Waandishi kujitosa kwenye siasa - ujanja au ujinga?

Jun 8, 2011
52
19
Natupa memory zangu nyuma i think ni 2008 kuna mwandishi mmoja anakwenda kwa jina la Rosemary Mwakitangwe aliwahi kuandika makala kwenye the number one newspaper in Tanzania almaarufu kama Raia Mwema akihoji mantiki ya wanahabari kujitosa kwenye siasa.

Sasa hapa jamvini kuna waandishi wengi Mwanakijiji na wenzake naomba mtweleze hivi baadhi yenu kama Nkamia mnapojitosa kwenye siasa mna maana gani? mnaenda kuharakisha ukombozi au kujiongezea kipato?

Sasa wote mkikimbilia huko nani atawesemea wanyonge? kwa maana mimi naamini vyombo vya habari ni mhimili wa kwanza wa jamii yoyote tofauti na upuuzi wa baadhi ya wanasiasa kuwa ni mhimili wa nne!

NAOMBA JIBU WANA JF
 
mbona umewaona waandishi peke yao wakati bungeni kuna walimu,madaktari,wanaimba hip hop,taarabu,wahandisi,wachumi nk.
siasa ni kwa kila mtu mkuu na si kwamba ukiwa mwandishi inakuondolea sifa.
tafakari.
 
Hii si kwa wanahabari peke yao, dhana nzima ya uongozi imepotea kabisa katika nchi yetu.

Nionavyo mimi: Kundi fulani la wanajamii linapendezwa na uzalendo, utashi, haiba na uwezo wa ndugu X katika kusimamia maslahi yao kisha wanamshawishi, kumpendekeza na hatimaye kumchagua kuwa mwakilishi wao.

Au basi walau: Ndugu Y anakerwa matatizo katika jamii inayomzunguka, anakuwa na upeo kisha wito wa kujitoa katika kuyatatua kisha anaomba ridhaa na ushirikiano wa wanajamii yake wamwezeshe kusimama mstari wa mbele katika utatuzi.

Lakini walio wengi: Ndugu Z anagundua kwamba ili afikie malengo yake inabidi apate wadhifa fulani. Kisha anaanza harakati zake ikiwa ni pamoja na kushawishi, kuahidi, kujiweka karibu na kundi fulani na hata kuwekeza mali kwa dhamira ya kuupata huo wadhifa.

Epuka sana akina Z.
 
Back
Top Bottom