Vurugu Makambako

Mangandula

Senior Member
Nov 30, 2011
184
37
Wafanyabiashara wa maduka yanayozunguka soko kuu Makambako, leo wameandamana na kuziba barabara zote kuu za songea, mbeya na Iringa. Tatizo ni walinzi waliowaweka wao wenyewe kwa ajili ya kulinda maduka usiku kukutwa na funguo bandia pia kuwafuma wakiwa ndani ya maduka yao usiku wa saa 8, hii ilitokana na mlinzi mwenzao kuwajulisha wenye mali! Vulugu zimeanza baada ya polisi kuwaachia watuhumiwa jioni hii na kumkamata m/kiti wa soko na kumsweka ndani, hapo ndipo peoples power ilipoanza, polisi wamelazimika kuita FFU kutoka Iringa na Njombe, hivi ninavyo andika post hii mabomu ya machozi yanapigwa hovyo na watu wanakimbia hovyo. Chanzo cha habari- wananchi Makambako.
 
walinzi wawaweke wenyewe waandamane kwa serikali!
Huu upuuzi wa maandamano ulioanzishwa na hawa jamaa bila elimu ya kutosha unaleta shida sana.
 
Hivi polisi hawana jinsi nyingine ya kutuliza mambo zaidi ya kutumia nguvu kupita kiasi. mbona hapa dhana ya polisi jamii inaonekana kuyeyuka? Nina question elimu na uwezo wa polisi kushughulikia matatizo ya raia kwani matukio ya polisi kuwaachia wahalifu yanazidi kupamba moto licha ya backlash wanazopata kutoka kwa wananchi wanaoathirika.
 
Read between the line. Wameanza kuandamana baada ya police kuwaachia hao walinzi bila kulidhishwa kuachiliwa kwao. May be hao policcm ndo walikuwa wanawatumia hao walinzi.
 
yawezekana polisi hufaidika na vitu vinavyoibwa ndiyo maana wameamua kuwachilia huru.
 
Wanyalukolo tulieni tu, mlikubali kupokea rushwa mkamchagua yule jamaa aliyeishia darasa la pili kuwa mbunge na sasa hamna mtetezi. Tofautisheni kati ya kuchagua mbunge na kuchagua mfadhili. Lema fika hadi Makambako kuelimisha.

Enzi Mwakipande yuko hai hao walinzi wasingethubutu kuingia dukani kuiba, kila duka lilikuwa na Self Defense
 
walinzi wawaweke wenyewe waandamane kwa serikali!
Huu upuuzi wa maandamano ulioanzishwa na hawa jamaa bila elimu ya kutosha unaleta shida sana.

Unaonekana hujaelewa, wanaandamana kwa sababu watuhumiwa wameachiwa halafu viongozi wao wametiwa ndani

Iinaonyesha
 
Hayo ndo matokeo ya kuwalipa walinzi mishahara midogo; hata hivyo JAH PEOPLE yupo atawasaidia.
 
walinzi wawaweke wenyewe waandamane kwa serikali!
Huu upuuzi wa maandamano ulioanzishwa na hawa jamaa bila elimu ya kutosha unaleta shida sana.

Kiongozi soma kwa makini. Watu wamewekwa ndani lakini kama kawaida polisi wanawaachia. Halafu kesho utawasikia Mwema na Chagonja wakiongea kihusu polisi jamii na utii wa sheria bila kushurutishwa!
 
imenibidi niongee na rafiki yangu ambaye ni mfanyabiashara hapo nijue kulikoni? huu mchezo wa walinzi kuiba usiku baada ya wenye mali kuondoka ulikuwa unafanyika kwa muda mrefu ila baadhi ya walinzi hawakuufurahia na hivyo kutoshiriki. walichofanya ni kuwataarifu viongozi wa soko nini huendelea usiku na kuwaahidi kuwa punde wakiwabip usiku basi wajue kazi imeanza. Viongozi wa soko wakapata missed call na kwenda sokoni wakawakuta baadhi ya walinzi wakiwa na master keys wamefungua duka na wanaiba bidhaa. viongozi wa soko wakawashushia kipigo kizito walinzi wezi na kuwaita polisi. polisi walichofanya walipofika eneo la tukio waliwachukua wale walinzi pamoja na viongozi wa soko. walipofika kituoni wakawaweka ndani viongozi wa soko na wale walinzi wakapelekwa hospitali ambako wamelzwa mpaka sasa hali zao zikiwa mbaya. wafanyabiashara wengine wamekasirishwa na kitendo cha polisi kuwaweka ndani viongozi wao ndipo akapelekea kufungwa kwa barabara kushinikiza viongozi wao kuachiwa na hatimaye polisi ikatii kutokana na vurugu hizo. kwa sasa viongozi wametolewa na walinzi bado wapo hospitali wakiwa mahututi na pingu mkononi.
 
Askari wa tanzania ni janga lingine la taifa.Kila siku ya Mungu ni mabomu ya machozi.Kwa bahati mbaya mimi si mwanajeshi wala si polisi ila kwa umri wangu naamini hayo mabomu wanayotumia yananunuliwa kwa fedha nyingi za kitanzania,je,hakuna njia nyingine ya kutuliza gasia kama maandamano?Sidhani kama watanzania wamefikia kiwango cha kutulizwa kwa kutumia mabomu.Ni hatari kwa serikali kuwapa mafunzo ya kijeshi wananchi ambao hawana mpango wa kujifunza mafunzo hayo.Ipo siku mabomu yatazoeleka tu na hapo ndipo mambo ya Cossovo yatakapoanza nchini.
Swala la muhimu kwa nchi yetu ni kuwa na maadili.Najua hapo Makambako mabomu yamepigwa na mwisho baadhi ya wananchi watakamatwa kwa kuwekwa ndani ya ulinzi wa polisi hapo ndipo biashara ya rushwa itakapoanza.Kwa njombe sasa ni fashion kuwaweka watu ndani kwa madai ya maandamano na kisha wanatolewa kwa fedha nyingi.Hakika rushwa ni aibu ya Taifa.tuwe wakweli nchi yetu inachungulia shimo la mauti.R.I.P CCM.Nguvu ya umma Makambako inatisha.
 
Back
Top Bottom