Wabunge wote wa CCM wameitwa dharura kikao cha DOWANS kesho

habari za kuaminika sasa hivi wabunge wote wa ccm wameitwa dodoma kuandaa na kuweka mkakati wa pamoja juu ya dowans. Nia ni kuzibwa midomo na imetamkwa kwamba dowans ina masilahi gani na kila jimbo la mbunge.

Baraza la mawaziri limeazimia hakuna kujadili suala hilo.

Taarifa hizi nimepata toka kwa mmoja wa wabunge akiwa anajiandaa kuelekea dodoma.

nashauri wasomaji wetu kabla ya kuingia kwenye article kama hizi kuwa karibu na kikombe ya maziwa kwani habari zingine hazina tofauti na sumu hivyo ukiona yanakuzidi dilute na maziwa
 
Suala hili la Dowans linaweza kutatuliwa kwa kutaifisha hii kampuni bila malipo ya fidia yoyote, (yaani "confiscate Dowans with all its assets on which the Government of Tanzania can place its hands") including any bank accounts with credits Dowans may have.

Richmond ilikuwa kampuni feki, na ile Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mhe. Harrison Mwakyembe ilithibitishiwa hivyo wakati ujumbe wake ulipotembelea Houston Texas. Kampuni iliingiza mitambo ambayo TANESCO walikuwa wanalipia "capacity charges" hata wakati haizalishi umeme.

Kampuni hii ikarithiwa na DOWANS. Yaani mitambo hiyo ambayo haizalishi umeme iliendelea kulipiwa na TANESCO kwa "capacity charges". TANESCO wanatulipisha sisi wananchi gharama za juu za umeme ili waweze kuwalipa Dowans.

Dowans ni feki pia. Mwana-Mfalme Mwarabu aliyesemekana ana hisa ktk Dowans, amekana na kusema huo ni uongo mtupu. Huko Costa Rica ambako inasemekana mwanahisa mwingine wa Dowans (Tanzania) anakaa, Serikali ya nchi hiyo imetamka kwamba hakuna kampuni ya jina hilo.

Nahisi ni hawa matapeli wa hapa hapa Tanzania, wanaomiliki Dowans (Tanzania), wakiongozwa na R.A. ambao wanalipwa hiyo compensation iliyoamriwa na ICC ya huko Paris. Kwa hiyo hao ndiyo wana-pressurize Serikali ilazimishe TANESCO walipe.

Nahisi pia ni hawa hawa matapeli mafisadi waliokwapua fedha za EPA toka BoT, wakaendeshea Uchaguzi Mkuu wa 2005, na kutumia nyingine kununulia mitambo ya Richmond.

Kama ni feki kweli, na TANESCO wamekwisha kutukamua vilivyo kwa miaka hii tangu wakati wa Richmond, basi hata hiyo mitambo ikiwa confiscated, kama ninavyopendekeza, watakuwa wamelipwa vya kutosha.
 
Maaskofu wenyewe wanashiriki UUaji wizi na uzinzi sembuse wabunge??
Tunamtaja Mungu tunasahau jambo moja kwamba Mimi na wewe ni Miungu vile vile tunalitaka hapa Duniani ndilo linalotendeka.
Tatuzo kubwa tulilolivaa kama joho ni kuwaacha Wendawazimu na washenzi kutoa maamuzi kwa niaba yetu na kuyatekeleza kwa niaba yetu.
Huu ndiyo wakati sahihi wa kusema basi, kila siku tunajidanganya kwa kusema wakati sahihi ni ule karibu ya uchaguzi.
Huu ni wakati sahihi Mwizi ni lazima aitwe mwizi na ikibidi sheria ichukuliwe mikononi mwetu.

Hata kama wewe mpagani ujue yupo Mungu aliyesababisha wewe kuwepo na unaowashutumu ni watumishi wake acha kujitafutia laana zisizo za lazima mkuu.
 
Wameitwa na nani? i think bunge linakaribia kuanza sidhani ni issue ya Dowans, maana
it is impossible to pay this lump sum of money, its repercussions will possibly lead to
impeachment of JK, hii ni hatari mno, kila mtu anajua, na ujue wabunge hata wa
CCM hawakubali kulipa, mmmhh hivi walikuwa wanatumia Chopa 3 eehh, like millitary
air show

Silioni Bunge la kum-impeach JK. Kama sakata la EPA lilipita salama na Richmond nayo ikapita salama. Hata Dowans nayo itapita salama tu. Hao akina Lembeli unaowasema, wakishashikishwa adabu kwenye vikao vya Wabunge wa CCM hakuna atakayekwenda kinyume na msimamo/maagizo/maelekezo ya chama. Wabunge wa CCM hawako independent kimawazo, kuna mambo mengi sana wanaunga mkono kwa kuwa ni msimamo wa chama. Lakini joto la 2010 halijasahaulika, wananchi tunawaangalia tu, wakae wakijua kwamba ufisadi ndio uliowatesa kwenye uchaguzi uliopita, na wakiendelea kucheza, 2015 tutaungana nao mtaani.
 
Habari za kuaminika sasa hivi wabunge wote wa CCM wameitwa Dodoma kuandaa na kuweka mkakati wa pamoja juu ya Dowans. Nia ni kuzibwa midomo na imetamkwa kwamba DOWANS ina masilahi gani na kila jimbo la mbunge.

BARAZA la mawaziri limeazimia hakuna kujadili suala hilo.

Taarifa hizi nimepata toka kwa mmoja wa wabunge akiwa anajiandaa kuelekea DODOMA.

Duh hii inaweza kuwa kali ya mwaka au uzushi mtakatifu, inaweza ikawa kweli wameitwa lakini kujua ajenda wakati mnoko aliekupa ukuda anajitayarisha inanifanya nisiamini habari yako na kuiona ya kutungatunga. Huo ni upeo wangu na mawazo yangu tu usipaniki mkuu wengine wameamini mia kwa mia mimi NO!
 
Hukiona hivyo mambo ni magumu, matumbo joto na wakileta ujinga watapita mawe na wananchi majimboni akianza kutetea matumbo yao.
 
Kuna ajabu gani manyang'au kukutana kwenye mzoga. Tatizo moja tu naloliona ni kuwa kuna hatari ya wale fisi wanyonge kutafunwa, si ndio tabia za kifisi ?
 
Habari za kuaminika sasa hivi wabunge wote wa CCM wameitwa Dodoma kuandaa na kuweka mkakati wa pamoja juu ya Dowans. Nia ni kuzibwa midomo na imetamkwa kwamba DOWANS ina masilahi gani na kila jimbo la mbunge.

BARAZA la mawaziri limeazimia hakuna kujadili suala hilo.

Taarifa hizi nimepata toka kwa mmoja wa wabunge akiwa anajiandaa kuelekea DODOMA.

Wanaenda kufunika moto wa majani makavu kwa blanket lazima waumbuke
 
waende wakajadili then waweke kando maslahi ya taifa..........sisi tupo na wala wasidhani hatuoni ......nani alijuia tunisia yatatokea !!!

na huyu wa kwetu hapa jamani lazima tufanye namna[/B] hadi 2015 ni parefu mno.....atatuua huyu


Hebu fanya faster kama mambo hayajaharibika.
 
TAARIFA KWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Ofisi ya Bunge inapenda kuwatangazia Waheshimiwa Wabunge wote kuwa kutakuwa na mafunzo ya awali (Orientation Course) yatakayotolewa kwao kuanzia tarehe 25 Januari, 2011 mpaka tarehe 3 Februari, 2011.
Mafunzo hayo yatatanguliwa na vikao rasmi vya Vyama vya Siasa kikiwemo CCM ambacho kitakuwa na semina kuanzia tarehe 22 – 24 Januari, 2011. Kikao cha Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitafanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Kwa taarifa hii, Waheshimiwa Wabunge wanaombwa kuwasili Dar es Salaam kwa kuzingatia tarehe ya vikao hivyo vya mafunzo.
Eliakim P. M. Mrema
KAIMU KATIBU WA BUNGE


Asante ndugu.

Siku hizi inabidi kuwa makini sana na baadhi ya post na thread ambazo nyingi ni uzushi na udaku. Watu mnaweza kujikuta mnaandamana na kuuawa halafu baadaye ndio mnajua mlichokuwa mnaandamana kwacho si sahaihi.

Punguzeni kukurupuka wanaJF mnaokurupuka.
 
Hivi hakuna njia ya kumfukuza mbunge baada ya kumchagua?? Wajuzi wa katiba tusaidieni.................... Nafikiri some of these MPs have to be recalled.

ndiyo maana tunaambiwa kabla ya kutenda tufikirie kwanza.Ukishamchagua mbunge habari imeisha hakuna njia ya kumwondoa.tulitakiwa kuwa makini wakati wa uchaguzi.kama ulifikiri uchaguzi ni kuchagua tu kwa ushabiki ndo matokeo yake ni hayo.
 
Wabunge tumewaamini tukawachagua kutetea maslahi ya majimbo yenu na watanzania kwa ujumla ikiwemo kutolea ufafanuzi suala la DOWANs. Ninawaomba MSITUSALITI JAMANI....

Tatizo la wabunge wengi wa CCM ni kwamba hawakuchaguliwa na wananchi lakini wakashinda.
Hii habari ya kusema wakiboronga tutawasubiri 2015 wao haiwatishi kwa sababu mfumo wao wa ushindi sio ule wa kwenye sanduku la kura.

Hivi tunadhani wananchi wa Igunga wanapenda kuwa na mbunge ambaye hajui matatizo yao, bubu akiwa bungeni, mwenye sifa mbaya machoni pa watanzania, mwenye uraia tata n.k?? Ungekuwa wewe ndio mkurungenzi wa uchaguzi igunga na RA akakukatia billioni moja ungefanyaje??
Kwa mfumo wa sasa (NEC-ccm), ukimtishia mbunge kama huyu kwamba tutaonana 2015 atakucheka.

Ushauri wangu kwenu: Hakikisha unatembea na dawa za kutuliza maumivu kila siku maana taarifa mbaya zitaendelea for the next 5 years.

Mechi ya Dowans Vs Watanzania mpaka sasa Dowans wanaongoza 5 - 0.
Ni vizuri watanzania wakakubali kuwa wamepoteza mechi hii ili wajipange kwa mechi ya kugombea kombe la KATIBA MPYA ambapo wanapambana na timu kali ya Watawala yenye uzoefu na michuano hii toka 1961.
 
‘Waliohusika sakata la Dowans wachukuliwe hatua za kisheria'

Wednesday, 19 January 2011 21:39

Sadick Mtulya

SUALA la malipo ya fidia kwa Kampuni ya Dowans, limeingia sura mpya baada ya wasomi kutaka Watanzania walioingia mkataba na kampuni hiyo wachukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kushtakiwa.

Wadau hao walitoa wito huo juzi jijini Dar es Salaam wakati wakichangia mjadala jinsi Tanzania itakavyoweza kunuifaka, ikiwamo kukuza uchumi kwa kutumia mbinu na ujuzi kutoka China.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Jamii (ESRF), Dk Bohela Lunogelo, alisema kitendo cha viongozi walioingiza nchi kwenye mikataba mibovu kutowajibishwa, kinaathiri mfumo mzima wa utendaji na akasisitiza wote walihusika na Dowans kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Tatizo kubwa tulilonalo ni viongozi kulindana, kitu ambacho ni tofauti na viongozi wa China. Kama kiongozi akifuja mali za umma, akihusika na ufisadi, achukuliwe hatua za sheria ikiwamo kushtakiwa,'' alisema Dk Lunogela
Dk Lunogela alisema kama viongozi katika ngazi zote wataendelea kulindana, itakuwa vigumu kwa nchi kupata maendeleo.

Akichangia mada, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Umaskini (Repoa), Profesa Samuel Wangwe, alitaka wote waliohusika kuingia mkataba wa Dowans wasiachiwe huru.

"Wote walioingiza nchi katika mkataba na Kampuni ya Dowans wachukuliwe hatua sio kuachiwa kama vile hawakufanya jambo baya,'' alisema Profesa Wangwe.

Hata hivyo, Profesa Wangwe alisema tatizo la kufa kwa miradi mingi nchini hasa ile inayochukua muda mrefu, ni kukosekana kwa ufuatiliaji na viongozi wengi hufurahia kuizindua sio kuifuatilia.

Hoja za wasomi hao kuhusu sakata la malipo kwa Kampuni ya Dowans, zimekuja wakati ambao Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wanaharakati wa haki za kijinsia tayari wamewasilisha pingamizi Mahakama Kuu kuzuia malipo hayo.
 
Hoja za wasomi hao kuhusu sakata la malipo kwa Kampuni ya Dowans, zimekuja wakati ambao Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wanaharakati wa haki za kijinsia tayari wamewasilisha pingamizi Mahakama Kuu kuzuia malipo hayo.

utaratibu huu na wala siyo ngebe za mahali popote pale ndizo zitamaliza utata huu wa kifisadi hapa nchini.....mahakamani tu.na wala siyo ndani ya CCM au bungeni.............................hawana mandate ya kurekebisha hii aibu kwa taifa..........................
 
Wanapewa vitisho vya hali ya juu hawa ikiwemo kufukuzwa chamani na hivyo kupoteza ubunge. Msiseme chochote katika kikao kinachokuja cha Bunge kupinga malipo ya $69 million kwa DOWANS au malipo ya $87 million kwa RITES, ole wake atakayejaribu kusema lolote ili kupinga malipo hayo. Ndiyo Tanzania yetu hiyo inavyoliwa na mafisadi.
Kwa maana hiyo kuwa mbunge wa CCM ni kukubali kuwa Zoba. Maana haiingi akilini mtu makini na anayeheshimu waliompa dhamana (wapiga kura) kufanya mambo kama hayo ya kupelekeshwa kama ling'ombe.
 
Back
Top Bottom