Wabunge wa CCM wakataa Kuunga Mkono hoja ya Kujadili Mgomo wa Madaktari

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Mheshimiwa Ndugulile na Mnyika walitoa hoja ya dharura kujadili mgomo wa madaktari maana watanzania wanakufa, kwa maana kuwa waahirishe kazi nyingine za Bunge ili wajadili jambo hili la muhimu. Bahati mbaya hoja zao hazikuungwa mkono wa wabunge kwa kusimama.

Ndipo Naibu Spika Ndugai akasema ni kweli hoja zao zina nguvu na wamefuata kanuni ya 47 ya taratibu za Bunge, Kanuni hii inasema hivi;

KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA 2007

47.-(1) Baada ya Muda wa Maswali kwisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwa Shughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye Orodha ya Shughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

(2) Hoja ya namna hiyo itakuwa ni maalumu na inaweza kutolewa wakati wowote hata kama majadiliano yatakuwa yanaendelea.
(3) Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge
kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

(4) Iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura, halisi na lina maslahi kwa umma, basi ataruhusu hoja hiyo itolewe kwa
muda usiozidi dakika tano na mjadala juu ya hoja hiyo utaendelea kwa muda ambao Spika ataona unafaa kwa kuzingatia mazingira ya suala linalojadiliwa.


Ila tatizo hazijaungwa mkono, kwa hiyo tunaendelea na kazi za kawaida.Ndipo wabunge wakachekelea kwa vicheko vya raha mustarehe utadhani ni jambo la kufurahia. Na nina shaka kuwa serikali inawachezea madaktari, nawaomba endeleeni kukaza uzi kama kawaida. Madam Spika anachelewesha kuruhusu tamko la serikali juu ya hili akiwa na uhakika kuwa madaktari watarudi kazini.

Naomba kazeni buti.

 
Jamani bunge linaendelea na huyu naibu spika kaombwa mwongozo kuhusu mgomo wa madaktari kapotezea. Alieomba ni daktari mbunge wa kigamboni na mbunge wa ubungo. Jamani..mbona bunge linakwepa hii ishu?
 
Hao hawana uchungu tumbo likivuruga wanakimbilia India
 
Hujaeleza kwa uwazi kapotezeaje? Lete kitu kamili ili watu wakuelewe maana tunaoangalia TV tuko wengi na maelezo ya Naibu Speaker yameeleweka?
 
Katika hali isiyotarajiwa mh Ndugai amekataa kuruhu wabunge kujadili mgomo wa madaktari kwa hati ya dharura.Baada ya maswali na majibu wabunge Ndugulile na Mnyika waliomba mwongozo lakini naibu spika kagoma eti wabunge wengine hawajaunga mkono, halafu wabunge ccm wanashangalia wakati watanzania wenzetu wanaendelea kuumia na kufa. Is this Tanzania we want?
 
Jamani bunge linaendelea na huyu naibu spika kaombwa mwongozo kuhusu mgomo wa madaktari kapotezea. Alieomba ni daktari mbunge wa kigamboni na mbunge wa ubungo. Jamani..mbona bunge linakwepa hii ishu?

Andika lugha sanifu ueleweke, vinginevyo ulichoandika ni uozo!
 
Hujaeleza kwa uwazi kapotezeaje? Lete kitu kamili ili watu wakuelewe maana tunaoangalia TV tuko wengi na maelezo ya Naibu Speaker yameeleweka?
  • Baada ya kipindi cha maswali na majibu kwisha,Speaker aka step down na naibu spika akachukua nafasi.
  • Kutokana na kanuni ya 47 ya bunge,ulikua wakati wasaa wa kuwasilisha mwongozo.
  • Wakajitokeza wabunge wawili kuomba mwongozo; 1.Ndungulile na 2.Mnyika-wote waliomba kujadili ishu ya madaktari kwani ni urgent.
  • Ndugai akakubaliana nao kwamba wametumia kanuni vizuri lakiniiiii hoja zao hazikuungwa mkono.
My take
Baada ya wabunge hao wawili kutoa hoja wabunge hawakuulizwa kama wanaunga mkono hoja.Ndugai ameizima hoja kiubabe.
 
kama aliwahonga wapiga kura wake,wakampigia kura ina maana alinunua ubunge kwa hiyo sasa mbunge wa aina hiyo ambao ni wengi wanahangaika kurudisha walicho honga,hawana habari na shida za wapiga kura wao.
 
Watanzania wenzangu hivi wooote tunaukumbuka huu wimbo????

Tanzania, Tanzania, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE (!!!!?????????)
nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana (!!!!!!?????)
NILALAPO NAKUOTA WEWE, NIAMKAPO NI HERI MAMA WE (!!!!!!!!??????)
 
The system failed to cater for Doctors,
The Government failed to listen and talk to Doctors,
The Parliament has failed to even discuss the issue........
THERE WILL NO BE SOLUTION ON THE SAGA AND ITS SISI TUNAOKUFA!!
LETS BE SERIUS........
KESHO.
 
Back
Top Bottom