Elections 2010 Wabunge Wengi Wakosea Viapo Vyao!

Inabidi warudie kuapa bse huwezi weka sharia mahala pa sheria.
Au unaweza kuta wengine wanapindisha makusudi bse dhamira yake inamsuta as hatenda kwa mujibu wa kiapo.
Such that akiflooku wakati anaapa atajipa moyo kuwa kwanza ata kuapa sikuapa
 
Hivi ni kwa sababu gani hivi viapo vina hii sentesi: "Ewe Mwenyezi Mungu Nisaidie". Hiki kipengele ndio kinasababisha watu kushika vitabu vya dini kama biblia au kurani wakati wa kuapa. Katiba ya nchi imetoa uhuru wa kuabudu au kutoabudu (Uwe muislamu, mkristo, mhindi, myahudi, au mpagani una haki na uhuru wa kuchagua kufuata imani au kutofuata imani yoyote ile). Jaribu kufikiria. Wahindi wanaabudu MIUNGU wengi (Gods and Goddesses). Kiapo kinalazmisha anayefuata dini ya 'Hindu' kuomba msaada kutoka kwa MUNGU mmoja! Hicho kipengele kwenye kiapo kinachomlazimisha anayeapa kuomba (kusali) nadhani ni 'unconstitutional'.
 
Jamani Hivi Wa bunge wengi ni Ngumbalu???

1. Stephen Ngonyani (maji marefu) strd 7
2. Livingstone Lusinde - Strd 7
3. Lameck Airo - strd 7
4. Deo Sanga (jah poeple) - strd 7

Hapa kazi ipo kweli kweli! Hivi kama wabunge wote wangekuwa strd 7 baraza la mawaziri itakuwaje? maana kwa katiba ya sasa mawaziri watatoka ndani ya bunge.
Nani waziri wa elimu?
Nani waziri wa mambo ya nje?
Nani waziri wa sheria na katiba?

Ndiyo maana ndiyo mzee nyingi.

Nilikuwa najibu neno NGUMBARU
 
Nakumbuka Rais Obama aliapishwa mara mbili kwa sababu alikosea kiapo chake kwa sababu ya kuweka neno "faithfully" mahali ambapo si pake! Kiapo chake kilikuwa kama ifuatavyo:
ROBERTS: I, Barack Hussein Obama...
OBAMA: I, Barack...
ROBERTS: ... do solemnly swear...
OBAMA: I, Barack Hussein Obama, do solemnly swear...
ROBERTS: ... that I will execute the office of president to the United States faithfully...
OBAMA: ... that I will execute...
ROBERTS: ... faithfully the office of president of the United States...
OBAMA: ... the office of president of the United States faithfully...

ht_obama-2nd-oath_090121_mn.jpg

Chief Justice administers oath of office again to President Barack Obama at the White House

Kwa upande wa Wabunge wetu walioapa leo, naona wengi wamekosea viapo vyao, aidha kwa kuongeza maneno au kuyaruka au kuyabadilisha, lakini Mheshimiwa Spika, Anne Semamba Makinda amekubali viapo vyao bila matatizo yoyote.

Kiapo chenyewe kina maneno yafuatayo:

"Mimi......................................................, naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba, nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie."

Wafuatao ni Wabunge waliokosea kuapa:

1. Peter Joseph Serukamba: hakutaja neno "wa Tanzania" ie alisema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano (bila kutaja wa Tanzania)...
2. Haroub Mohamed Shamis: alisema Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
3. Said Musa Zuberi: alisema "na nitaitumikia" badala ya "na kuitumikia," pia alisema Ewe Mwenyezi Mungu, "unisaidie" badala ya "nisaidie."
4. Ayoub Jacob Hashim: alianza na maneno "Bismillah Rahman Rahim" ambayo hayapo kwenye kiapo na alimalizia kwa maneno "inshallah" ambayo hayapo pia kwenye viapo.
5. Asa Osman Hamad: alisema kwa mujibu wa Sheria "iliyoweka" badala ya "iliyowekwa."
6. Hamad Zahara Ally: alisema Ewe Mwenyezi Mungu "naomba" nisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
7. Shawalla Azan: alisema "nitahifadhi" badala ya "nitaihifadhi," pia alisema "nitalinda" badala ya "nitailinda."
8. Silima Musa Hamis: alitaja neno "sharia" badala ya "Sheria" ambalo lipo kwenye kiapo. Pia aliongeza neno "amin" ambalo halipo kwenye kiapo.
8. Salim Hassan Turkey: huyu alisema kwa mujibu wa Sheria, hakutaja neno "iliyowekwa."

Hayo ndio makosa niliyoyaona kwa leo, sikufuatilia viapo vya Waheshimiwa Wabunge jana, labda makosa hayo yalikuwepo pia.

Mimi naamini, nikiwa Mwanasheria, Waheshimiwa Wabunge waliokosea viapo vyao wanatakiwa warudie kuapa kwa mujibu wa Kanuni ya 24, Fasili ya 1 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, kama alivyorudia kuapa Rais Obama kwa Sheria za Marekani.

Tujadili.

Buchanan, kama sijakosea katika kile kiapo cha Rais Obama sio Obama aliyekosea bali Roberts ndiye aliyekosea hivyo kumfanya arudie kumuapisha tena. Ndio maana alipokuwa anakula kile kiapo utaona Obama anasita kumfuatila alivyosema Roberts kwani aligundua kuwa Roberts alikuwa amekosea!! I stand to be corrected.
 
...Hawa Ghasia alisema "....nitaitekeleza katiba...." badala ya nitaitetea Katiba. Speaker mwenyewe aliyepasa kuhakikisha maneno yanatamkwa vema, waliomweka pia wamekosea. Ndio hivyo tena mwendo mdundo kwelikweli session hii
 
Inabidi warudie hivyo viapo. Kwa kuwa pale walikuwa wanaapa kwa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sisi ndio waajiri. Spika ni msimamizi kwa niaba ya wananchi. Kwa hiyo kama hawakuapa inavyotakiwa, ni vyema wakarudia kwa kuwa kuapa si hiyari yao ni lazima
 
Sure!
 
Nadhani ilikuwa ni lazima kwa Mh.Spika awatake warudie ili kuwajengea umakini kwenye mambo ya msingi right from day one. Hali hii ya kuipotezea na hasa kwa baadhi yao ambao vijielimu ni vya taaabu! :nono:. Tusipoanza sasa ni lini????????
 
Kuna baadhi yao na hata hiyo katiba ya JMT hawaijui kwa hiyo hicho kiapo inabaki kuwa single ya kawaida tu na at the end of the day ana-sign kwenye register, yupo kwenye payroll, cool !!.

Mimi nashauri wangewaapisha ki-nursery (neno moja moja) hata kama itachukua muda mrefu ili wajue kile wanachopaswa kukisimamia.
 
Buchanan, kama sijakosea katika kile kiapo cha Rais Obama sio Obama aliyekosea bali Roberts ndiye aliyekosea hivyo kumfanya arudie kumuapisha tena. Ndio maana alipokuwa anakula kile kiapo utaona Obama anasita kumfuatila alivyosema Roberts kwani aligundua kuwa Roberts alikuwa amekosea!! I stand to be corrected.

jaji alikosea mara moja (position ya neno faithfully)
obama naye alikosea mara moja ("... to the united states..." badala ya "... of the united states....")
 
Inabidi warudie hivyo viapo. Kwa kuwa pale walikuwa wanaapa kwa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sisi ndio waajiri. Spika ni msimamizi kwa niaba ya wananchi. Kwa hiyo kama hawakuapa inavyotakiwa, ni vyema wakarudia kwa kuwa kuapa si hiyari yao ni lazima

nafikiri hata kiapo kingeondolewa tu, hakina faida yoyote, watu wanaapa na wanvynja viapo bile kuchukuliwa hatua. JK aliapa kulinda katiba lakini kaongoza kikao kilichobagua wagombea uspika juzi kwa jinsia zao? si kinyume cha katiba hapo? aliitetea sheria pale kama alivyoapa?

viapo havina maana yoyote kama nchi haiongozwi na utawala wa sheria.

i may be corrected
 
Hivi ni kwa sababu gani hivi viapo vina hii sentesi: "Ewe Mwenyezi Mungu Nisaidie". Hiki kipengele ndio kinasababisha watu kushika vitabu vya dini kama biblia au kurani wakati wa kuapa. Katiba ya nchi imetoa uhuru wa kuabudu au kutoabudu (Uwe muislamu, mkristo, mhindi, myahudi, au mpagani una haki na uhuru wa kuchagua kufuata imani au kutofuata imani yoyote ile). Jaribu kufikiria. Wahindi wanaabudu MIUNGU wengi (Gods and Goddesses). Kiapo kinalazmisha anayefuata dini ya 'Hindu' kuomba msaada kutoka kwa MUNGU mmoja! Hicho kipengele kwenye kiapo kinachomlazimisha anayeapa kuomba (kusali) nadhani ni 'unconstitutional'.

Hata doctors by profession (Medical/Veterinary) wanavyoapa wakati wa graduation, wanamalizia na "Mungu Nisaidie". Sijui kama tumerithishwa au kumweka Mungu katika utendaji inaongeza tija/ufanisi (psychologically).
 
Nakumbuka Rais Obama aliapishwa mara mbili kwa sababu alikosea kiapo chake kwa sababu ya kuweka neno "faithfully" mahali ambapo si pake! Kiapo chake kilikuwa kama ifuatavyo:
ROBERTS: I, Barack Hussein Obama...
OBAMA: I, Barack...
ROBERTS: ... do solemnly swear...
OBAMA: I, Barack Hussein Obama, do solemnly swear...
ROBERTS: ... that I will execute the office of president to the United States faithfully...
OBAMA: ... that I will execute...
ROBERTS: ... faithfully the office of president of the United States...
OBAMA: ... the office of president of the United States faithfully...

ht_obama-2nd-oath_090121_mn.jpg

Chief Justice administers oath of office again to President Barack Obama at the White House

Kwa upande wa Wabunge wetu walioapa leo, naona wengi wamekosea viapo vyao, aidha kwa kuongeza maneno au kuyaruka au kuyabadilisha, lakini Mheshimiwa Spika, Anne Semamba Makinda amekubali viapo vyao bila matatizo yoyote.

Kiapo chenyewe kina maneno yafuatayo:

"Mimi......................................................, naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba, nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie."

Wafuatao ni Wabunge waliokosea kuapa:

1. Peter Joseph Serukamba: hakutaja neno "wa Tanzania" ie alisema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano (bila kutaja wa Tanzania)...
2. Haroub Mohamed Shamis: alisema Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
3. Said Musa Zuberi: alisema "na nitaitumikia" badala ya "na kuitumikia," pia alisema Ewe Mwenyezi Mungu, "unisaidie" badala ya "nisaidie."
4. Ayoub Jacob Hashim: alianza na maneno "Bismillah Rahman Rahim" ambayo hayapo kwenye kiapo na alimalizia kwa maneno "inshallah" ambayo hayapo pia kwenye viapo.
5. Asa Osman Hamad: alisema kwa mujibu wa Sheria "iliyoweka" badala ya "iliyowekwa."
6. Hamad Zahara Ally: alisema Ewe Mwenyezi Mungu "naomba" nisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
7. Shawalla Azan: alisema "nitahifadhi" badala ya "nitaihifadhi," pia alisema "nitalinda" badala ya "nitailinda."
8. Silima Musa Hamis: alitaja neno "sharia" badala ya "Sheria" ambalo lipo kwenye kiapo. Pia aliongeza neno "amin" ambalo halipo kwenye kiapo.
8. Salim Hassan Turkey: huyu alisema kwa mujibu wa Sheria, hakutaja neno "iliyowekwa."

Hayo ndio makosa niliyoyaona kwa leo, sikufuatilia viapo vya Waheshimiwa Wabunge jana, labda makosa hayo yalikuwepo pia.

Mimi naamini, nikiwa Mwanasheria, Waheshimiwa Wabunge waliokosea viapo vyao wanatakiwa warudie kuapa kwa mujibu wa Kanuni ya 24, Fasili ya 1 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, kama alivyorudia kuapa Rais Obama kwa Sheria za Marekani.

Tujadili.

kunawatu wanalazimisha maneno ya kiislamu kwakujifanya hawajui kuapa.maneno mengine yapo kwenye dini ya kiislamu sasa nani kamwambia aweke hapo,kama walikuwa wanasoma mahali palipo andikwa hayo maneno bismilah,wametoa wapi.wanalazimisha OIC hapa.
asante mimi naitwa Ramadhani na huu ni mtazamo tu.
 
1. Stephen Ngonyani (maji marefu) strd 7
2. Livingstone Lusinde - Strd 7
3. Lameck Airo - strd 7
4. Deo Sanga (jah poeple) - strd 7

Hapa kazi ipo kweli kweli! Hivi kama wabunge wote wangekuwa strd 7 baraza la mawaziri itakuwaje? maana kwa katiba ya sasa mawaziri watatoka ndani ya bunge.
Nani waziri wa elimu?
Nani waziri wa mambo ya nje?
Nani waziri wa sheria na katiba?

Ndiyo maana ndiyo mzee nyingi.

Nilikuwa najibu neno NGUMBARU

sisiem wanafanya uzembe kwakuegemea katiba,darasa la saba hawa watakapo maliza miaka 5 watakuwa wapehitimu degree mbalimbali.
 
Jamani Hivi Wa bunge wengi ni Ngumbalu???

Usisisahau kuwa asilimia tatu (3%) ya wabunge waliharibu kura zao kwenye uchaguzi wa spika. Kiwango hicho kinalingana na kile kilichoharibu kura za urais. Hakika kuna wabunge waliharibu kura zao wenyewe.

Ukisema walikuwa nervous, ndio...........lakini ni makosa. Fikiria kama mtendaji serikalini akiiba fedha kwa kusaini cheki ya TSH 7,000,000/= badala ya TSH 700,000/=, akajitetea kuwa alikuwa nervous kuidhinisha huo mradi, atasamehewa?

Au NEC wakijibu kuwa walikuwa nervous walipokuwa wanaingiza kura kwenye jedwali wakakosea asilimia, mtakubali..............Au hivi karibuni Katibu wa Bunge akisema alikuwa nervous wakati akikokotoa "mahesabu" ya kura za uspika kiasi kwamba akakosea asilimia/kura alizopewa Mhe. Makinda, atasamehewa?

Watanzania tuamke, uozo uanaanza taratibu.
 
No question, inabidi warudiea viapo vyao.

Bado nimekuwa natafuta sheria ya viapo kuangalia legality ya rais kuapa kwa kutumia katiba badala ya msahafu. Nilikuwa na kopi yangu wakati wa sakata la Shitambala kujiapisha wakati wa uchaguzi mdogo wa Mbeya, lakini siioni tena. Kama mwanasheria Buchanan unayo kopi ya sheria hiyo naomba utuwekee hapa tujipige msasa tena.
 
Haya ndo mambo yenye tija kama mimi siijui sheria vizuri ivo inshallah sijatoka kapa bwana Buchaman thanks..
 
Tatizo ni kuwa wanaosimania kiapo na wanaokula kiapo kutojua maana yake halisi hivyo wanachofanya ni formality tu. Tunakushukuru kwa kuwakumbusha maana hawajui hata kwamba wanachofanya ni kosa kubwa.
 
Back
Top Bottom