Vyuo vikuu wampendekeza January Makamba kuwa Rais ajaye

Ni aibu kwa mtu mwenye akili sawasawa kufanya ujinga huo mbali ya kujiita wasomi. Ni aibu kubwa kwa nchi na chama walichotoka hao wanaojiita wasomi wa sampuli hiyo. Vyuo vikuu ni sehemu ya watu wenye akili ya kufikiri, kuchambua matatizo katika jamii na kuyapatia majibu ya kitaalamu. Licha ya hivyo, jamii zote zilizoendelea duniani zilitumia sana vyuo vikuu kama taasisi kuu ya kutengeneza viongozi katika ngazi mbalimbali. Narudia kutengeneza viongozi na sio kupiga kura ya eti nani awe rais. Hivi hawa ndio watu tunaowategemea kuwa ndio msingi wa taifa lijalo kweli? Napata shida sana, yaani kwa tamko lao hawa ni masalia ya wanafunzi /mediocre students na si wanafunzi wa chuo kikuu chochote. Kama akili kama hizi zipo vyuoni kwa sasa basi hata hivyo vyuo vyao ni "glorified high schools and not universities"

kamanda naona unapiga 'pentagon' tehe tehe tehe tehe.....
 
Kumbe Urais imekuwa ni kazi ya kawaida kabisa eee; sioni ni kigezo gani kinachotumika kumpendekeza mtu awe rais wa nchi yetu?

Je anaweza kutekeleza haya kwa vitendo?

a) Utetezi wake kwa wanyone, hasa wananchi wa kipato cha chini
b) Ushiriki wake katika vita dhidi ya ufisadi, wizi wa mali za umma, Madawa ya kulevya nk
c) Ushiriki wake katika kujenga uchumi hasa kwa wananchi wa kipato cha chini - akianzia jimboni kwake kwa akitumia kauli mbiu ya kilimo kwanza.

Tunahitaji Rais ambaye walau aweze kusimamia yafuatayo
1. Kupunguza matumizi ya serikali, kusimamia uwajibikaji
2. Kunyenyua kilimo kuanzia ngazi ya kaya (kilimo kirudi kuwa ndio uti wa mgogo wa uchumi wetu.
3. Kutetea haki za wafanyakazi hasa waalimu, madaktari na mapolice wenye vyeo vya chini
4. Kusimamia elimu ya Tanzania, kurudisha hadhi ya shule za serikali kuwanzia msingi hadi vyuo vikuu
5. Kuboresha sekta ya afya nchini
 
huyo february makamba hana hata sifa za kuwa m/kiti wa mtaa kwa watu wanaojielewa kama huku kwetu labda huko bumbuli tu
 
ha ha ha ha h aha ha ha! wanajiita wasomi hata ikiwaambia waandike michangnua inayoweza kuisadia inchi kuendelea hmna hata moja atayeleta kitu cha maana........
 
Ujumbe muhimu ninaouona hapa ni kwamba WASOMI wetu hawa wanasema CCM ndio chama kinachopaswa kuiongozi Tanzania towards a brighter tomorrow...

Tumia kipimo cha miaka 50 ya SISIEMU madarakani na maendeleo duni ya nchi kisha useme kama nchi haihitaji mabadiliko ya mfumo wa utwala.
 
Dickson Ng'hily,
Mie niliisha jua nini kitafuata katika maazimio ya huo mkutano wa Jumamosi.
Mpaka pale Vijana watakapo kuwa tayari kufanya maamuzi kwa utashi na akili yao ndo watastahili kushiriki uongozi na si kushirikishwa! Ukichunguza hata huo mkutano ni wa "kushirikishwa" kama huamini subiri Tamko baada ya mkutano.
attachment.php
 
Huwa nawasikia mkisema ccm hakuna vijana wasomi. Sasa mkuu hawa wametoka wapi?

He he mkuu na fikiri umekuwa mbali na siasa za elimu ya juu siku hizi baada ya vyama vya upinzani kujikita kwenye vijana na hasa wa vyuo vikuu kwa miaka kama mi nne nyuma, ccm wali gundua kuwa fikira za wao kupata ushindi kwa kupitia uwt,pamoja na watu wa vijijini na wazee, kuwa zipo ukingoni then ndio wakarudi na wao kwenye vyuo vikuu kutafuta wanachama wao kwa nguvu zote, kwani hukumbuki kuna wanachama wao fulani ambao wapo kwenye chuo kikuu fulani ndio walitoa pesa ya kwenda kuchukua fomu za kugombea urais wa rais wa sasa Dr JK.

Hivyo hivi sasa wanavijana vyuo vikuu ila nimejaribu kufatilia kwa karibu asilimia kubwa ya vijana hawa hata baada ya kuwa viongozi lakini na wao huwa wanaingia kwenye ile cancer ya ufisadi kwa kuiba pesa za mfuko wa wanafunzi au kutumia vibaya kule kuaminiwa kwao.
 
eti hawa ndio wasomi tunaowategemea hayo ni mawazo yenu au ya taasisi mnazoziongoza

ni mawazo yao wenyewe na sio ya taasisi na wala ya wanafunzi wao. Kingine mbona marais wa vyuo vingine hawakuhusishwa? Na taarifa hawakupata? Mfano sua na mzumbe. Inakuwaje hapo.
 
safari hii inawezezekana huu umoja unaongozwa na matahira, ivi hawa watoto wamesoma katiba ya taifa ili?au wanasema tanzania ipi iyo?? Huo umoja ni wa kitoto sana,sijui kwa nini wanakosa muda wa kusoma na kuanza ujinga huo. Katiba pamoja na madiliko ya katiba yametaja hadi umri wa mgombea,ila vijana 'wasomi' wanajifanya mbu mara tatu,yani mbumbumbu kwa kujifanya hawajawahi kumsikilza mzee warioba na tume yake,ambayo obvious ndo itatupa katiba mpya.
Watoto kasome
 
Kuna maraisi wengi kuna rais wa masharobaro,rais wa sinza mariaga,kuna rais wa madalali kuna rais wa mapresenter sam misago kuna poor people's president mchomvu kuna rais wa akudo bella kuna rais wa fm akademia nyoshi sasa huyo january wamempendekeza awe rais wa tegeta?


Hapo kwenye red: Labda anapendekezwa kuwa rais wa mashangingi (rejea huyo anayebusu picha yake). Hii ni siasa au mahaba? Tanzania kuna tatizo la msingi nalo ni uwezo mdogo wa raia wake kifikra. Kama taifa hatuna budi kulijadili hili jambo kwa mapana yake kuliko kuendelea kuwa taifa la majuha namna hii. Hawa vijana kwa akili yao ndogo wapo tayari kupendekeza mvuta bange mwenzao kwa kuwa tuu wanakutanaga kwenye vijiwe vyao na night clubs.
 
hii tabia ya wanafunzi wa elimu ya juu kujiita wasomi inanisumbua sana, vyama vyao vyote hivyo viongozi wao ni undergraduate halafu wanajiita wasomi!hivi usomi wao huwa ni kitu gani kilicholeta tija kwa jamii, zaidi ya kujumuika kwenye hizo taasisi na kuutafuta huo usomi? Tukirudi kwenye mada huyo waliyempigia kura ameleta mchango chanya upi kwenye serikali? amepitia mapito gani yakuweza kumchunguza kuwa kweli ataweza kuyakabili majukumu ya uraisi, wahenga walisema mkate bila kupitia kwenye tanuri la moto aislani hauwezi kuiva? sasa huyu mtu wao kapitia tanuri gani? URAISI SI LELEMAMA KAMA MADESA NYIE WANAFUNZI MJIITAO WASOMI!

wanafunzi wa zama hizi wengi ni vilaza and they dont know what they are doing, their lore to the sosciety and waseme nini na wasiseme nini, kiujumla watoto wa enzi hizi wako kimaslahi zaidi! Sijui ndio shule a kata hizo?
 
Jamani watanzania usomi na kumiliki vyetu ni vitu tofauti,hawa wanavyeti lakini walivipata kwa kubebwa sio wasomi kama wanaotoka harvard
 
Hawa vijana wamepoteza mwelekeo. Utashi wao utatimia tu endapo wataandikisha umoja wao kama chama cha siasa halafu ndipo wamsimamishe JM
 
Back
Top Bottom