Vyama vya upinzani na mgomo wa TUCTA

Ningependa kujua kuwa vyama vya upinzani vina mawazo gani kuhusu suala zima la madai ya TUCTA na kufuatilia vitisho vya serikali kuzuia wafanyakazi kugoma.

Mkuu, kwangu mimi vinavyoweza kuitwa vyama vya siasa ni vile vilivyoweza kuambulia angalau viti vya Ubunge. Vikubwa viko vitatu navyo ni CUF, CCM na Chadema na kile cha binafsi cha Cheyo ambacho siwezi hata kukumbuka jina lake. Kwa bahati mbaya CUF kimeamua kujenga uswahiba na CCM na hivyo kukosa sifa ya kuitwa chama makini cha upinzani. Kama lengo ni kuiondoa CCM madarakani, basi CUF wamechemsha na hivi sasa hakina uhalali wa kujinadi kwa sera ya kutetea maslahi ya wanyonge wa Taifa hili.

Kwa mantiki hiyo ni chama kimoja tu, Chadema, ambacho mpaka sasa kinajali na kimeonyesha nia thabiti ya kuipeleka CCM mapumzikoni kama tutakiunga mkono. Ile jazba, matusi, vitisho na kupayuka ovyo kwa Kikwete ni dalili na matokeo ya mapungufu ambayo yamejitokeza hivi karibuni katika kambi ya upinzani. Kufagiliwa na Mrema wa TLP na tamaa ya Shariff wa CUF kwa serikali ya mseto ni mambo mazito yanayoweza kumpa faraja ya muda na kumvimbisha kichwa Raisi wetu mpaka anajisahau.

Toka lini kiongozoi wa nchi akatoa ahadi ya kutembezea kipigo kwa wafanya kazi kama watathubutu kudai haki zao huku amezungukwa na wakuu wa jeshi na polisi ? Anazidi kudai na kuonya kuwa wapo watakaoumia na wengine hadi kupoteza maisha - jamani, ni wakati wa vita tu Raisi anaweza kutumia jukwaa kama lile kwa maadui wa nje wenye lengo la kulishambulia taifa. Na atafanya hivyo kulingana na katiba alioapa ya kuwalinda wananchi waliomweka madarakani na kamwe si kutangaza vita dhidi yao.

Kwa kutoa hotuba kama alivyofanya, Kikwete anakosa kabisa uhalali wa kuendelea kuliongoza taifa kwani ni wazi amevunja katiba. Je ikitokea leo mwananchi yeyote akipoteza maisha akiwa mikononi mwa vyombo vya usalama, Kikwete yuko tayari kuwajibika ? Anapomnyooshea kidole mwananchi mmoja na kutishia kuwa hataonekana tuelewe nini kwani serikali ndiyo inatakiwa isimamie usalama wa Nicolas Mgaya. Kwa wazee wa Dar es Salama kukubali kutumiwa kubariki njama hizi za kifashisti dhidi ya raia wema wa nchi hii nasema shame, shame, shame !

Kikwete must go na Chama Chake cha Mauaji !

 
Nadhani unge-rekebisha sentensi yako na kuwa hivi...."Dr. Slaa ana maoni gani?" maana so far sioni chama cha upinzani kilichosimama imara zaidi ya Mh. Dr. Slaa as an individual.

Naona sentensi ulivyotaka iwe "Dr Slaa ana maoni gani?" Ni mtazamo wa chuki dhidi ya Chadema hauwezi kutenganisha Kiongozi na Chama.Slaa umemjua kwa sababu ya Chadema ni dhahiri hauwezi kuzungumzia harakati za Uhuru ukamtaja Nyerere bila TANU. Nyerere ni Tanu na TANU ni Nyerere vivyo hivyo Slaa ni Chadema na Chadema ni Slaa
 
Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania wengi ni kutokuwa na uwezo wa kufaya uchambuzi yakinifu na wa kisayansi ambao ungeweza kupelekea kuwa wabuni. Hili ni tatizo sana matokeo yake tunasubili kitu kitokea kitu ndipo kila Kiongozi, kila mwenye uwezo wa kuandika na kutuma taarifa, kila mwenye uwezo wa kusoma n.k n.k utamuona anajitokeza.

Unajua inashangaza sana

Kwa bahati mbaya sana suala hili lipo hadi Ikulu ambapo tulidhani ni eneo Takatibu kama vile kule Mbinguni ambapo wanakaa watakatifu ambaye anashindwa kuwa mtakatifu hutolewa ni kama alivyofanywa yule ibirisi. Sasa nasema hebu tuache kuwa kama FISI anayesubili mtu apite ili afuate nyuma kwa matarajio ya mkono wa mtu utaanguka na atapata mlo.

Tuwe WABUNIFU tuache kubwabwaja.
 
nchi inaingia kwenye makundi nadhani ndio mwanzo wa mwisho kuburuzana, najua maandamano yakianza
nchi itapoteza uelekeo kwenye uchumi na siasa
 
Back
Top Bottom