Waarabu hawakuwa Wakoloni Afrika?

Waarabu hawakuwa wakoloni Afrika. hilo ni jibu tosha.

Usichanganye Uarabu kama ni Taifa fulani, Uarabu ni lugha zaidi ya Taifa. Kama vile Mswahili, mswahili si Taifa. Nadhani umenipata.

Hao wengine wote uliowataja ni mataifa ambayo yanaweza kuwa na koloni lake. Kama si Taifa huwezi kuwa na koloni. Simpo.

Very interesting. Sikuwa nimeangalia hii dhana kwa muktadha huu. Je ni sahihi pia kusema kuwa uzungu ni zaidi ya lugha na hivyo wazungu hawakuwahi kuwa wakoloni afrika?
 
Naona hujanielewa, nimekuambia Uarabu sio Utaifa kwa maana hiyo sio nchi. Uarabu ni lugha. Sasa kama Lugha ya Kiarabu imefanya koloni Afrika basi lugha ya Kiswahili imefanya koloni Afrika Mashariki na inaendelea kukuza koloni lake. Sijui umenielewa au?

Hapo kakuelewa majibu kuntu!
 
teh teh teh! Waarabu wabaya sana coz walishiriki kuwauza Maniga huko ufaransa,uingereza,marekani{kwa mabwana zenu wazungu ambao mnawaona wema }lakini aliogopa kuwapeleka kule arabuni coz biashara hiyo ilikuwa haramu.. Lakini Waarabu ndo wakoloni pekee walo"zaa" na dada zenu weusi na kuish nao kama wake zao...
.
.
Namaliza kwa kusema kuwa waarabu walikuwa wakoloni "waungwana" walotuletea Uislam

Heeh! hivi kumbe kuna wakoloni waungwana na wasiokuwa waungwana? Vipi wajerumani waliotujengea reli ya kati na bandari na kuleta imani ya ukristo wa killutheri nchini je nao ni wakoloni waungwana?
 
Historia ya Afrika ya zamani haijakamilika vizuri.Tukichukulia mantiki ya neno ukoloni kwatasifiri ya Colonial histographers unaweza sema kuwa waarabu hawakuwai fanya hivyo.
Lakini pia ukitumia uweridi na uelewa zaidi utaona kuwa waarabu alifanya ukoloni hapa Afrika mfano ni hapa tu Zanzibar sultan kutoka Oman alikuwa na dora na mfumo wote wa serikali.
Ukienda Afrika kasikazini mfano Misri na Libya utakuta kuwa waarabu ndo wakwanza kutawala sehemu hizo na waingereza na wafaransa wamewatoa waarabu kutawala hapo.
 
Very interesting. Sikuwa nimeangalia hii dhana kwa muktadha huu. Je ni sahihi pia kusema kuwa uzungu ni zaidi ya lugha na hivyo wazungu hawakuwahi kuwa wakoloni afrika?

Wazungu ni utambulisho na inasemekana hilo ni neno la kibantu likimaanisha waliotoka kwa Mungu, kwani historia inatufundisha kuwa hawa wazungu walikuwa wakija hapa kwa kueneza neno la mungu na kurusedi ndio iliwafikisha huku.

Ukisema wazungu wamewahi au hawajawahi kuwa wakoloni wa Afrika si sahihi na Uarabu, Uzungu si lugha Uarabu ni lugha. Wazungu kama mataifa waliwahi kuwa na makoloni si Afrika tu bali sehemu mbali mbali duniani.
 
Jamani Ukoloni ni neno au ni matendo??
 
Historia ya Afrika ya zamani haijakamilika vizuri.Tukichukulia mantiki ya neno ukoloni kwatasifiri ya Colonial histographers unaweza sema kuwa waarabu hawakuwai fanya hivyo.
Lakini pia ukitumia uweridi na uelewa zaidi utaona kuwa waarabu alifanya ukoloni hapa Afrika mfano ni hapa tu Zanzibar sultan kutoka Oman alikuwa na dora na mfumo wote wa serikali.
Ukienda Afrika kasikazini mfano Misri na Libya utakuta kuwa waarabu ndo wakwanza kutawala sehemu hizo na waingereza na wafaransa wamewatoa waarabu kutawala hapo.

Hayo unayabadilisha sijui kwanini? Zanzibar ni "Zenj Empire" ambayo ilikuwa na himaya hadi Oman, hakukuwa na himaya ya Oman.
 
Waarabu walikuwa wafanya biashara. Waliuza kuanzia watu mpaka pembe za ndovu. Na hawa jamaa walivyo na akili mbovu walikuwa wanawahasi wanaume waliowakamata kama watumwa kisha wakawauza sehemu mbalimbali wakafanye kazi.
Bagamoyo na Kilwa, kuna historia ya kutosha kuonyesha nini walikuwa wanafanya
 
Jibu swali la msingi je Waarabu hawakuwa wakoloni afrika?
 
Jamani Ukoloni ni neno au ni matendo??

In politics and history, a colony is a territory under the immediate political control of a state.
source: Colony - Wikipedia, the free encyclopedia

[h=2]col·o·ny[/h]   [kol-uh-nee] Show IPA
noun, plural -nies. 1.a group of people who leave their native country to form in a new land a settlement subject to, or connected with, the parent nation.

2.the country or district settled or colonized: Many Western nations are former European colonies.

3.any people or territory separated from but subject to a ruling power.

4.the Colonies, those British colonies that formed the original 13 states of the United States: New Hampshire, Massachusetts, Rhode Island, Connecticut, New York, New Jersey, Pennsylvania, Delaware, Maryland, Virginia, North Carolina, South Carolina, and Georgia.

5.a number of people coming from the same country, or speaking the same language, residing in a foreign country or city, or a particular section of it; enclave: the Polish colony in Israel; the American colony in Paris.

Source: Colony | Define Colony at Dictionary.com

Naona kwa tafsiri hizo zilizo wazi kabisa utaelewa kuwa Waarabu hawajawahi kuwa koloni kwani hawa "qualify" kwenye vigezo.
 
Ukisema wazungu wamewahi au hawajawahi kuwa wakoloni wa Afrika si sahihi na Uarabu, Uzungu si lugha Uarabu ni lugha. Wazungu kama mataifa waliwahi kuwa na makoloni si Afrika tu bali sehemu mbali mbali duniani.
Hivi Kila anayeongea kiarabu ni mwarabu? Maana nafikir ukisema uarabu ni Lugha sikuelewi kabisa.
 
Waarabu walikuwa wafanya biashara. Waliuza kuanzia watu mpaka pembe za ndovu. Na hawa jamaa walivyo na akili mbovu walikuwa wanawahasi wanaume waliowakamata kama watumwa kisha wakawauza sehemu mbalimbali wakafanye kazi.
Bagamoyo na Kilwa, kuna historia ya kutosha kuonyesha nini walikuwa wanafanya

Hivi inakuingia akilini hivi vijitu vinavyoongea Kiarabu vije kuwakamata vikaka vya Kibantu kwao? mnhhh, hapa kuna kasoro kubwa sana inabidi tuiweke sawa kwa kufunguwa akili zilizokuwa "brain washed".
 
Hivi Kila anayeongea kiarabu ni mwarabu? Maana nafikir ukisema uarabu ni Lugha sikuelewi kabisa.

Hapana, si kila anaeongea Kiarabu ni Mwarabu, kila ambae Lugha yake ya asili ni Kiarabu basi ni Mwarabu. Kwa lugha ya asili nadhani unanielewa nna maanisha nini. Unaweza ukawa na asili ya lugha ya Kiarabu lakini hukijui, unakuwa si Mwaarabu bali una asili ya Kiarabu.
 
Hivi inakuingia akilini hivi vijitu vinavyoongea Kiarabu vije kuwakamata vikaka vya Kibantu kwao? mnhhh, hapa kuna kasoro kubwa sana inabidi tuiweke sawa kwa kufunguwa akili zilizokuwa "brain washed".

Na wewe unataka kutu - Brainwash ?
 
Hapana, si kila anaeongea Kiarabu ni Mwarabu, kila ambae Lugha yake ya asili ni Kiarabu basi ni Mwarabu. Kwa lugha ya asili nadhani unanielewa nna maanisha nini. Unaweza ukawa na asili ya lugha ya Kiarabu lakini hukijui, unakuwa si Mwaarabu bali una asili ya Kiarabu.
Kwa hiyo uarabu si lugha pekee bali ni sehemu ya uarabu. Desturi Mila, asili, tamaduni na nchi wakati mwingine ndivyo vinajenga utaifa wa mtu. Kwa maana nyingine waarabu ndiyo tuliwaona wakija Afrika na wala si Lugha yao ililetwa Afrika.
 
Hivi inakuingia akilini hivi vijitu vinavyoongea Kiarabu vije kuwakamata vikaka vya Kibantu kwao? mnhhh, hapa kuna kasoro kubwa sana inabidi tuiweke sawa kwa kufunguwa akili zilizokuwa "brain washed".

Nani amenibrain wash? Huo ndio ukweli maana sio suala la kutunga. Wanyamwezi na waha waliipata kubebeshwa mizigo mizito ya pembe za ndovu na baadae kuhasiwa kabla ya kuuzwa kwenda kufanya kazi majuu..sijui ndo Oman hiyo unayoisema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom