Vyuo vikuu wampendekeza January Makamba kuwa Rais ajaye

View attachment 107667
Caption: Mmoja wa Mashabiki wa January Makamba, akibusu picha ya Mbunge huyo aliyoitumia wakati wa kampeni za Ubunge mwaka 2010.

UMOJA wa viongozi wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania umempendekeza Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, kuwa ndio anayefaa kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kwakuwa hajawai kuhusishwa na kashfa za rushwa na ufisadi .


Umoja huo unakusudia kutembea nchi nzima kwajili ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba katika kinyanganyiro cha na nafasi ya urais katika uchaguzi ujao kwakuwa ndio kiongozi atakayeleta matumaini mapya.

Akitoa tamko la Umoja huo wa vyuo vikuu baada ya kumaliza mkutano wa siku mbili wa viongozi hao wa Vyuo vikuu 21 hapa nchini,Rais wa Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya,Theonest Theophily,alisema Makamba amechaguliwa kutokana na uadilifu na kukubalika na makundi yote yakiwemo wazee,vijana na wasomi.

Tamko hilo limetolewa baada kumalizika kwa mkutano wa siku mbili uliofanyika katika Hoteli ya Maunti Uruguru mjini hapa na kufadhiliwa Asasi isiyo ya kiserikali ya kuondoa Umasikini,Ujinga na Maradhi(FPID) .

Alisema kuwa umoja huo umempitisha Makamba baada ya kupata kura 72 na kuwashinda Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliyepata kura 20 na Mbunge wa Ubungo John Mnyika kura 9 kati ya wajumbe 105 ambao ni viongozi wa Vyuo vikuu hapa nchini waliopiga kura hizo huku kura sita zikiharibika.

Alisema kuwa baada ya kupendekeza majina mengi na matatu kupigiwa kuwa na Makamba kuibuka mshindi walianza kuchambua sifa za Makamba na kuona kama anaweza kuibuka kuwa Rais wa nchi hii na kuona kuwa wala haitajiki kusafishwa kutoka na uadilifu wake.

Alisema kuwa sifa nyingine za Makamba ni pamoja na uwezo na ujasili katika nafasi za uongozi alizoshika ikiwemo ya Ubunge wa jimbo la Bumburi mkoani tanga,uwenyekiti wa kamati ya nishati na madini,ujumbe wa kamati kuu na naibu waziri alinao sasa.

Rais huyo wa Chuo kikuu cha Mzumbe alisema kuwa katika mkutano huo wasomi hao walijadili kwa kina sifa ya rais anayepaswa kuchaguliwa katika uchaguzi ujao bila kujadili itikadi za kisiasa ambaye atawaunganisha watanzania na kutibu uhasama na mgawanyiko ulianza kujitokeza baina ya makundi mbalimbali.

Alisema kuwa katika mjadala huo wasomi hao walitaka kiongozi atakayeenda na wakati wa sasa na mwenye fikra mpya na asiyekuwa na udini wala mkabila na asiyeendeleza siasa za kikanda na asiye kuwa na chuki wala mapambano ya kisiasa na uhasama na kubaini Makamba ndie anayefaa kwakuwa anazo sifa zote.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari endapo viongozi hao wametumiwa na Makamba,alisema kuwa katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali likiwemo hilo na kwamba mpaka sasa hawana mawasilino yoyote na Makamba.

“ Tunataka kuwakikishia hatujatumiwa na mtu yoyote,tulifanya mkutano wetu tumejadili masuala ya elimu na na hili likajitokeza tukajadili na kuweka itikadi zetu pembeni kwa pamoja tukaona makamba ndiye anafaa kuwa raisi wa nchii hana kashfa yoyote,na hivi tunavyoongea nanyi hata yeye hajui suala hili” alisema Theophily.

Alisema wamechoka kutumika na viongozi katika masuala mbalimbali na kwamba hivi sasa ni wakati wa vijana kuongoza nchi hii kwakuwa ndio wamekuwa wakichangia kuleta maendeleo.

Naye mmoja wa viongozi hao Shibanda Mwashibanda,alisema kuwa katika kufanikisha suala hilo wanakusudia kumfata Makamba kumuomba aingie katika kinyanganyiro hicho cha uraisi katika uchaguzi ujao.

Alisema kuwa tayari wameshapanga vijana mbalimbali kuzunguka katika kila kanda kwajili ya kumpigia debe Makamba ili aweze kuchaguliwa kuwa raisi katika uchaguzi ujao.

“ Tumejipanga kila kanda kwa gharama zetu wenyewe ili vijana washambulie kila mkoa kwajiali ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba awe rais katika kipindi kijacho” alisema Mwashibanda.

Alisema kuwa muda wa nchi hii kutawaliwa na wazee hivi sasa umekwisha na ahadi zao zisizotekelezeka na kwamba huu ni muda wa vijana kuongoza nchi hii ili kukabiuliana na changamoto mbalimbali zinazojitekeza kila wakati.

Naye katibu wa asasi hiyo ya FPID Francis Ndunguru alisema kuwa asasi hiyo imewezesha viongozi hao kukutana na kujadili mambo yao ikiwemo ya elimu na haina mlengo wowote wa kisiasa wala kutumiwa na chama chochote cha kisiasa.
Source: Ashton Balaigwa; NIPASHE Morogoro



Sasa hivi kuna raisi wa umoja wa viongozi wa wanavyuo? Au wanampendekeza awe raisi wa chuo gani? Kwa hiyo sasa vyuo vinaweza kuchagua raisi ambaye si mwanachuo? Au January Makamba amejiunga tena na chuo? Nisaidieni.
 
Hata sijaisoma habari yenyewe kwa sabau haina Mashiko. badala ya kujadili mustakabali wa Taifa tunakaa kujadili mabo ya january makamba huu ni upumbavu
 
Elimu ya chuo kikuu ndo iko hv! ?

Labda ya mtihani ya hivi:

MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA.
MAELEKEZO.
i. Jibu maswali yote.
ii. Kila swali linabeba maksi kumi
iii. Zingatia mpangilio wa kazi.
iv. Unaruhusiwa kutumia BLOGS na MAGAZETI
YA UDAKU
iv. SWALI LA TISA NI LAZIMA KUJIBU.
MUDA; Masaa matatu.
SECTION A.
1. Kwa kutumia mifano hai, elezea chanzo cha
Kim Kadarshian kugombana na Kanye west.
2. Taja tofauti kuu nne kati ya MLIMANI CITY na
QUALITY CENTER.
3. Kwa kutumia maeneo ya samakisamaki, Coco
beach, Steers, na Kunduchi beach resort elezea
maana ya neno BATA.
4. Mapenzi hujengwa kati ya msichana na
mvulana. Je Vipini masikioni, Kuvaa mlegezo,
mwanaume kusuka na kujipaka carolight
vinachangia vipi kufanya penzi lichanue?
Fafanua!! Tumia mifano hai ya maboyfriend wa
watoto wa kishua
5. Kwa kutumia tamthilia za MARA CLARA na zile
nyingine za PROMISE na TIMELESS elezea nafasi
ya mwanamke katika jamii.
SECTION B
6. Elezea sababu kuu tano za WEMA na Diamond
kugombana!! Na kisha elezea mapinduzi
yaliyofanywa na Jokate Mwegelo. Na je kwa nini
hawakudumu
7. Inasemekana kuwa Chipsi mayai ni mojawapo
ya chakula kinachowachanganya wasichana
wengi na mwisho kujikuta wametoa penzi. Kwa
kutumia maeneo ya Masaki na Mikocheni elezea
Baga na Pizza zinavyosababisha tatizo hili.
8. Kwa kuwatumia wasanii wa Bongofleva kama
Diamond na wa mtoni kama Chriss Brown elezea
maana ya neno SWAGA.
9. Watoto wengi wa kishua hukimbilia kutafuta
mademu wa uswazi wakidai kuwa wasichana wa
geti kali hawajui lolote kitandani. Elezea kiufasaha
ukitumia mifano hai kwanini wasichana wa kishua
ni bomu kitandani.
10. Kwa kutumia mifano hai ya PLAYSTATION
elezea ni ipi ngumu sana kucheza kati ya PS 2 na
PS 3…..
NAWATAKIA MTIHANI MWEMA!!!
 
Taka taka zimeanza kupepeluka!!khaaaaaaa!! Makamba ni taka taka lile likachafue ikulu?......chama cha mataka taka (ccm)

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom