Wababa mliotelekeza watoto subirini mpaka mtafutwe na watoto wenu, acheni usumbufu!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,405
52,046
Anaandika, Robert Heriel

Sakata la Ommy Dimpoz na baba yake linanifanya na mimi nipigilie msumari kusisitiza.

Kuna wanaume wenye tabia za kizamani kuwa ati, anaacha kwa makusudi kabisa kulea mtoto wake halafu anakuwa na mtazamo kuwa; "Akikua atanitafuta, atamtafuta baba yake". Hiyo tabia ipo na baadhi ya sisi wanaume.

Mtoto haramu,
Mtoto wa uzinzi,
Mtoto wa single mother,
Mtoto chokoraa,
Mtoto asiye na baba,
Mtoto wa nje!

Na majina mengine kama hayo licha ya kuwa yalikuwa adhabu kwa mtoto wako, hukupata muda wa kumfariji na kumuonyeshea ukaribu wako kama baba. Wewe kama baba ukachangia kwa sehemu kubwa kumuumiza mtoto kwa kile kiitwacho kutafuta maisha, kile kiitwacho ujana, kile kiitwacho magomvi yako na mama yake na sababu zingine.

Leo mtoto anakuwa, anajiweza, unafikiri atakuheshimu, unafikiri atakupenda, unafikiri atakuchukulia wewe ni baba yake? Kama wewe hukumchukulia kama mtoto wake ni ngumu yeye kukuchukulia kama baba yake. Yeye anakuona kama watu wengine, kama wewe ulivyomuona kama watoto wengine.

Ooh! Hujajua maisha, ooh huyo ni baba yako. Ndiyo ni baba lakini simchukulii kama baba, kama yeye alivyokuwa hanichukulii kama mwanaye. Mila na desturi za kijingajinga kuendekeza upuuzi ndiyo zimeifikisha Afrika hapa ilipo. Unafiki unafiki kila mahali.

Kama ulisema mtoto atakutafuta kaa usubiri mpaka utafutwe na mwanao sio usubiri amekua na kujiweza ndio uanze kumsumbua dogo.

Na dunia ilivyombaya sasa, yule uliyemtelekeza ndio Mungu anapigilia baraka hukohuko, ili akufundishe.
Mtoto wako ambaye mara nyingi ulikuwa unamuona hana msaada kwako ndiye mara nyingi baadaye huwa jiwe kuu la msingi katika sehemu ambayo wengine wote hawana uwezo wa kukusaidia.

Wanaume tujitahidi kulea watoto wetu, iwe waliozaliwa kwa bahati nasibu au wale tuliopanga. Na kama tutaamua kutelekeza basi tusisumbue watoto wetu tuliowatelekeza.

Msamaha sio lazima. Msamaha ni neema tuu ambayo siyo haki ya mkosaji. Hivyo mtoto atakavyotuchukulia ni sawa tuu, tusiwe watu wa kulalamika.

Huwezi hukumiwa na Mungu kwa kushindwa kusamehe watu. Hakuna sheria ya hivyo. Kama vile Mungu anavyosamehe apendavyo ndivyo na wewe/mimi unatoa msamaha vile upendavyo na siyo kwa shinikizo.

Mwisho, watoto waliotelekezwa kama itawapendeza mnaweza wasamehe wazazi wenu. Ingawaje najua hakuna uwezekano wa kuwa na ukaribu au mazoea ya mzazi aliyekutelekeza. Siyo baba tu hata mama. Kama hajakulea ni ngumu kuwa na ukaribu na upendo naye.

Hivyo ndivyo karma inavyofanya kazi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom