Wabunge wa Upinzani watoka bungeni wakiwa wameziba midomo yao

Nafikiri hapa bila kuweka itikadi za vyama vyetu ni bora bunge letu lifikirie njia sahihi ya kumaliza
tofauti zao kwa sababu tusipende kudharau tuu Upinzani.Kumbuka kuna faida nyingi tuu za Upinzani pale Bungeni ambazo
zinaonekana wazi japo wao sio wenye serikali, ila changamoto zao zinasaidia sana chama Tawala, mfano Elimu bure hii ni sera ya Upinzani, hakuna mtu ambae angejua kuna takatata inayoitwa Escrow, Lugumi kama siyo Upinzani. Hivyo kubalance mambo nyeti kama bageti vyama vya upinzani vina umuhimu pia kuwepo pale bungeni !! Nasema haya nikiwa namaanisha nilielewa vizuri lile somo la civics form two "Importance of Multipart system "
 
Pamoja na Kasoro nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza hapa na pale kutokana na ubovu wa Serikali yetu hii ya Awamu ya Tano, lakini hili la Kupuuzia mambo ya msingi especial suala la Huyu Naibu spika kutaitia Doa kubwa sana Serikali yetu Pendwa.

Hofu yangu ni kuwa Budget inayo pita sasa inapitishwa pasipo kuwa na analysis yeyote, wala angalizo, kwasababu Wabunge wengi wa CCM ni wabovu katika kusoma, kuelewa na kufuatilia effects za budget husika na hivyo kuwepo na uwezekano wa kupitishwa budget isiyo na mashiko kwasababu tu za kishabiki.

Swali ninalojiuliza mimi ni kuwa inamaana Bunge limeshindwa kabisa kuchukua hatua stahiki kwa kuangalia nani mkosaji kati ya Naibu spika na Wabunge asilimia 42% ya wabunge wote Tanzania? Je Mtu mmoja anaweza akasingiziwa na hawa watu wote ambao ni watu wazima wenye akili Timamu?

Je Nihasara ipi ambayo Bunge inaiingiza Serikali kwa kuto changamana na Akili pevu kama yakina Tundulisu, Kina Mbatia, Zitokabwe kina Halima Mdee, Nasari Joshua na wengine wengi? Ni kweli Bunge limeshindwa kufikiria Uwakilish wa wananchi usivyo tendewa haki na Mtu mmoja tu ambaye hupigiwa kura na wabunge wachache Bungeni, kuhariu Interest ya Nchi nzima?

USHAURI WANGU
Bunge na Kamati zake, ziweke chini ushabiki wa kisiasa, watafute suluhu ili Wananchi wapate uwakilishi sawasawa na wabunge wengine.

Hii hata ningekuwa Mimi kama ukinipuuza ningetoka tu, hakuna haja ya kuendelea kukaa Bungeni kujadili vitu na watu ambao uwezo wao ni mdogo then wanataka kuniambukiza na Mimi.
 
Sawa, wamefungwa midomo ya kusema; hakuna namna.
ifike wakati haya mambo yaishe, yanatia hasira.
 
Hili bunge kwa ujumla naona kama wanatuchezea tu wananchi,wameshindwaje kukaa na kuyamaliza wakati wanakutana baa na kuongea vizuri haswa,,so shame bunge la tz
 
Bunge naona bado lipo kwenye kampeni mkuu !! Naona wamesahau kuwa wanafanya mambo nyeti yanayohusu
Watanzania kwa Ujumla. Kila kitu kinafanyika kwa Sifa !! Nchi zilizoendelea hazina haya Mambo
 
Bungeni hawasikilizwi sasa wafanyeje?
Watasikilizwa wakijenga hoja za msingi zenye mashiko. Na wengi tutawaunga mkono zikikataliwa. Kama kuna kanuni za bunge zinazowanyima uhuru wa kuongea/kuwasilisha hoja zao, wao ndo wenye uwezo wa kuzibadilisha.
 
Msikilize vizuri Mbatia utapata jibu.
Mbatia amekuwa bungeni muda na pia kwa hisani ya Rais, aliweza kuleta hoja za kubadilisha kanuni za bunge zinazominya uhuru wao. Aache unafiki kwa kuwa tunamheshimu kwa misemo yake "mama Tanzania". Ni Mh ambaye hatutegemei achochee kutokutii sheria ambazo ameshiriki kuzitunga au ana uwezo wa kuzibadilisha kama Mbunge
 
Hivi hawa ukawa kweli wana akili sawa sawa leo naona wame-edit staili yao ya kutoka bungeni kwa kubandika makaratai kwenye midomo yao sasa sijui hasa walichokuwa wanamaanisha wakati tuliambiwa hakuna aliye wazuia kuingia bungeni ni utashi wao wenyewe

Sasa naanza kuliona kaburi la upinzani 2020 sijui kama watatoboa tena hawa dah kweli za kuambiwa changanya na zako tangu wameaambiwa hawataki kuchanganya zao
Kwanini akili zetu ziko hivi ?
 
Hili jina Tulia lina maana gani? Majina mengine watoto hupewa kutokana na jinsi walivyokuwa utotoni. Kwa nini alipewa hili jina? Alikuwa hatulii, au lilikuwa na maana fulani katika lugha yake ya asili?

Laana siyo tu pale mnaponyimwa mvua au kupewa mvua kupita kiasi. Kuna wakati Muumba hutoa laana kwa jamii fulani kwa kuipa watawala watakaowatesa na kuwanyanyasa. Tumwombe Mungu ili kama ni laana, basi atuepushie, nasi tupate neema ya kupata viongozi wenye manufaa kwa kila mtu, kama wale wenzetu wa Botswana.
 
Mbatia amekuwa bungeni muda na pia kwa hisani ya Rais, aliweza kuleta hoja za kubadilisha kanuni za bunge zinazominya uhuru wao. Aache unafiki kwa kuwa tunamheshimu kwa misemo yake "mama Tanzania". Ni Mh ambaye hatutegemei achochee kutokutii sheria ambazo ameshiriki kuzitunga au ana uwezo wa kuzibadilisha kama Mbunge
Kwanini hatuwezi kufikiri mbali ?
 
Mnaumiaje sasa kwa sababu hata wanachochangia hakisikilizwi hata hao wa CCM wanaobaki hawana hawana cha kukuongezea wewe mwananchi wa kawaida.

Yaani inaonesha JF kuna watu wengine ni watoto, hata ukiangalia comments zao bado hazijakomaa....Utakuta mtu anauliza swali la kijinga ambalo mtu mzima haulizi bila hata kusoma.
 
Hivi hawa ukawa kweli wana akili sawa sawa leo naona wame-edit staili yao ya kutoka bungeni kwa kubandika makaratai kwenye midomo yao sasa sijui hasa walichokuwa wanamaanisha wakati tuliambiwa hakuna aliye wazuia kuingia bungeni ni utashi wao wenyewe

Sasa naanza kuliona kaburi la upinzani 2020 sijui kama watatoboa tena hawa dah kweli za kuambiwa changanya na zako tangu wameaambiwa hawataki kuchanganya zao
Huna akili timamu wewe sijui nani amekuruhu uje hapa JF
 
Hakuna kuweka suluhu, Dk Tulia aendelea kukaza tu, kama wapinzani wanadhani wanamkomoa Dk Tulia ni wajinga, hasara ni kwa waTz waliowapigia kura, 2020 si mbali, tutasikia malalamiko mengi ya tulishindwa kufanya tuliyo ahidi kwa sababu tulibanwa.

Unaijua kazi ya Mbunge?
 
Pamoja na Kasoro nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza hapa na pale kutokana na ubovu wa Serikali yetu hii ya Awamu ya Tano, lakini hili la Kupuuzia mambo ya msingi especial suala la Huyu Naibu spika kutaitia Doa kubwa sana Serikali yetu Pendwa.

Hofu yangu ni kuwa Budget inayo pita sasa inapitishwa pasipo kuwa na analysis yeyote, wala angalizo, kwasababu Wabunge wengi wa CCM ni wabovu katika kusoma, kuelewa na kufuatilia effects za budget husika na hivyo kuwepo na uwezekano wa kupitishwa budget isiyo na mashiko kwasababu tu za kishabiki.

Swali ninalojiuliza mimi ni kuwa inamaana Bunge limeshindwa kabisa kuchukua hatua stahiki kwa kuangalia nani mkosaji kati ya Naibu spika na Wabunge asilimia 42% ya wabunge wote Tanzania? Je Mtu mmoja anaweza akasingiziwa na hawa watu wote ambao ni watu wazima wenye akili Timamu?

Je Nihasara ipi ambayo Bunge inaiingiza Serikali kwa kuto changamana na Akili pevu kama yakina Tundulisu, Kina Mbatia, Zitokabwe kina Halima Mdee, Nasari Joshua na wengine wengi? Ni kweli Bunge limeshindwa kufikiria Uwakilish wa wananchi usivyo tendewa haki na Mtu mmoja tu ambaye hupigiwa kura na wabunge wachache Bungeni, kuhariu Interest ya Nchi nzima?

USHAURI WANGU
Bunge na Kamati zake, ziweke chini ushabiki wa kisiasa, watafute suluhu ili Wananchi wapate uwakilishi sawasawa na wabunge wengine.

Hii hata ningekuwa Mimi kama ukinipuuza ningetoka tu, hakuna haja ya kuendelea kukaa Bungeni kujadili vitu na watu ambao uwezo wao ni mdogo then wanataka kuniambukiza na Mimi.
Hio Katiba mpya mnayoitaka itatekelezwa vipi kama watu watakua hawataki kufuata sheria????

Yani watu wakatae kufuata utaratibu na kanuni za bunge na kiongozi(spika) awaangalie tu....hii hapana jamani...kama tunataka maendeleo ya kweli sharti tupate viongozi mithili ya Dr. Tulia otherwise tutaendelea kupiga marktime kwenye maendeleo...
 
Naibu Spika ameaibikaje sasa, yaani waache kuaibika waliofanya huo utoto aibike Naibu Spika, hebu tuache ushabiki wa kimbeya mbeya!
Ni aibu sana kwa serikali, ubabe hauna sifa jambo la muhimu kwa nchi ya demokrasia ni kukaa mezani kama alivyokuwa anafanya spika wa bunge lilipita la 2005-2015. Mh Anna Makinda.
 
Back
Top Bottom