Waandishi wa habari wakacha mkutano ulioitishwa na naibu waziri wizara ya uchukuzi

Tatizo halikuwa kusubiri ila ni mazingira yenyewe ya kusubiri yaliyokuwepo pale, waandishi walitelekezwa kana kwamba ni watu ambao hawana maana, waandishi walikaa pale nusu saa na hakuna aliyekuwa anaenda kuwapa taarifa ya kuchelewa ilionyesha kuwa ni jinsi gani waandishi wanadharaulika wakati wao ndio wamewaweka hao viongozi hapo walipo. Napenda kuwashauri waandishi kuwa na umoja na kuona kuwa hata wao ni mawaziri katika department waliopo hakuna kutoa nafasi ya kudharaulika na pia waandishi wasikubali kutumiwa kama Condom.
 
hao waandishi nao walikua na zao..tangu lini hapa bongo mkutano na waandishi wa habari ukaanza on time? haijawahi kutokea sasa wanalalamika nini...hawa walikua na lao leo
 
Walikuwa wanawahi sehemu nyingine ambayo ina vibahasha.
Waandishi wa habari wa bongo wacha kabisa..wanaendekeza njaa ni balaa. Kama kuna semina watachakachua hata pipi na karanga za wageni waalikwa, tena bila haya! wengine ni masharobaro & masista du kimuonekano lakini loh hawana hata mshipa wa aibu na lugha yao ya 'sasa unaniachaje?' wakiitwa mahali wakiona hakieleweki wanakusanya ma-tripod yao wanatokomea kwene 'next target' na taarifa yako ndio imechinjiwa baharini hata iwe na umuhimu kiasi gani kwa umma wa walipakodi, mi nafikiri ni wakati Takukuru & TRA ziwaangalie hawa jamaa kwa macho matatu.
 
Back
Top Bottom