Wabunge wazoa Sh 90mil kila mmoja kujinunulia Magari

Hongera zao, tutawafata hukohuko. maana tukipiga kelele vipi hawatakubali kupunguziwa, wanazidi kujijazia mihela tuu wakisahau wapiga kura wao, dawa kubanana 2015.
 
Na hilo gari nililoweka ni FOB... ndugu yangu ukweli ni kwamba tunafikiria kimaskini mno. mfano tunataka mbunge ananunue used car... gari jipya hiyo hela ni cha mtoto labda anunue RAV 1800cc sasa sijui kama majimbo yote ni kama Ilala... ulizeni land cruser jipya mkonga ni sh. ngapi hata bila kodi... tuweni makini kidogo.

Una uhakika gani wewe ndiye uliye makini? Au mtu atakuwa makini tu iwapo atasapoti mawazo yako? Labda nikueleze tu kwamba mkichukua hayo mashangingi kwa maelezo hayo hayo ambayo sisiemu wamekuwa wakiyatumia kujinunulia mashangingi yasiyo na tija, mtakuwa mmewakana wananchi waliowatuma mkapigane kufuta matumizi yasiyo na tija? Na hasa ukizingatia kwamba sasa hivi hiyo haitakiwi iwe kipaumbele chetu
 
Hongera zao, tutawafata hukohuko. maana tukipiga kelele vipi hawatakubali kupunguziwa, wanazidi kujijazia mihela tuu wakisahau wapiga kura wao, dawa kubanana 2015.

Naunga mkono mawazo yako mengine mama isipokuwa hayo yenye red. Hii ya kusubiri uchaguzi ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo. Uchaguzi unachakachuliwa na mafisadi ndio wanaon'gara kwa sababu wapiga kura wanajali zawadi.

Tunabanana sasa hivi, hakuna kusubiri uchaguzi
 
Na hilo gari nililoweka ni FOB... ndugu yangu ukweli ni kwamba tunafikiria kimaskini mno. mfano tunataka mbunge ananunue used car... gari jipya hiyo hela ni cha mtoto labda anunue RAV 1800cc sasa sijui kama majimbo yote ni kama Ilala... ulizeni land cruser jipya mkonga ni sh. ngapi hata bila kodi... tuweni makini kidogo.

Kuna wabunge wa viti maalumu 102 na wa kuteuliwa na rais 10 jumla 112. Unadhani wanaingia kwenye mantiki yako ya kwamba wanahitaji mashanginghi ili waweze kufikia wapiga kura? Hesabu ya haraka haraka ni bilioni 10 hizo.

Hoja hapa siyo kufikia wapiga kura kwa mashangingi bwana wakati tuko kwenye dunia ya digitali. Uwe na shangingi la milioni 90 kutembelea wananchi ambao zahanati yao haina dawa za Shilingi milioni 10 tu? Kwa nini utumie pesa nyingi sana kuwafikia wapiga kura ambao hawana maji, huduma za afya, elimu, barabara, n.k? Ili kwenda kuwapa ahadi? Walishapata ahadi za rangi na harufu mbalimbali!
 
Tuache porojo za kwenye majukwaa na dhana ya "staki nataka".Wabunge wa CDM kama kweli ni Wazalendo na njaa zao haziwazibi macho wafanye yafuatayo na wathibitishie umma wa Watanzania kuwa si sawa na CCM Club:
1.Kuamua kwa kauli moja kuzikataa ama kurudisha pesa hizo kama wamekwisha chukua.
2.Kuchukua na kuzielekeza kwenye matatizo ya Wananchi (Elimu,Afya & Ajira).
3.Kuzigawa kwa wao kupata usafiri wa bei nafuu(RAV 4) na kiasi kingine kuelekeza kwa Wananchi.

Ni mbunge mmoja wa CCM(Lameck Airo) ndiye aliyetamka kubadili matumizi ya hizo fedha kwa kununua katapila ya kuchonga barabara jimboni kwake.

Tunaomba CDM watoe tamko kati ya hayo na si porojo za "ndumilakuwili".
Halafu litakuwa mali ya JImbo lake au la kwake binafsi? Hofu yangu ni kwamba hawa wafanyabiashara siku zote hawataki kupoteza. Inawezekana ukawa mchongo wa kifisadi tu. Dili zote za ukarabati wa barabara kwenye Halmashauri hiyo zitakuwa za kwake. Ni mtazamo tu
 
Hawawezi kuzikataa. Baadhi yao kwenye kampeni wametumia zaidi ya hizo. Walikuwa wanawekeza. Sasa zinarudi. ROI kwenye siasa za Tz haisumbui sana.
Kuna baadhi ya memba hawajaliona hili...Wengi wa wabunge wana madeni kibao kutokana na uchaguzi....
 
Kama Mbunge anaweza kukopeshwa milioni 90 kila baada ya miaka mitano kwa nini tunashindwa kumpa mwanafunzi wa Engineering pale UDSM sh milioni 5 kwa miaka mitano tukaachana naye?
 
Mh. Lema mbunge wa Arusha akatatae hizo milioni 90 ili iwe mfano kwa wabunge wengine na wananchi kwa ujumla!!
achukue apelekee yatima na wenyeshida mbalimbali mkuu aaache lowasa atazitafuna (NB Lowasa imechukua nafasi ya MFISADI)
 
Kuna baadhi ya memba hawajaliona hili...Wengi wa wabunge wana madeni kibao kutokana na uchaguzi....

Nani aliwatuma wakope pesa kutafuta ubunge? Walipe kutokana na mishahara yao ambayo hata hivyo ni minono. Au wakajieleze kwa wapiga kura wao wawalipie hayo madeni kwa sababu wanawapenda ndiyo maana wakawachagua. Pesa ambazo mtu alitumia kujitafutia ubunge kwenye jimbo lake zitalipwaje na watanzania wote?
 
Halafu litakuwa mali ya JImbo lake au la kwake binafsi? Hofu yangu ni kwamba hawa wafanyabiashara siku zote hawataki kupoteza. Inawezekana ukawa mchongo wa kifisadi tu. Dili zote za ukarabati wa barabara kwenye Halmashauri hiyo zitakuwa za kwake. Ni mtazamo tu

Mkuu mawakala wa viwanda vya magari ndio wanaoamua serikali yetu itumie vipi pesa katika hili sakata. Wakishirikiana na maafisa wa serikali wanafaidi cha juu, hupanga kabisa gari ngapi za aina ngapi zitanunuliwa katika mwaka wa bajeti. Halafu mnamsikia Pinda akijisemea kwamba wanataka kupunguza ununuzi wa magari ya kifahari lakini huku yananunuliwa.

Nahisi hivi tunavyoongea wanaweza kuwa tayari wameshaanza kutangaza magari yao kwa Wabunge kwa sababu kwao hii ni biashara ya uhakika.

Ndio maana unaona hata baadhi wa wabunge kwenye hii thread wanatetea kuchukua hizo pesa na kununua mashangingi eti waweze kutembelea wapiga kura!
 
Nani aliwatuma wakope pesa kutafuta ubunge? Walipe kutokana na mishahara yao ambayo hata hivyo ni minono. Au wakajieleze kwa wapiga kura wao wawalipie hayo madeni kwa sababu wanawapenda ndiyo maana wakawachagua. Pesa ambazo mtu alitumia kujitafutia ubunge kwenye jimbo lake zitalipwaje na watanzania wote?
Walikopa wakijua hizi na nyingine zipo. Siasa za Tanzania ni uwekezaji. Ni gulio. Unanunua kura kama bidhaa nyingine yoyote sokoni.
 
Nani aliwatuma wakope pesa kutafuta ubunge? Walipe kutokana na mishahara yao ambayo hata hivyo ni minono. Au wakajieleze kwa wapiga kura wao wawalipie hayo madeni kwa sababu wanawapenda ndiyo maana wakawachagua. Pesa ambazo mtu alitumia kujitafutia ubunge kwenye jimbo lake zitalipwaje na watanzania wote?
Gari, posho na mshahara ni sehemu ya vitu unavyopata ukiwa mbunge, na hivi karibuni watajengewa na nyumba kabisa. Zaidi ya nia ya uwakilishi wa wananchi wao wana nia nyingine zaidi na ndio maana wanatumia pesa nyingi katika kampeni zao wakijua fika wakifanikiwa zitarudi tu!
 
Wabunge wetu wapige hatua moja zaidi....

Inasikitisha kwamba katika nchi hii ambayo ina struggle kukamilisha bajeti yake ya 2010/2011, hadi leo wafanyakazi wengi hawajalipwa malimbikizo ya mishahara yao, tunaweza kumpa kila mbunge milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la matairi manne kwa ajili ya kusafiria. Tunawapongeza wabunge wetu wa CHADEMA kwa kuliona hili. Sasa baada ya kuanika uozo huu hadharani, ningependa wabunge wetu wapige hatua moja mbele.

Mapendekezo yangu ni kwamba wachukue hizo fedha na wakubaliane kununua magari yasiyozidi milioni 40 au 50. Pesa inayobaki wakubaliane kutekeleza mradi mmoja wenye manufaa kwa wananchi nzima. Wanaweza, kwa mfano, kuamua kutumia hizo pesa kununua madawati katika shule zetu nyingi ambazo watoto wanakaa chini. The impact will be immerse and far reaching.

Wabunge wa CHADEMA wapo 48. Kama watakubaliana kutumia sh 45m kununua magari kila mmoja ataokoa shilingi milioni 45. Kwa ujumla wao watakuwa wameokoa sh 2,160,000,000 (zaidi ya sh. 2bn). Kwa pesa hii wataweza kununua madawati takribani 47,000 yenye uwezo wa kukalisha watoto takribani 188,000! What a service that will be to a country, and ,of course, the political gain will not be insignificant.

nimependa hoja yako lakini nadhani either hesabu imepiga chenga au bei ya hayo madawati imepanda kupita kiasi. Kwa hesabu ya numba ulizotoa; Tsh 2,160,000,000 na madawati 47,000, ina maana kuwa dawati moja ni around tsh 46,000. Je hii ni sahihi? Hawataweza kupata tenda ya kutengeneza dawati moja kwa hata sh 10,000 na hivyo kuzidisha hiyo idadi yako ya 47000x4 kufikia 188,000 na hivyo kubeba wanafunzi karibia millioni moja?
Pili, gara la mil 45 ni la aina gani?
 
Mh. Lema mbunge wa Arusha akatatae hizo milioni 90 ili iwe mfano kwa wabunge wengine na wananchi kwa ujumla!!
Sasa akizikataa zipelekwe wapi? acha achukue ni haki yake.Hakuziomba yeye bali ni wabunge waliowengi wa CCM mliowachagua wenyewe ndo walipitisha kwa wingi wao.
 
Hii topic inazua maswali kibao:
1. Je huu ni mkopo?
2. Wabunge walio na wizara nao hupewa hizi pesa? Na magari ya wizarani anatumia nani?
Mfano ni Waziri Mkuu. je huyu naye anahitaji gari?
3. Wabunge wanaorudi kwa mara nyingine, na wao hupewa hii pesa without any questions?
4. Gari la aina gani lina-gharimu Tsh Mil 90?
bei ya hizi toyota hard bodies ni kiasi gani?
Kwa hesabu ya haraka haraka kwa kuangalia idadi ya magari yatakayonunuliwa, Je sio rahisi zaidi kwa bunge kutuma order directly kiwandani ambapo wanaweza kupata discount kubwa?

Ujinga unatumaliza...
 
Sasa akizikataa zipelekwe wapi? acha achukue ni haki yake.Hakuziomba yeye bali ni wabunge waliowengi wa CCM mliowachagua wenyewe ndo walipitisha kwa wingi wao.

Mbona walitoka nje kupinga marekebisho ya definition ya kanuni ambazo wabunge wengi wa ccm walizitunga? Kwa nini Chadema wamekuwa wakiikosoa serikali kwamba wanatumia magari ya bei mbaya wakati wananchi hawana huduma? Tayari wamesahau maneno ya Dr. Slaa kwenye kampeni za uchaguzi kuhusu hili? Au ilikuwa ni mkuki kwa nguruwe?

Msitufanye mandondocha kama sisiem walivyotufanya miaka yote bana, wanatuibia kwa amani na utulivu
 
Msikatae hela maana ni halali yenu ila kama zimewazidia wasaidieni wasiojiweza maana nchi ishakuwa ya wavivu kufikiria ukikataa wanapewa wengine,bora mpokee nanyi mzigawe au mtumie
 
Kweli kuwa mbunge ni neema maana kuna wabunge ambao wana muda mrefu bungeni hivyo watatia milioni 90 mfukoni maana hawana haja ya kununua magari mapya kutokana na ya kipindi kilichopita bado wanayo.
 
Back
Top Bottom