Wabunge wangi wa CCM hawajui kujadili na hawawezi kujenga hoja

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
1. Bajeti ya serikali ikisomwa bungeni, wabunge wanapaswa kusikiliza kwa makini, kuisoma na kuielewa ili waweze kuchangia/kuijadili vizuri.

2. Kambi Rasmi ya Ushindani bungeni inatoa bajeti mbadala kwa ile ya serikali kwa kukosowa vipengere ambavyo Kambi imeona serikali imeshindwa kuviona na kuonesha namna gani vinaweza kutekelezwa. Kambi Rasmi ya Ushindani inaweza isikosowe au kupendekeza mambo mapya kama yote yanayotakiwa yako kwenye hotuba ya serikali. Labda tu pale inapohitajika kusisitiza zaidi.

3. Baada ya haya, majadiliano yanaanza. Huu ni muda, ambao wabunge wanatoa mawazo yao kwa kuonesha ni mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa kwenye bajeti. Yanaweza yakawa yale yaliyoletwa na serikali na yale ya Kambi Rasmi ya Ushindani.

4. Kujadili maana yake ni kuchangia hoja (kuonesha mazuri na mabaya ya bajeti) na na siyo kumshambulia mtu kwa yale aliyochangia kwani ni mawazo yake na wewe changia ya kwako. Kumshambulia mtu siyo kutoa hoja bali ni kwenda nje ya hoja.

5. Kama kuna sababu ya kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya maeneo kwenye bajeti, kazi hii inafanywa na mawaziri/manaibu/mwanasheria mkuu wa serikali.

6. Kwa hiyo, baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa wakikosa mwelekeo kwa kuanza kuwashambulia wabunge wa Kambi Rasmi ya Ushindani kwa mapendekezo yao mbadala. Mbunge anapaswa kuchangia kile tu achoona na kuamini kitajenga taifa letu na kitaondoa kero za wapiga kura wake. Nje ya haya ni kupoteza muda na kutojua nini kichangiwe. Nina hakika wabunge wa CCM wakisoma points hizi na hata wabunge kutoka vyama vingine, itasaidia kuboresha michango ya wabunge. Mbunge siyo msemaji wa serikali – kazi yake ni kuikosoa, kuishauri na kuisimamia serikali iboreshe untendaji na iwajibike vizuri zaidi.
 
1. Bajeti ya serikali ikisomwa bungeni, wabunge wanapaswa kusikiliza kwa makini, kuisoma na kuielewa ili waweze kuchangia/kuijadili vizuri.2. Kambi Rasmi ya Ushindani bungeni inatoa bajeti mbadala kwa ile ya serikali kwa kukosowa vipengere ambavyo Kambi imeona serikali imeshindwa kuviona na kuonesha namna gani vinaweza kutekelezwa. Kambi Rasmi ya Ushindani inaweza isikosowe au kupendekeza mambo mapya kama yote yanayotakiwa yako kwenye hotuba ya serikali. Labda tu pale inapohitajika kusisitiza zaidi.3. Baada ya haya, majadiliano yanaanza. Huu ni muda, ambao wabunge wanatoa mawazo yao kwa kuonesha ni mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa kwenye bajeti. Yanaweza yakawa yale yaliyoletwa na serikali na yale ya Kambi Rasmi ya Ushindani.4. Kujadili maana yake ni kuchangia hoja (kuonesha mazuri na mabaya ya bajeti) na na siyo kumshambulia mtu kwa yale aliyochangia kwani ni mawazo yake na wewe changia ya kwako. Kumshambulia mtu siyo kutoa hoja bali ni kwenda nje ya hoja.5. Kama kuna sababu ya kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya maeneo kwenye bajeti, kazi hii inafanywa na mawaziri/manaibu/mwanasheria mkuu wa serikali.6. Kwa hiyo, baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa wakikosa mwelekeo kwa kuanza kuwashambulia wabunge wa Kambi Rasmi ya Ushindani kwa mapendekezo yao mbadala. Mbunge anapaswa kuchangia kile tu achoona na kuamini kitajenga taifa letu na kitaondoa kero za wapiga kura wake. Nje ya haya ni kupoteza muda na kutojua nini kichangiwe. Nina hakika wabunge wa CCM wakisoma points hizi na hata wabunge kutoka vyama vingine, itasaidia kuboresha michango ya wabunge. Mbunge siyo msemaji wa serikali – kazi yake ni kuikosoa, kuishauri na kuisimamia serikali iboreshe untendaji na iwajibike vizuri zaidi.

Weka paragraphs isomeke kwa urahisi zaidi.
 
1. bajeti ya serikali ikisomwa bungeni, wabunge wanapaswa kusikiliza kwa makini, kuisoma na kuielewa ili waweze kuchangia/kuijadili vizuri.

2. kambi rasmi ya ushindani bungeni inatoa bajeti mbadala kwa ile ya serikali kwa kukosowa vipengere ambavyo kambi imeona serikali imeshindwa kuviona na kuonesha namna gani vinaweza kutekelezwa. Kambi rasmi ya ushindani inaweza isikosowe au kupendekeza mambo mapya kama yote yanayotakiwa yako kwenye hotuba ya serikali. Labda tu pale inapohitajika kusisitiza zaidi.

3. baada ya haya, majadiliano yanaanza. Huu ni muda, ambao wabunge wanatoa mawazo yao kwa kuonesha ni mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa kwenye bajeti. Yanaweza yakawa yale yaliyoletwa na serikali na yale ya kambi rasmi ya ushindani.

4. kujadili maana yake ni kuchangia hoja (kuonesha mazuri na mabaya ya bajeti) na na siyo kumshambulia mtu kwa yale aliyochangia kwani ni mawazo yake na wewe changia ya kwako. Kumshambulia mtu siyo kutoa hoja bali ni kwenda nje ya hoja.

5. kama kuna sababu ya kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya maeneo kwenye bajeti, kazi hii inafanywa na mawaziri/manaibu/mwanasheria mkuu wa serikali.

6. kwa hiyo, baadhi ya wabunge wa ccm wamekuwa wakikosa mwelekeo kwa kuanza kuwashambulia wabunge wa kambi rasmi ya ushindani kwa mapendekezo yao mbadala. Mbunge anapaswa kuchangia kile tu achoona na kuamini kitajenga taifa letu na kitaondoa kero za wapiga kura wake. Nje ya haya ni kupoteza muda na kutojua nini kichangiwe. Nina hakika wabunge wa ccm wakisoma points hizi na hata wabunge kutoka vyama vingine, itasaidia kuboresha michango ya wabunge. Mbunge siyo msemaji wa serikali – kazi yake ni kuikosoa, kuishauri na kuisimamia serikali iboreshe untendaji na iwajibike vizuri zaidi.
ni kweli kabisa.nimeshuhudia katika maeneo kadhaa hapa mjini iringa mfano katika kumbi za vyuo na katika baa mahali ambapo tv huwekwa,anapochangia hoja mbunge wa upinzani watu huwa makini kumsikiliza lakini akichangia mbunge wa ccm hakuna anayemzingatia.
 
Back
Top Bottom