Umuhimu wa Wabunge wa Upinzani Bungeni

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
23,529
70,400
Ifikie mahali Watanzania wote tukubaliane kuwa hata kama chama tawala hampendi upinzani lakini kuna umuhimu wa wabunge wao kuwepo bungeni.

Fikiri kuhusu hizi tozo zinazoumiza ambazo zimeongezwa katika bei za mafuta, voucher na katika huduma za pesa kwa njia ya simu. Tukubali kabisa kuwa wangekuwepo upunzani ndani ya bunge lazima wangepigia kelele unyonyaji huu na kututetea sisi wananchi wao. Sio hawa wa CCM ambao kila mswaada/pendekezo wao wanapitisha tu kwa maslahi yao binafsi.

Kwasasa walipo wote hawana uchungu wowote na wananchi tunaoumizwa kwa kuongezeka kwa kodi kila siku bila maisha yetu kuwa na nafuu yoyote. Yani tozo zinaongezwa lakini huduma bado ni mbovu na zinazidi kuwa mbovu kila siku.

Wabunge wa CCM wao hawaoni mateso wanayoyapata walipa kodi zaidi kabisa wanadai kuongezewa mishahara. Kwanza wao hawakatwi kodi mishahara yao, bado wana mishahara zaidi ya mmoja, posho za vikao kila kona, safiri kila kukicha, allowance za usafiri, makazi, mawasiliano, bima za afya n.k. Pesa yote ya kuwalipa na kuwagharamikia ni majasho ya walalahoi.

Hao hao bado hawajafanya kupiga deal za magendo. Wao wanaishi maisha kama wapo peponi na familia zao wakati wavuja jasho wakianza kuvuja jasho la damu. Hakuna anaejali.

Lakini watu wenye nia njema na nchi hii ndio kila siku husingiziwa kuwa wanatumika na mabeberu kwasababu tu wanawatetea walalahoi na kufichua wizi wa wachache waliojimilikisha nchi.

Inaumiza sana hawa hawa wabunge wanapitisha uozo huu kuwaumiza wananchi halafu kipindi cha uchaguzi wanarudi tena kuomba kura na ahadi nyingi sana za uongo. Bila wapinzani bungeni tutaendelea kuumia kila siku.
 
Kodi hii Haikatwi kwa watanzania wote makato haya ni wapinzani tu.

Au Nadanganya CCM wenzangu?.
Wangeweza kuibagua,wenye mawazo mbadala wangekoma,kwani kijani hawaaminiki iwe ,utawala gani.
 
Kweli kabisa, ifike mahali Bunge liwe 51:49 in favour of upinzani. Huu upumbavu wa hawa wanyonyaji utaisha kwa namna hii...
Ila hayo yatawezekana kwa kurejelewa kwa katiba pendekezwa ya mzee wetu,jaji mzalendo wa kweli jaji Warioba.
 
Yani bado unamashaka na upinzani kwa Kikundi hichi cha Majizi , wanaongelea KATIBA upo kimya kima wewe , wamesema malipo ya viongozi upo kimya kima wewe n.k
Upinzani unaoongizwa na wezi wa magari wa zamani?
 
Back
Top Bottom