Wababe wameishia wapi? zamani kulikuwa na wababe kwelikweli mtaani kila mtu anamuogopa

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,969
6,460
Nakumbuka mtaani kwetu jamaa mmoja wakati huo, kwa sasa ni mzee alikuwa na uwezo wa kuja shambani kwako asubuhi akachukua mazao na akaondoka hata ukimshtaki hakuna wa kuthubutu kuongea hiyo kesi.

Kuna ule ubabe wa mashuleni wa kutumana sukari, sabuni, maandazi kwa sh. 200 na chinchi urudishe
Tunaenda kwenye kizazi cha namna gani? Wako wapi watu hawa?

Kwa kifupi siku hizi hakuna wababe watu wanabeba vyuma tu hawaexpose ubabe wao mtaani.
 
zamani palikuwa na ubabe wakiboya sana ..visu nje nje ..kama machinjoni
 
Aiseee kitaan kwetu kulikuwa na hilo jamaa linaitwa marwa ninja, duuuh lilikuwa ni noma, yaaan vijana wote kitaan walikuwa wanaligwaya, ikipigwa ndondo cup timu yake ikifungwa refa lazima atoe penati kabla game haijaisha ili timu yake ishinde, ila tangu ilipoletwa kanda maalum Tarime jamaa akapigwa jela 3years alivyotoka kawa RAIA mwema.
 
zamani palikuwa na ubabe wakiboya sana ..visu nje nje ..kama machinjoni
Aaah umenikumbusha jamaa yangu walimtishiaga kisu arusha,
bodaboda kamtoa stend pale akampeleka Nakumati mahali pa buku 1, boda akataka buku 10 kwa kisu
 
Aaah umenikumbusha jamaa yangu walimtishiaga kisu arusha,
bodaboda kamtoa stend pale akampeleka Nakumati mahali pa buku 1, boda akataka buku 10 kwa kisu
hiiiii hahaaaa ...umeona sasa ...yaani nakumbuka mnamo miaka ya 94 mitaani palikuwa na uhuni wakishamba kabisa...watu wanapigana visu na viwembe ama chupa hadharani ..wakati huo bar palikuwaga na viti vile vya Chuma ...basii usiombee ugomv utokee bar ..daahhh viti vyageuka kuwa silaha watu wanapasuana vibaya
 
Kinondoni ...kulikuwa na wababe Wakina bob chura(rip)po,Paul siza(tip),Juma ngedere
Ukienda migomigo utamkuta wakati Huo Jamaa alikuwa mbabe anaitwa stiba,
Ukienda manzese kuna mbabe alikuwa anaitwa santana......
Kulikuwa na mbabe mmoja nakumbuka anaitwa wandiba(rip)

Siku Hzi ubabe utamfanyia nani maana kila mtu Yuko resi na maisha

Ova
 
Nakumbuka form one niliwahi kukamatwa na wababe wa form two wakanipeleka chooni nikaambiwa niwapigie wazazi wangu simu kwenye tundu la choo kuwa nimekamatwa na magaidi iyo ilikuwa mwaka 1998
Unamaanisha shithole ya trampu?
 
Wanume wa mikoani wanapenda vitu vya kijinga. Sa ubabe wa nini akati umeambiwa hii dunia ni akili tuu. Sasa hivi pigana uone kama hujamalizia hela polisi na mahakamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom