Wabunge wazoa Sh 90mil kila mmoja kujinunulia Magari

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Wabunge wazoa Sh90mil kila mmoja

Tuesday, 15 February 2011
Mwandishi Wetu, Dodoma

JUMLA ya Sh3.24 bilioni zimelipwa kwa wabunge ili kuwawezesha kununua magari binafsi kwa ajili ya shughuli za kibunge, imeelezwa.

Kwa mujibu wa habari hizo kila mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelipwa Sh90 kwa ajili ya kujinunulia gari.

Aidha, wabunge hao wapatao 360 wamekatiwa bima ya afya inayotarajiwa kuanza kutumika kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika uzinduzi wa Tawi la Chadema, Mipango Kata ya Miyuji mkoani Dodoma wabunge wa Chadema, walisema kuwa wanashangazwa na hatua ya Rais Kikwete kuweka pikipiki za matairi matatu (Bajaji) kama moja ya vipaumbele vyake ili zitumike kubeba wajawazito wakati wabunge wanalipwa mamilioni.

Katika hotuba yake ya kulizindua bunge Kikwete alieleza mpango wa serikali yake kununua pikipiki hizo 400 zitakazosambazwa maeneo mbalimbali hasa vijijini kwa ajili ya kuwabebea wajawazito kama njia ya kupunguza matatizo ya usafiri kwenye maeneo hayo.

"Ndugu zangu hali ni mbaya, siku moja tutafanya maandamano bungeni, sio kutoka nje ya ukumbi. Inashangaza, tumepewa Sh90 milioni za magari kwa wabunge wote, huku bungeni tunajadili bajaji kuwa 'ambulance'(gari ya kubebea wagonjwa),'" alisema mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Alisema mbali na hilo katika hali inayoonyesha kuwa hospitali za serikali ni mbaya, katika semina iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni, wabunge waliomba kuwekewa bima za afya, kutibiwa nje ya nchi na katika hospitali binafsi hapa nchini.

Aliongeza kuwa: Ndoto ya kuiondoa CCM ni 'serious' (thabiti), lakini mkifanya noma ya kupata haki, hiyo imebarikiwa. Kama (CCM) wanafikiri wanaweza kuendesha nchi watakavyo, sasa hawawezi, ninyi vijana msipojitoa kwa sasa nchi itakufa."

Alikwenda mbali zaidi akisema anaomba wake za viongozi wapate ujauzito na kupakiwa katika bajaji hizo wakati wa uchungu kwenda kujifungua ili waone adha ya usafiri huo itakavyokuwa.

Akiongea katika mkutano huo naye mbunge Tundu Lissu aliwataka wananchi kutoogopa mabadiliko na kwamba historia haiheshimu watu wanaoogopa.

""Historia haiheshimu wanaoogopa, tusije kusahau bei ya mabadiliko, bei yake ni kupigwa, kufungwa hata bei kubwa zaidi ya kifo," alisema Lissu.

My take: Nakubaliana na uchungu walionao hawa makamanda, nasubiri kuona watafanyaje kuhusu hizo Sh 90mil

Asante kwa kuwatetea ila naomba nikuulize tuseme mshahara wa mbunge ni milioni 2 kama alivyosema mh Sitta:-

a. Unsecured loan yenye lowest risk ni ile ya miezi kumi na mbili so 2,000,000 x 12 = 24,000,000 (hatujaweka interest ya 20% walalahoi wanalipa kule katika mabenki)

b. Loan za kawaida zinategemea na mapato na biashara unayofanya.

Turejee katika mkopo wa wabunge:-

a. Tukicalculate Pay Back Period milioni 90 = 90,000,000/ 2,000,000 = 45 months = 3.75 almost 4 years

b. Wabunge muda wao bungeni ni 5 years.

c. Wakimaliza wanapata kiinua mgongo bungeni cha milioni kama 60,000,000.

Sasa tuulizane je wanahaki ya kupata hizo milioni 90?? for 4 years? Ni wafanyakazi wangapi wanapata mikopo hiyo? Tena mbaya zaidi ni zero interest for 4 years wakati walalahoi wanakatwa na interest inakuwaje? Vilevile nikuulize ahadi za JK za bajaji na ambulance bajaji kwa wamama wajawazito wewe unahisi ni sahihi halafu wabunge wachukue milioni 90 za kununulia mikoko ambayo tayari wanayo??

Ushauri wangu:-
a. Wabunge wasipewe mkopo wa magari wakitaka wakachukue mkopo benki wa kununua gari.
b. Wabunge wasipewe nyumba bali wapewe allowance ya nyumba ambayo hiyo ni rahisi kuwa audited na inasaidia kusave hela.
c. Wabunge wapewe allowance ya petrol na sio kujaziwa mafuta tupate kusave hela.
 
Attachments

  • MFUKO_WA_JIMBO_MGAWANYO_WA_KWANZA.pdf
    61.8 KB · Views: 210
Wabunge wamelipwa milioni 90 kwaajili yakununulia magari............... Mh. Lema mbunge wa Arusha "CHADEMA" anasema ameshangazwa na jambo hili kwani wanajadili Ambulance za Bajaji wakati wao wanapewa 90M kwaajili ya magari pia Bima ya afya kwaajili ya wabunge wanataka wapatiwe katika Hospitali Binafsi na siyo za serikali kutokana na uduni wa huduma katika Hospitali za Serikali....

Source: MWANANCHI Leo Tar: 15/02/2011
 
Kwa hiyo hizo zenye huduma duni ndo sisi wananchi tutibiwe huko? Kwali aliyeshiba hamjui mwenye njaa!!
 
Hilo la Afya wamechemsha.

Hospitali za serikali ndiyo Hospitali zitokanazo na Mipango yao Bungeni.
Kwa nini wanakimbia matokeo ya mipango yao?

Ubovu wa hospitali za serikali unatokana na Ubovu wa mikakati yao ya Afya Bungeni.

Sasa watakimbia mambo mamngapi yaliyo matokeo ya Mipango yao Bungeni??

Hivi karibuni wataomba Wanunuliwe Helcopter kwa sababu Barabara ni mbaya.

Wabunge wamelipwa milioni 90 kwaajili yakununulia magari............... Mh. Lema mbunge wa Arusha "CHADEMA" anasema ameshangazwa na jambo hili kwani wanajadili Ambulance za Bajaji wakati wao wanapewa 90M kwaajili ya magari pia Bima ya afya kwaajili ya wabunge wanataka wapatiwe katika Hospitali Binafsi na siyo za serikali kutokana na uduni wa huduma katika Hospitali za Serikali....

Source: MWANANCHI Leo Tar: 15/02/2011
 
Mh. Lema mbunge wa Arusha akatatae hizo milioni 90 ili iwe mfano kwa wabunge wengine na wananchi kwa ujumla!!
 
Hilo la Afya wamechemsha.

Hospitali za serikali ndiyo Hospitali zitokanazo na Mipango yao Bungeni.
Kwa nini wanakimbia matokeo ya mipango yao?

Ubovu wa hospitali za serikali unatokana na Ubovu wa mikakati yao ya Afya Bungeni.

Sasa watakimbia mambo mamngapi yaliyo matokeo ya Mipango yao Bungeni??

Hivi karibuni wataomba Wanunuliwe Helcopter kwa sababu Barabara ni mbaya.

Mtawajua kwa matunda yao!
 
  1. inaonyesha hata fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme hapa nchini zipo ila wanazibania tu.ukifanya hesabu ya harakaharaka unaweza ukajua kuliko serikali kununua bajaji 400 wangechukua zile fedha za magari ya wabunge wakanunua ambulance kwa kila jimbo.
  2. pili ni magari gani wanaenda kununua kwa hizo fedha?
kwa hesabu za nyepesi inatosha kabisha kwa mbunge kununuliwa nissan hard top ambayo haizidi milioni 45 that means tax exception.na fedha zinazobaki zikaelekezwa katika sehemu nyingine ambazo zingeleta tija kwa jamii

ni vizuri tukahoji ina maana wabunge waliokuwepo kwenye bunge lililopita nao wanapata tena hizo fedha za magari au inakuwaje? je ambao ni wakuu wa mikoa na wabunge pia nao wanapata tena
 
shame on them,nawalaani wooote waliopokea,hata kama wachadema nao wamepokea tena wao ndo nawalaani zaidi!!!!Lema,mbowe,sweetheart wangu mdee na mylove wangu mnyika nawaalani pia kama mmekubali hizo hela za wanyanganyi hao inhali mwajua nchi yetu na hali za watanzania zilivo ngumu!!Naomba muwe mfano......

Hela hizo mzipeleke kwenye huduma za jamii,zito kigoma watt wanakalia mawe darasani tena hata madasa wanasomea ya makuti!!UBAO NDIO HAWANA KABISA......we lema arusha vijana ajira hawana kabisa tumia hela hiyo kufanya miradi utakayotengeneza japo ajira 200...

MMH JAMANI AFYA ETI HOSPITALI BINAFSI KWAHIYO NDOMAANA HAWAZIJALI HOSPITALI ZETU HATA!!!NDO MAANA WAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WANAKUFA OVYO... NDO MAANA MWANANYAMALA IPO ILIVYO.....SABABU WAO WANATIBIWA TMJ, AGHAKAN....

MMMH.....INAUMA!!!!!!!!!!!!
 
Mh. Lema mbunge wa Arusha akatatae hizo milioni 90 ili iwe mfano kwa wabunge wengine na wananchi kwa ujumla!!

Unataka afanye kama Pinda alivyokataa shangingi wengine wakaendelea kujinafasi nalo? Na hizo akizikataa ndio zitapelekwa Mwananyamala au Muhimbili?
 
Mipango na matokeo mabovu Bungeni ndiyo inawafanya na wao wakimbie hosiptali za Serikali kutokana na mipango yao mibovu ndio maana wanataka wakatibiwe katika hosiptali za binafsi, hii yote inatokana na ubovu wa mikakati katika Sekta ya Afya, kama ndio wamenza kudai hivyo kesho watadai wabadilishiwe magari kwa kuwa hayo waliyonayo sio hadhi yao.

Wanajadili maslahi yao binafsi badala ya kujadili maslahi ya wananchi waliowatuma bungeni
 
Unataka afanye kama Pinda alivyokataa shangingi wengine wakaendelea kujinafasi nalo? Na hizo akizikataa ndio zitapelekwa Mwananyamala au Muhimbili?
Pinda naye alikuwa anajikosha tu mbona wakati gari linaagizwa hakusema chochote gari lifike ndio ulikatae??? Wakati watu wameishaingia gharama za kuliagiza halafu anasema eti Serikali inataka kubana matumizi
 
shame on them,nawalaani wooote waliopokea,hata kama wachadema nao wamepokea tena wao ndo nawalaani zaidi!!!!Lema,mbowe,sweetheart wangu mdee na mylove wangu mnyika nawaalani pia kama mmekubali hizo hela za wanyanganyi hao inhali mwajua nchi yetu na hali za watanzania zilivo ngumu!!Naomba muwe mfano......hela hizo mzipeleke kwenye huduma za jamii,zito kigoma watt wanakalia mawe darasani tena hata madasa wanasomea ya makuti!!UBAO NDIO HAWANA KABISA......we lema arusha vijana ajira hawana kabisa tumia hela hiyo kufanya miradi utakayotengeneza japo ajira 200....................
MMH JAMANI AFYA ETI HOSPITALI BINAFSI KWAHIYO NDOMAANA HAWAZIJALI HOSPITALI ZETU HATA!!!NDO MAANA WAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WANAKUFA OVYO......NDO MAANA MWANANYAMALA IPO ILIVYO.....SABABU WAO WANATIBIWA TMJ,AGHAKAN..........
MMMH.....INAUMA!!!!!!!!!!!!

Kweli, Lema zichukue ukaboreshe huduma za hospitali Arusha!
 
Hii inaonyesha kabisa kwamba wabunge wetu wanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba wanakuwa kwenye 1st class citizens wakati wapiga kura wao wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la ufukara!
 
  1. inaonyesha hata fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme hapa nchini zipo ila wanazibania tu.ukifanya hesabu ya harakaharaka unaweza ukajua kuliko serikali kununua bajaji 400 wangechukua zile fedha za magari ya wabunge wakanunua ambulance kwa kila jimbo.
  2. pili ni magari gani wanaenda kununua kwa hizo fedha?
kwa hesabu za nyepesi inatosha kabisha kwa mbunge kununuliwa nissan hard top ambayo haizidi milioni 45 that means tax exception.na fedha zinazobaki zikaelekezwa katika sehemu nyingine ambazo zingeleta tija kwa jamii

ni vizuri tukahoji ina maana wabunge waliokuwepo kwenye bunge lililopita nao wanapata tena hizo fedha za magari au inakuwaje? je ambao ni wakuu wa mikoa na wabunge pia nao wanapata tena

Unauliza maswali mazuri na hilo la mwisho ni zuri zaidi. iweje wabunge wa zamani na wapya wote wapewe pesa za magari? Labda watu wa ofisi ya bunge watupe ufafanuzi. Na vipaumbele vyetu ni huduma kwa wananchi au ni welfare ya wanasiasa?
 
Hii inaonyesha kabisa kwamba wabunge wetu wanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba wanakuwa kwenye 1st class citizens wakati wapiga kura wao wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la ufukara!

Ndiyo maana wanakuwa wakali sana kwa mtu yeyote anayehamasisha wananchi kudai haki yao na kuhoji maamuzi mabovu ya serikali, kama haya ya kununulia wabunge magari ya kifahari na kupeleka bakuli kwa wafadhili kuomba wachangie huduma na miradi ya jamii. Kwamba anahatarisha amani na utulivu!!!!
 
Mrs Mallaba:Are you coming to vote? The polling station will be closing in an hour.
Mr Mallaba :It's raining!
Mrs Mallaba:So what?
Mr Mallaba: I can't be bothered. It doesn't matter who I vote for, we always end up worse off. They're all as bad as each other.
Mrs Mallaba:Well don't complain to me if you don't like the policies of whoever wins.
Mr Mallaba:I don't think anyone will win. They're predicting a hung parliament.
Mrs Mallaba:Well if no one bothers to vote, I guess they'll be right. I'll be back in ten.
 
24 bln!!!..wakati wa kampeni walitembea kwa miguu? hebu nenda mwananyamala wodi ya wazazi uone kufuru hii,one bed wamama 4 na vichanga..
ubunge sio ajira..kama kweli wapo kihalali kila mbunge achangiwe na wapiga kura wake wa jimboni waliomchagua..sasa mbunge wa ilala anapewa gari yenye thamani sawa na mbunge wa Nkasi kusikokuwa na lami hata ya maonyesho!
 
Hilo la Afya wamechemsha.

Hospitali za serikali ndiyo Hospitali zitokanazo na Mipango yao Bungeni.
Kwa nini wanakimbia matokeo ya mipango yao?

Ubovu wa hospitali za serikali unatokana na Ubovu wa mikakati yao ya Afya Bungeni.

Sasa watakimbia mambo mamngapi yaliyo matokeo ya Mipango yao Bungeni??

Hivi karibuni wataomba Wanunuliwe Helcopter kwa sababu Barabara ni mbaya.

Yaani nimeipenda sana logic yako.
Ndiyo maana tangu wiki iliyopita ninafanyia kazi tija na ufanisi wa bunge na wabunge.
Hizi ndizo sababu zilizowapelekea watunisi na wamisri kutumia nguvu ya umma.
Kwa sababu una uchaguzi ambao matokeo ya uchaguzi ni kinyume cha matakwa ya wananchi na una bunge ambalo ni rubber stamp, wanafanya uvuvuzela zaidi kuliko kushikisha serikali adabu.
 
Back
Top Bottom