Wababa mliotelekeza watoto subirini mpaka mtafutwe na watoto wenu, acheni usumbufu!

Anaandika, Robert Heriel

Sakata la Ommy Dimpoz na baba yake linanifanya na mimi nipigilie msumari kusisitiza.

Kuna wanaume wenye tabia za kizamani kuwa ati, anaacha kwa makusudi kabisa kulea mtoto wake halafu anakuwa na mtazamo kuwa; "Akikua atanitafuta, atamtafuta baba yake". Hiyo tabia ipo na baadhi ya sisi wanaume.

Mtoto haramu,
Mtoto wa uzinzi,
Mtoto wa single mother,
Mtoto chokoraa,
Mtoto asiye na baba,
Mtoto wa nje!

Na majina mengine kama hayo licha ya kuwa yalikuwa adhabu kwa mtoto wako, hukupata muda wa kumfariji na kumuonyeshea ukaribu wako kama baba. Wewe kama baba ukachangia kwa sehemu kubwa kumuumiza mtoto kwa kile kiitwacho kutafuta maisha, kile kiitwacho ujana, kile kiitwacho magomvi yako na mama yake na sababu zingine.

Leo mtoto anakuwa, anajiweza, unafikiri atakuheshimu, unafikiri atakupenda, unafikiri atakuchukulia wewe ni baba yake? Kama wewe hukumchukulia kama mtoto wake ni ngumu yeye kukuchukulia kama baba yake. Yeye anakuona kama watu wengine, kama wewe ulivyomuona kama watoto wengine.

Ooh! Hujajua maisha, ooh huyo ni baba yako. Ndiyo ni baba lakini simchukulii kama baba, kama yeye alivyokuwa hanichukulii kama mwanaye. Mila na desturi za kijingajinga kuendekeza upuuzi ndiyo zimeifikisha Afrika hapa ilipo. Unafiki unafiki kila mahali.

Kama ulisema mtoto atakutafuta kaa usubiri mpaka utafutwe na mwanao sio usubiri amekua na kujiweza ndio uanze kumsumbua dogo.

Na dunia ilivyombaya sasa, yule uliyemtelekeza ndio Mungu anapigilia baraka hukohuko, ili akufundishe.
Mtoto wako ambaye mara nyingi ulikuwa unamuona hana msaada kwako ndiye mara nyingi baadaye huwa jiwe kuu la msingi katika sehemu ambayo wengine wote hawana uwezo wa kukusaidia.

Wanaume tujitahidi kulea watoto wetu, iwe waliozaliwa kwa bahati nasibu au wale tuliopanga. Na kama tutaamua kutelekeza basi tusisumbue watoto wetu tuliowatelekeza.

Msamaha sio lazima. Msamaha ni neema tuu ambayo siyo haki ya mkosaji. Hivyo mtoto atakavyotuchukulia ni sawa tuu, tusiwe watu wa kulalamika.

Huwezi hukumiwa na Mungu kwa kushindwa kusamehe watu. Hakuna sheria ya hivyo. Kama vile Mungu anavyosamehe apendavyo ndivyo na wewe/mimi unatoa msamaha vile upendavyo na siyo kwa shinikizo.

Mwisho, watoto waliotelekezwa kama itawapendeza mnaweza wasamehe wazazi wenu. Ingawaje najua hakuna uwezekano wa kuwa na ukaribu au mazoea ya mzazi aliyekutelekeza. Siyo baba tu hata mama. Kama hajakulea ni ngumu kuwa na ukaribu na upendo naye.

Hivyo ndivyo karma inavyofanya kazi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
huu msumari wa moto sana natamani baba yangu angekuja kuusoma... amenivuruga utotoni baadae nishakuwa mkubwa amekuja kusikia mwanaye nipo zangu canada nakula maisha anahangaika kuwasumbua ndugu kutaka nimtafute how comes? ikiwa alinitelekeza mimi na mama yangu mzazi ? ubarikiwee
 
Hizi mambo zimewahi kunikuta nikiwa mdogo,baada ya kuachana wazazi,mama yangu hakutaka msaada wowote ule wa baba,ilifikia hatua hata mshua akileta nguo alizichoma moto,baadae mshua akaamua kukaa pembeni na kutojihusisha na kutoa matunzo yoyote yale kwangu,ulipofika umri wa shule alinipa majina ya baba wa kambo aliyemuoa wakati huo,nilisoma mpaka chuo kikuu nikitumia hayo majina,nimebahtika kupata ajira,sasa nikipata kidgo namtumia biological father,hiyo hali ya kumtumia pesa baba yangu mzazi,mama yangu imekuwa inamkera mno ni vile tu nimekuwa mtu mzima anashindwa kunikemea au kunipangia ila anaumia sana! So wakati mwengine mama zetu huchangia hiyo hali,ndo maana mimi siwezi kutupa lawama kwa baba yake dimpoz,hatujui huko walikuwaje na mzazi mwenzake.

Unafikiri Ommy Dimpoz ni mjinga au Hana haki au Hana akili Kama wewe?

scenario yako na ommy ni mbingu na Ardhi.
Umemaliza Chuo lakini unashindwa kuona utofauti wa Stori ya Ommy Dimpo na yako. Kweli elimu haimfanyi mtu kuwa na uwezo wa kuchambua Mambo.

Wewe Baba yako alikuwa anania na anaonyesha Nia yake na upendo wako kwako lakini Mama alikuwa anakataa,
OmmyDimpo maelezo yake ni kuwa Mzee Hakuwa na time naye.

Ommy Dimpo yupo wazi Kabisa kuwa yupo tayari kupata Laana kama anakosea wewe bado huoni tuu.
 
Wanawake ndio wanamezesha sumu. Mtoto wangu wa kwanza mama yake anampa sumu sana kuhusu mimi wakati huwa namtafuta kwenda kumjulia hali na hela natoa ila mama sababu tuna ugomvi anaihamisha hadi kwa mtoto.

Nami kwa jeuri hata akinikataa huko mbele ni poa tu.

Yaani mtoto umhudumie alafu apandikizwe chuki ikubali? Hiyo haliwezekaniki!
WATOTO wanaakili, wanaona, wanasikia,
Wanajua Mama anakosea, au Baba anakosea.

Ukionana na mwanao mpe pesa yeye, mpe vitu yeye alafu uone mama hizo sumu za Mama yake zitafanya kazi.

Mama akimuambia Baba yako hakuhudumii alafu kweli humhudumii hiyo sio sumu, huo ni ukweli anamuambia ili aone kuwa anababa asiyejielewa.

Wanaume lazima tubadilike
 
Ndio mama yako alivyofanya?

Muulize Mama yake akifanya Jambo Baya au Baba yake akifanya Jambo Baya Hana uwezo wa kuliona?

Ni kweli mtoto anaweza kudanganywa lakini kuna umri akifika hasa umri wa kupevuka anaanza kujua mbivu na mbichi.

Tukubali tuu kuwa kama kuna watoto tumetelekeza iwe Kwa sababu yoyote basi tukubali matokeo tuu
 
Nimemuuliza makusudi najua hajalelewa na mama ila watu kama huyu ndio wanaongeza kusema akina mama wanapandikiza chuki Kwa watoto.
 
Na wewe mama yako alikupandikiza chuki?
Sana tu! Tena ilifikia hatua wakishirikiana na baba wa kambo ambaye nilikuwa natumia majina yake shuleni,walikuwa wananimbia negative kuhusu mzee,mara mshirikina,nikimuona nisimsalimie,na kweli ilifika kipindi nikienda likizo kumuona auncle,akija nilikuwa simsalimii kabisa! Na nilikuwa namkimbia.hahahaha
 
Hizi mambo zimewahi kunikuta nikiwa mdogo,baada ya kuachana wazazi,mama yangu hakutaka msaada wowote ule wa baba,ilifikia hatua hata mshua akileta nguo alizichoma moto,baadae mshua akaamua kukaa pembeni na kutojihusisha na kutoa matunzo yoyote yale kwangu,ulipofika umri wa shule alinipa majina ya baba wa kambo aliyemuoa wakati huo,nilisoma mpaka chuo kikuu nikitumia hayo majina,nimebahtika kupata ajira,sasa nikipata kidgo namtumia biological father,hiyo hali ya kumtumia pesa baba yangu mzazi,mama yangu imekuwa inamkera mno ni vile tu nimekuwa mtu mzima anashindwa kunikemea au kunipangia ila anaumia sana! So wakati mwengine mama zetu huchangia hiyo hali,ndo maana mimi siwezi kutupa lawama kwa baba yake dimpoz,hatujui huko walikuwaje na mzazi mwenzake.

Hii ndio comment ya kikubwa kabisa imekaa poa sana wengine wanakoment kwa mihemko tu
 
Omy dimpoz atakua anaujua ukweli, achukue hatua stahiki kulingana na ukweli wake.Na inaonekana media ndo zimewaunganisha tunamuachia yeye ndo mwanuzi wa mwisho.
 
Back
Top Bottom