Wabunge wanasemaje kuhusu Maji ya ziwa victoria kutokana na msimamo wa Misri?

Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,003
83
Wakubwa, sisi wengine hatupo hapo bongo kwa sasa, kutokana na kazi zetu. Nilikuwa naomba kuuliza, hivi bunge la tz linakaa lini? na kama tayari, WABUNGE WANALIONGELEAJE SUALA LA TZ KUTUMIA MAJI YA ZIWA VICTORIA, kutokana na msimamo wa Misri? tunataka kuwasikia wabunge wakiongea hili. na tunataka waliongelee bungeni. nimesoma baadhi ya threads humu, nimeona inauma. kwamba watz singinda, shinyanga, Dodoma na maeneo mengine ya Arusha etc, wanakunywa maji ya topa, wakati kulikuwa na uwezekano wa kuwavutia maji wakanywa, wakauza wakamwagilia hadi kwenye vitalu vya mashamba yao.....hivi anayetunza ziwa victoria ni nani? ni Misri au tz, hivi ziwa victoria liko Misri?hivi mbona wanatuchezea hivi? rais wetu yuko wapi, na ajitokeze basi kuliongelea hili, tunamtaka aliongelee, au ndo kama wengine wanavyosema, anawaabudu hao watoto wa mamdogo....kwa hili asipoangalia, litagawa wengi. ujumbe kwa vyama vya upinzani, tunaoma chukueni hili kama silaha nzito juu ya kikwete kwenye kampeni za uchaguzi mwaka huu, mtwangeni nayo hadi atoe maelezo kuhusu msimamo wake, kwasababu kama yeye anaenda kwenye birthday za kina Gadafi, si wote tz tunamfagilia huyu gaidi wa Libya, pamoja na rafiki zake wa Sudan na misri. la sivyo, aachie ngazi, kuna wengi tu tunaweza kuongoza nchi na kutetea maslahi ya nchi. period. inaudhi sana.
 
Hili jambo hata mimi nimeliwazia sana, nikitamani serikali itoe tamko rasmi lakini inaelekea se3rikali ya Kikwete ina uhusiano wa karibu sana na hizi nchi za kaskazini mwa Afrika. Lakini sasa hata wabunge hawalizungumzii?
 
Tunahitaji Rais kama Vladmil Putin....lakini kwa mkwere....mh hakuna lolote hapo akienda libya anapewa tende anakula anajiona kama vile watanzania ni matajiri kuliko hata libya.......ovyo!!!
 
Jamani hili jambo linazungumzwa. Misri haiwezi kutukataza kutumia maji ya Victoria. Mikataba wanayoishuparia waliingia na Waingereza siyo na Tanzania huru. Nakumbuka Lowassa akiwa bado WM aliliweka wazi hilo Misri ilipolalamikia mradi wa kupeleka maji ya Victoria huko Shinyanga/Kahama. Huu mradi umeishakamilika na maji yameishaanza kutumika lakini kama ada kuna matatizo ya hapa na pale. Katika majadiliano ya kimataifa mara nyingi kila nchi huanza na msimamo mkali lakini hii huwa inalenga kupata muafaka unaoridhisha pande zote mbili - acceptable middle ground. Victoria ni chanzo cha Mto Nile na ndio life blood ya Misri. Wana haki ya kuwa concerned lakini hawawezi kuzipa nchi nyingine masharti magumu.
 
the issue sio kujadili, kujadili na nani? tuanze kujadili na mtu wakati maji yapo kwetu na watu wetu wanakunywa matope, na chaajabu zaidi, badala ya kuja kwa heshima, wanakuja kwa kututisha, hivi watz tunatishika kirahisi tu hivi ehee, yaani wamisri wanatoa vitisho na sisi tumenyamaza tu. viongozi wetu wanatuwakilisha nini sasa, hivi kikwete yupo kweli, au amesafiri. nimeona picha zake zingine akiwa amepiga na Gadafi, hivi hawa waarabu wanatusaidia nini? mnataka kuigawa nchi ninyi CCM, mi sitaki kusema hapa, mbona inakera kutawaliwa na mwarabuuuuu,
 
Back
Top Bottom