Spika na Wabunge kumbukeni maneno haya ya Dua ya kuiombea nchi na kuliombea Bunge mnapokwenda kuuza Bandari

juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
Dua ya kuiombea nchi na kuliombea Bunge

“Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu naDunia, umeweka katika Dunia Serikali za Wanadamu naMabunge ya Mataifa ili haki yako itendeke. Twakuomba, uibariki nchi yetu idumishe uhuru, umoja, haki na amani, umjalie Rais wetu hekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri, wadumishe utawala bora. Utuongezee hekima na busara, sisi Wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wakujadili kwa dhati, mambo yatakayoletwa mbele yetu leo, ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu. Amina.

Kiapo cha Spika

:“Mimi, Tulia Ackson Mwanasasu, naapa kwamba, nitaitumikia vyema nakwa moyo thabiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zangu kama Spika wa Bunge, na katika kutimiza wajibu wa cheo hicho nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa Katiba, Kanuni za Bunge, na Sheria, Mila na Desturi za Jamhuri ya Muungano na kwa vyovyote vile sitatoa siri za Bunge. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”


Dr-Tulia-Ackson.jpg
 
Back
Top Bottom