya walimu mfano tunapiga kelele maabala mbona watoto wamefeli hadi kiswahili au nacho kinahitaji maabara, Inasikitisha sana kusikia kiongozi wa selikali kusema haiwezekani kuongeza mshahara wa walimu!

Kama enzi za mwalimu walimu walilipwa pesa za kukidhi mahitaji yao vizuri kwa pesa za pamba, korosho na katani, iweje leo kuna pamba, katani, korosho, utalii unafanya vizuri, uvuvi, madini kibao yanachibwa, bandari iko vizuri, na kodi za bidhaa ambazo ziko juu sana kuliko wakati wowote wa miaka 50 ya uhuru, eti inashindikana kuongeza mshahala, kipato cha mwalimu sasa hivi hakina utofauti na muuza mchicha pale kariako, kweli inawezekana kufundisha vizuri mwalimu huku akiwa yeye ndie muuza karanga na mandazi shuleni, leo hii tunapiga kelele hakuna ukaguzi mashule je?

Kwa hiki kipato unaweza kumlimiti mwalimu ahudhurie shule kila siku badala ya kutafuta ridhiki sehemu nyingine sanasana atakwambia potelea mbali wakinifukuza nitafungua genge na hayo ndiyo yanayo wakuta walimu wakiomba ruhusa ya kwenda kusoma wakikataliwa tu wanatoroka kwa mantiki ya rorote liwe kwanza maslahi yenyewe madogo.

Suruhisho inabidi kwenye katiba tuweke kipengele kinacho piga marufuku mtoto wa kiongozi yeyote wa selikali lazima asome shule za selikali, hii itaongeza uwajibikaji kwani hawa ndio wachawi wa elimu yetu.

Ninaamini mtoto wa raisi akipata zero viongozi kibao watajiuzuri kwa hofu lakini leo hii matokeo ambayo yawezekana yamevunja record ya dunia hata kiongozi mmoja hajajiudhuru, hii ni kwa kuwa familia za watu wanao ogopwa zote ziko salama kwa hili tatizo.

Asanteni Mungu ibariki elimu yetu, Mungu ibaliki Tanzania
 
Tangu nizaliwe sijashudia Tanzania ikiwa na njaa ya kiongozi kama ilivyo leo hii. Hadi inatia aibu. Raisi ameshindwa katika secta zote. Sheria hakuna, elimu sifuri, matibabu yai, miundombinu usiseme. Tunaenda wapi watanzania? Yaani hadi inatia huruma nchi haina waziri hata mmoja vilaza kibao utendaji sifuri kabisa. Yaani jamani tunapitwa na Waganda ambao walikuwa na vita za wenyewe kwa wenyewe miaka yote. Wameamka wanasomesha watoto wao sisi tunachekeana na vilaza wa kutupwa. Ni lini tutawawajibisha hawa wezi wasiojali taifa hata chembe kazi kukwapua tu raslimali zetu huku wakituacha tunaangamia?
 
mbona unawasahua walimu... siku hizi wanaitwa shemeji madarasani!

kama umesoma vizuri niasema kuna sababu nyingi ila hizo ndio kuu, kinacho sababisha hayoyote nikwasababu hawana cha kupoteza ndio maana hawaheshimu kazi yao sasa hivi maslahi madogo
 
Tangu nizaliwe sijashudia Tanzania ikiwa na njaa ya kiongozi kama ilivyo leo hii. Hadi inatia aibu. Raisi ameshindwa katika secta zote. Sheria hakuna, elimu sifuri, matibabu yai, miundombinu usiseme. Tunaenda wapi watanzania? Yaani hadi inatia huruma nchi haina waziri hata mmoja vilaza kibao utendaji sifuri kabisa. Yaani jamani tunapitwa na Waganda ambao walikuwa na vita za wenyewe kwa wenyewe miaka yote. Wameamka wanasomesha watoto wao sisi tunachekeana na vilaza wa kutupwa. Ni lini tutawawajibisha hawa wezi wasiojali taifa hata chembe kazi kukwapua tu raslimali zetu huku wakituacha tunaangamia?

kweli kabisa
 
Kuna hili la ualimu kuwa kazi ya watu waliopata alama za chini kwenye matokeo yao nadhan nalo kuna haja ya kuliangalia upya, suala hili ni ukweli mchungu ila hatuna budi kulisemea. Mwalimu wa leo hii ni yule aliyepata DIV 4 na points zake, haiwezekani utegemee mwalimu wa Hisabati afaurishe watoto wapate A kwenye Hisabati wakati yeye mwenyewe enzi zake alipata Hisabati D au alifail kabisa.

Mfumo wetu huu unafanya elimu ni sehemu ambayo waajiriwa wake ni wale waliopata alama za chini wakiwa wanafunzi. Hivi hapo unategemea nini hasa????Mbona vyuo vikuu wameweka GPA za juu kama kigezo?? Kwann wasiweke GPA za chini pia kama kigezo cha kuajiri wahadhiri??? Au elimu ya chuo kikuu haina uhusiano na hii elimu ya huku chini????Au tunategemea miujiza ipi mwalimu wa sekondari aifanye katika kufundisha kitu asichokiweza?????

Serikali inadhan nini kinazuia mtu aliyefauru vizuri kukimbilia ajira za ualimu???Mtu aliyefauru anaona kuwa mwalimu wa sekondari sio option ya ajira maana anaona kwenda huko ni kujitaftia umaskini. Kama mishahara ya walimu wetu ingekuwa minono kama at least ile ya karani wa TRA au wa Bunge au kama ule wa Livingstone Lusinde kibajaji hiv unadhan wale wenye Div I point 7 msingewaona huko?????

Mishahara ya walimu ingekuwa kama ya Politicians unadhan wakina Mwakyembe, Maghembe, Kawambwa, Msolla name them wangekuwa na haja ya kukimbia kazi ya Uhadhiri/ualimu???? Nani anapenda umaskini???Kumbukeni kuwa mwalimu hana kikao cha kulipwa posho na wala hatoki kwenda safari nje ya nchi za kujifunza wenzao huko wanafanyaje kama wanavyopishana airport wanasiasa wetu. Sasa unapompa mshahara kiduchu kimsingi unamtaka ajiongeze kujazia kinachopungua. Anaweza kujiongeza kwa kumega muda wa muajiri au kwa kutowajibika kabisa na kuwazuga wanafunzi kwa vile anajua akigoma kabisa majiwasha yatamhusu.

Hatuhitaji microspic eyes au rocket scientists wala tume kama Pinda anavyotaka kutuaminisha katika kubaini matatizo ya walimu nchini. Vilio vya kuporomoka kwa elimu havijaanza leo, mengi yalishasema serikali ikaweka pamba maskioni. Waziri mkuu ajiulize huko huko nyumbani kwake, maslahi anayoyapata je yanalingana na ya mwalimu???? Au anataka kusema yeye analipwa hivyo kwa vila amesoma sana?? Kwa vile anaitumikia sana Serikali yetu au kwa vile mzalendo sana???? Inahitajika Political will tu kuiinua sekta ya elimu.

Kwa nini serikali inahisi walimu hawapaswi kupata maslahi bora??? kama nyumba nzuri, afya bora, allowances nzuri na mishahara minono??? Kazi ya ualimu ni ngumu sana kuliko hata kukusanya kodi au kuratibu michango ya NSSF, PPF,PSPF, ni ngumu kuliko jeshi maana ina implication kubwa sana kwenye mustakabali wa taifa husika. Ni kazi inayohitaji moyo wa kizalendo kuifanya na upendo wa dhati wa kiuzazi kwa mwanafunzi unayemfundisha.

Itoshe kusema, kimsingi anguko la elimu hapa nchini limechangiwa kwa kiasi kikubwa na serikali yetu. Sasa nini kifanyike nadhani wadau humu mtaweza kuweka mitazamo vizuri! Mana kulaumu tu bila kutoa suluhu pia si busara. Ni mtazamo wangu tu...
 
Kuna hili la ualimu kuwa kazi ya watu waliopata alama za chini nadhan nalo kuna haja ya kuliangalia upya ingawa ni gumu sana wengi wetu kulizungumzia. Haiwezekani utegemee mwalimu wa Hisabati afaurishe watoto wapate A wakati yeye mwenyewe mwalimu enzi zake alipata Hisabati D au alifail kabisa.

Mfumo wetu unafanya elimu ni sehemu ambayo waajiriwa wake ni wale waliopata alama za chini wakiwa wanafunzi. Hivi hapo unategemea nini hasa????Mbona vyuo vikuu wameweka GPA za juu kama kigezo?? Kwann wasiweke GPA za chini pia kama kigezo cha kuajiri wahadhiri??? Au elimu ya chuo kikuu haina uhusiano na hii elimu ya huku chini????Au tunategemea miujiza ipi mwalimu wa sekondari aifanye katika kufundisha kitu asichokiweza?????

Serikali inadhan nini kinazuia mtu aliyefauru vizuri kukimbilia ajira za ualimu???Mtu aliyefauru anaona kuwa mwalimu wa sekondari sio option ya ajira maana anaona kwenda huko ni kujitaftia umaskini. Kama mishahara ya walimu wetu ingekuwa minono kama ile ya TRA au kama wa Livingstone Lusinde kibajaji hiv unadhan wale wenye Div I point 7 msingewaona huko?????Au kama mishahara ya walimu ingekuwa kama ya Politicians unadhan wakina Mwakyembe wangekuwa na haja ya kukimbia chaki???? Nani anapenda umaskini???

Hatuhitaji microspic eyes au rocket scientists wala tume kama Pinda anavyotaka kutuaminisha katika kubaini matatizo ya walimu nchini. Vilio vya kuporomoka kwa elimu havijaanza leo, mengi yalishasema serikali ikaweka pamba maskioni. Waziri mkuu ajiulize huko huko nyumbani kwake, maslahi anayoyapata je yanalingana na ya mwalimu???? Au anataka kusema yeye analipwa hivyo kwa vila amesoma sana?? Kwa vile anaitumikia sana Serikali yetu au kwa vile mzalendo sana???? Inahitajika Political will tu kuiinua sekta ya elimu.

Kwa nini serikali inahisi walimu hawapaswi kupata maslahi bora??? kama nyumba nzuri, afya bora, allowances nzuri na mishahara minono??? Kazi ya ualimu ni ngumu sana kuliko hata kukusanya kodi au kuratibu michango ya NSSF, PPF,PSPF, ni ngumu kuliko jeshi maana ina implication kubwa sana kwenye mustakabali wa taifa husika. Ni kazi inayohitaji moyo wa kizalendo kuifanya na upendo wa dhati wa kiuzazi kwa mwanafunzi unayemfundisha.

Itoshe kusema, kimsingi anguko la elimu hapa nchini limechangiwa kwa kiasi kikubwa na serikali yetu. Sasa nini kifanyike nadhani wadau humu mtaweza kuweka mitazamo vizuri! Mana kulaumu tu bila kutoa suluhu pia si busara.

Mkuu umemaliza, kama inawezekana hiyo tume ya Pinda ipitie hiki kipande.
 
Pamoja na walimu kutopata haki zao lakini tatizo lililopo ni kutokana mfumo wa elimu ulivyo tangu chekechea hadi Chuo Kikuu.Moja chekechea lazima wawe na muundo wao wa kuanza kujifunza.Zamani elimu ya awali ilikuwa katika mfumo wa 3Ks maana yakeKUHESABU,KUSOMA na KUANDIKA ndio sababu huko kwetu shamba tulianzia kuandika kwenye udongo-kibao na baadae daftari.:yo:Tulianzia kuhesabu vidole-kuhesabiana mstarini vijiti na baadae tebo ambayo kila daftari ilikuwa nayo.Kinyume na sasa mtoto wa elimu ya awali anabeba vitabu zaidi ya kilo tatu,anajifunza nini?Kwaa mtindo huu mtoto anakariri tu bila kujua anachokalili kilipatikanaje kwa elimu yake aliyonayo.Kwa kutofuata mbinu za ufundishaji ndo maana watoto wengi wanadumaa kiakili hadi elimu ya juu.Kama janga lilotupata 2012 haiwezekani mwanafunzi akashindwa kujibu hata swali moja .Mitaala mibovu ndo maana hata shule za binafsi na zenye vipaji wote kushnee.Wananchi tunamlaumu Ms Ndalichako kwa watoto kufeli mlitaka afanye standardization ili washinde bila kufaulu .Tumshukuru huyo mama kwa sababu ameonyesha zaili jinsi gani elimu yetu iko duni inatakiwa ifanyiwe ukarabati mnono.mazara ya kuiba mitihani na kununua ufaulu unajionesha kwa sasa ni jinsi gani tunavyokosa ajira kwa visingizio kibao.Hata tukiodoa Kawambwa hakuna jipya kwa sababu mitaala yote kaikuta.Wakati umefika tusiwe na akili mgando tuwe na mageuzi kwenye sekta ya elimu na matunda tutayaona.Watanzania tunao wataalamu kibao mpaka wengine wanapew uraia ,uwaziri nk jaribuni kuwarudisha ili wakarabati nchi yao kwa sababu msingi wa elimu zao ni tanzania.Hapo awali enzi za Nyerere Tz ilikuwa inaongoza kwa elimu Africa ,jaribu kuperuzi nyaraka zinazo husu Chuo kikuu cha dsm ,Ihungo,Nganza,Tanga School,mzumbe,Kahororo,Nyakato,Nsumba,Galanos,Bwiru,Kib :wink:
 
Big up bro
 
Mkuu umemaliza, kama inawezekana hiyo tume ya Pinda ipitie hiki kipande.

inamaana na hao walimu wa sekondari waliotoka vyuo vikuu ni failure au walipata division 4? au hawa wa division 4 mnaowaita failure ndo wameanza kufundisha kuanzia matokeo yalipoanza kushuka 2010? na hapo nyuma waliokuwa wanafundisha primary walikuwa na division ngapi? na kwani hawapo mpaka sasa?nadhani mkijibu haya maswali mtapata mchanganuo mzuri.
 
Nina uhakika unaelewa vizuri utaratibu wa elimu ya Tz, mwalimu yeyote awe wa Certificate, Diploma au Degree, ni chaguo la Division za chini. Hii ina maana mwanafunzi ambaye hakua mzuri darasani ambaye sasa ni mwalimu anafundisha wanafunzi kwa kiwango hicho cha uelewa mdogo. Sasa basi, angalia hiyo hali ikijikusanya kwa miaka tuseme 10, kiwango cha uelewa kitazidi kushuka sana.

Ni jambo linaloeleweka kwamba katika darasa, wanafunzi wanaopata Div 1 na Div 2 ni nadra sana kusoma ualimu (sidhani kama wapo wanaosoma ualimu). Sasa hawa ndo tunaofahamu kwamba uelewa wao uko juu zaidi na hata ktk discussions za mashuleni unakuta hawa ndo wanawaelekeza hao wanaopata Div 3 na Div 4 (hao wa Div 0 tusiwaongelee kabisa) na wakitoka hapo wanakwenda kusoma ualimu waje wafundishe unategemea nini???.

Kwa wale wa Degree hata kama hawakupata Div 4, lakini bado ufaulu wao si mzuri kama wale wanaochukua fani zingine kama Wahandisi, Madaktari, Wahasibu, Wanasheria nk. Hatutegemei mtu amepata Div 1 point 3 hadi 9 Form Six aende University akasome Education (kama amewahi kutokea naomba unifahamishe).

Sasa basi ukilimbikiza kwa muda mrefu kama nilivyosema hapo juu au hata miaka 20, kwa wale wanaoelewa kidogo kufundisha, unakuta idadi ya wanaoelewa kidogo inazidi kuongezeka. Kwa nini Lecturers wanabakizwa wale waliofanya vizuri??? kwa sababu wanafunzi wanaokwenda Universities ni wale wenye uelewa wa juu hivyo ukimbakiza mtu aliyepata PASS sidhani kama atawezana na mwanafunzi aliyepata Point 3.

Ninaamini nimeweza kukupa majibu ya maswali yako, ingawa haikua nia yangu kuzungumzia ufaulu wa walimu katika ngazi tofauti (kwenda kusoma Certificate, Diploma na Degree) lakini imenibidi kufanya hivyo ili kukidhi haja ya maswali yako. Hata kama nawe unasoma ualimu au ni mwalimu tayari, nia yangu ilikua ni kueleza hali ya elimu ya Tanzania, hivyo nitaomba nisieleweke vibaya japo naamini hata wewe unafahamu hayo niliyoyaeleza.
 
Ng'wale mi nimesoma na watu wengi tu walipata 1 ya 6 na nane walienda ualimu kukariri kubaya hiyo kasumba ya kuwa walimu ni wale waliofeli au wenye uelewa mdogo inawaangamiza watanzania kwa kutotambua adui wao ni nani na wale wanaofundisha private na hao hao pia wapo serikalini wao wametoka wapi hadi wafaulishe? sio kila ambaye hakupata one ni kilaza au ana uelewa mdogo wangapi wamefoji vyeti au waliiba mitihani na wengine wanakipaji cha kukariri?ungekuwa umesoma kuhusu intelligence ungeona kila mtu anavyokuwa shupavu katika nyanja zao.Wangapi waliosomea ualimu na wapo vyuoni na wanafundisha ina maana wangekuwa vilaza hata hizo sifa za kufundisha wamezipataje?
 
Last edited by a moderator:
Nina uhakika unaelewa vizuri utaratibu wa elimu ya Tz, mwalimu yeyote awe wa Certificate, Diploma au Degree, ni chaguo la Division za chini. Hii ina maana mwanafunzi ambaye hakua mzuri darasani ambaye sasa ni mwalimu anafundisha wanafunzi kwa kiwango hicho cha uelewa mdogo. Sasa basi, angalia hiyo hali ikijikusanya kwa miaka tuseme 10, kiwango cha uelewa kitazidi kushuka sana.

Ni jambo linaloeleweka kwamba katika darasa, wanafunzi wanaopata Div 1 na Div 2 ni nadra sana kusoma ualimu (sidhani kama wapo wanaosoma ualimu). Sasa hawa ndo tunaofahamu kwamba uelewa wao uko juu zaidi na hata ktk discussions za mashuleni unakuta hawa ndo wanawaelekeza hao wanaopata Div 3 na Div 4 (hao wa Div 0 tusiwaongelee kabisa) na wakitoka hapo wanakwenda kusoma ualimu waje wafundishe unategemea nini???.

Kwa wale wa Degree hata kama hawakupata Div 4, lakini bado ufaulu wao si mzuri kama wale wanaochukua fani zingine kama Wahandisi, Madaktari, Wahasibu, Wanasheria nk. Hatutegemei mtu amepata Div 1 point 3 hadi 9 Form Six aende University akasome Education (kama amewahi kutokea naomba unifahamishe).

Sasa basi ukilimbikiza kwa muda mrefu kama nilivyosema hapo juu au hata miaka 20, kwa wale wanaoelewa kidogo kufundisha, unakuta idadi ya wanaoelewa kidogo inazidi kuongezeka. Kwa nini Lecturers wanabakizwa wale waliofanya vizuri??? kwa sababu wanafunzi wanaokwenda Universities ni wale wenye uelewa wa juu hivyo ukimbakiza mtu aliyepata PASS sidhani kama atawezana na mwanafunzi aliyepata Point 3.

Ninaamini nimeweza kukupa majibu ya maswali yako, ingawa haikua nia yangu kuzungumzia ufaulu wa walimu katika ngazi tofauti (kwenda kusoma Certificate, Diploma na Degree) lakini imenibidi kufanya hivyo ili kukidhi haja ya maswali yako. Hata kama nawe unasoma ualimu au ni mwalimu tayari, nia yangu ilikua ni kueleza hali ya elimu ya Tanzania, hivyo nitaomba nisieleweke vibaya japo naamini hata wewe unafahamu hayo niliyoyaeleza.

hebu acha upotoshaji wa wazi kabisa tena acha dharau kwenye fani za wenzio.
labda nikuulize nini qualification za mtu kujiunga chuo?? na je wataka kuniambia hakuna wanafunzi waliopata div 1 wakasomea ualimu?? na je mwanafunzi anayesoma ftc cheti huyu ana division gani??

kimsingi elimu kama ilivyo fani nyingine imegawanyika katika makund ya cheti, dip na shahada. katika ngaziz zote hizo huwa kuna qualification tofauti mathalan anayesomea cheti elimu yake inatakiwa iwe ni form 4 ila anayesomea shahada awe ana elimu ya form six na ufaulu kulingana na viwango ambavyo vhuo na TCU imekubaliana.

kuwepo kwa waalimu mathalan wanao kuwa na alama za chini na mfano point 5 akakubaliwa kusomea ualimu hii ni kutokana na kutaka kuoneza idadi ya watumish waalimu na si kwasababu eti wamefeli.

mwaka huu wa masomo wanafunzi waliojiunga kusoma uhandisi hapa mlimani ukiuliza ama kutafuta wenye div 1 za form six ni wachache sana na wengi wana div 3. wengi wa waliopata div 1 wamekimbilia kusomea bcom kwa kipengele kwamba ni fani inayolipa mapema zaid na unasoma ukila bata. kutokana na hili baraza la senete la chuo walidiriki hata kushusha point alimradi wapatikane wanafunzi watakao somea uhandisi. kwangu mimi hii haina tofauti na ilivyofanyika kwenye elimu.

sio kweli kwamba mwl mwenye degree ana div 4, na hata mwenye diploma sio kwamba anaufaulu mdogo zaidi kuliko daktari ama mwanafunzi wa fani nyingine.
 
Nina uhakika unaelewa vizuri utaratibu wa elimu ya Tz, mwalimu yeyote awe wa Certificate, Diploma au Degree, ni chaguo la Division za chini. Hii ina maana mwanafunzi ambaye hakua mzuri darasani ambaye sasa ni mwalimu anafundisha wanafunzi kwa kiwango hicho cha uelewa mdogo. Sasa basi, angalia hiyo hali ikijikusanya kwa miaka tuseme 10, kiwango cha uelewa kitazidi kushuka sana.

Ni jambo linaloeleweka kwamba katika darasa, wanafunzi wanaopata Div 1 na Div 2 ni nadra sana kusoma ualimu (sidhani kama wapo wanaosoma ualimu). Sasa hawa ndo tunaofahamu kwamba uelewa wao uko juu zaidi na hata ktk discussions za mashuleni unakuta hawa ndo wanawaelekeza hao wanaopata Div 3 na Div 4 (hao wa Div 0 tusiwaongelee kabisa) na wakitoka hapo wanakwenda kusoma ualimu waje wafundishe unategemea nini???.

Kwa wale wa Degree hata kama hawakupata Div 4, lakini bado ufaulu wao si mzuri kama wale wanaochukua fani zingine kama Wahandisi, Madaktari, Wahasibu, Wanasheria nk. Hatutegemei mtu amepata Div 1 point 3 hadi 9 Form Six aende University akasome Education (kama amewahi kutokea naomba unifahamishe).

Sasa basi ukilimbikiza kwa muda mrefu kama nilivyosema hapo juu au hata miaka 20, kwa wale wanaoelewa kidogo kufundisha, unakuta idadi ya wanaoelewa kidogo inazidi kuongezeka. Kwa nini Lecturers wanabakizwa wale waliofanya vizuri??? kwa sababu wanafunzi wanaokwenda Universities ni wale wenye uelewa wa juu hivyo ukimbakiza mtu aliyepata PASS sidhani kama atawezana na mwanafunzi aliyepata Point 3.

Ninaamini nimeweza kukupa majibu ya maswali yako, ingawa haikua nia yangu kuzungumzia ufaulu wa walimu katika ngazi tofauti (kwenda kusoma Certificate, Diploma na Degree) lakini imenibidi kufanya hivyo ili kukidhi haja ya maswali yako. Hata kama nawe unasoma ualimu au ni mwalimu tayari, nia yangu ilikua ni kueleza hali ya elimu ya Tanzania, hivyo nitaomba nisieleweke vibaya japo naamini hata wewe unafahamu hayo niliyoyaeleza.

mtaweweseka sana na matokeo ya kitihani ya taifa!nyie paruaaneni weeeeee lakini msidharau kazi za wenzenu!
mimi ni mwalimu
KIDATO CHA NNE NINA DIVISION 2
KIDATO CHA SITA NINA DIVISION 1.9
DEGREE NINA G.P.A YA 3.7
kwa taarifa yako yapo mengi sana yanapaswa kubadilishwa lakini mkibaki na imani kuwa walimu ndio chanzo tutazidi kuumia sana kama taifa! na serikali yenu ndo upopo inaowajaza huo kichwani!
nyie endeleeeni tu!
 
Kwa wale wa Degree hata kama hawakupata Div 4, lakini bado ufaulu wao si mzuri kama wale wanaochukua fani zingine kama Wahandisi, Madaktari, Wahasibu, Wanasheria nk. Hatutegemei mtu amepata Div 1 point 3 hadi 9 Form Six aende University akasome Education (kama amewahi kutokea naomba unifahamishe).

acha dharau nenda Faculty of education siku hizi inaitwa college of education kaangalie wanafunzi walioanza 2000 walikwenda kusoma ualimu wakiwa na point ngapi??

halafu usiwe na akili fupi eti kama kuna mwenye point 9 sasa naomba Invisible aniruhusu nikuwekee vyeti vyangu vyote hapa.

kisha nakuomba kesho asbh nenda pale COET ulizA mwaka juzi na mwaka jana wanafunzi waliosoma uhandisi wanakwenda na minimum point ngapi ndipo uje ujambe upuuzii wako hapa.

halafu nenda College of business school kaangalie wanafunzi wanaosoma kule shahada wengi waliosoma ECA, na HGE wameingia na qualification gani kama utakuta div 1 zikiwa nyingi kama za wanafunzi waliosoma PCB na PCM. hivi umewah kumkuta lini mwanafunzi amesoma ECA akawa na div 1 ya point 3?? sasa kuliko kubwabwaja ujinga wako kaa chini ufikiri kwa makini.

kumbuka kwamba maslah madogo ya kazi yenyewe yamewafanya watu wasomee ualimu kisha wakimaliza waukimbie kama huamini chunguza graduates wa 2000-2006 nenda mashulen uwafanyie hesabu utawakuta ni 1/4 tu ndio wamebaki wengine wote wapo kwenye kazi tofauti na wamejiendeleza kwa maslah yao.

idadi ya graduates wa ualimu ni kubwa kuliko fani yyte ile ila kazini wapo wachache kuliko fani nyingine yyte umewah kujiuliza sababu?? na wamekwenda wapi??

Yaani ulivyonikera natamania kesho nikwambie uje ofcn kwangu nikuonyeshe kinachoua elimu ya taifa hili ili ubongo wako uwe na akili. nyambaffffffffffff
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom