Vyama vyote vya upinzani katika nchi za kiafrika siyo vya kuaminika

Makamanda

Taarifa za uhakika nilizopata CCM imeandaa utafiti feki kupitia Twaweza....watasema Magufuli ana asilimia 68% na Lowassa 22%

Ripoti halali wanayo ya Lowassa kuongoza lakini watatoa ripoti Feki.

Kwa huu muda wa asubuhi mpaka saa 4 pigeni kelele kupitia njia mbalimbali kulaani ushenzi huu.Tumieni JF,FB,tweeter,Instagram nk...
 
You must always learn through others!
You must not take the mistakes of your neighbour as an opportunity, but rather take his fruits as a challenge to your journey!
 
Vyama vyote vya upinzani vilivyo shinda kwa kishindo na kuvibwaga vyama vya toka uhuru, Afrika vimeleta shida ambazo hata enzi za uhuru hazikwepo mfano mzuri ni nchi zinazotuzunguka kama Kenya, Malawi na Zambia. Akina Uhuru Kenyatta walijinadi watabadilisha masilahi ya walimu Kenya wakipewa nchi lakini cha kushangaza wameendeleza mambo yaleyale.

Walimu wakigoma badala ya kuwasikiliza wanakimbilia mahakamani, mikataba tu ya malipo ya walimu waliyoingia na serikali ya Moi wameshindwa kuitekeleza, wamekuwa walalamikaji kama wananchi wa kawaida na wamezidiwa mpaka wameamua kufunga shule zote. Ule msemo "ukitaka kwenda ikulu bila principles ukifika tu lazima uta-fail tu", umetimia Kenya.

Mkuu hongera kwa darasa zuri,haiingii akilini kuleta hoja mfu kwamba eti ccm ibaki yenyewe kwa kuwa zambia,kenya,rwanda,burundi wamebadilisha vyama lakini hawasemi kwa nini kati ya nchi zote hizo ya kwetu ndio ina amani
 
Unaweza kudanganya baadhi ya watu kwa muda lakini huwezi danganya watu wote siku zote. Utajiri na mali ghafi iliyopo tanzania sio sawa na maendeleo yanayoonekana. Tulitakiwa kuwa na barabara za njia sita hadi nane, flyovers, huduma za afya, elimu bora na za uhakika. Ccm imetudanganya kasungura kadogo kwa miaka mingi. Je, itafanikiwa kudanganya watu wote siku zote.
 
Online polling mbali mbali zinaonyesha Lowasa ana 80plus dhidi ya 20plus za magufuli hii inamaana wanaopata taarifa wamekataa kudanganyika. Tar 25 wote tukapige kura tuone tumebaki na asilimia ngapi ya wanaokubali kudanganywa na ccm.
 
Mkataa pema pabaya panamuita, waliopewa nafasi kugombea wameokotwa toka kwenye vyama tofauti, yupo kwenye chama A lakini mawazo yake mawazo yake yapo chama B, hapa hakuna siasa ya kweli hata kidogo. Juma Duni alisusia kampeni kisa chadema wanatawala zaidi kuliko CUF, sijui mwisho wao utakuaje hawa jamaa

Kwa historia ya Tanzania unaamini ungeweza kupata mgombea katika ngazi yoyote ile ambae amezaliwa na kukuwa bila kuwa mwanachama wa chama kingine? Ni lazima ujue kuwa viongozi wengi hutoka katika chama kimoja kwenda kingine kwa kuwa wamekosa nafasi ya kusikilizwa au kuonyesha uwezo wao wa kuwatumikia wananchi. Hatukatai, maslahi binafsi hujificha nyuma ya nia njema na hilo halipo kwa unaemdhania tu.
 
Mkuu hongera kwa darasa zuri,haiingii akilini kuleta hoja mfu kwamba eti ccm ibaki yenyewe kwa kuwa zambia,kenya,rwanda,burundi wamebadilisha vyama lakini hawasemi kwa nini kati ya nchi zote hizo ya kwetu ndio ina amani

Danganya wajinga Zambia ina amani na demokrasia ya kweli kuliko Tz mnapumbaza watu kwa kisingizio cha amani wakati watu wenu maskini na rasmali zimewazunguka ila wageni ndiyo wanao faidi
 
Back
Top Bottom