Wafanyabiashara wa maduka yanayozunguka soko kuu Makambako, leo wameandamana na kuziba barabara zote kuu za songea, mbeya na Iringa. Tatizo ni walinzi waliowaweka wao wenyewe kwa ajili ya kulinda maduka usiku kukutwa na funguo bandia pia kuwafuma wakiwa ndani ya maduka yao usiku wa saa 8, hii ilitokana na mlinzi mwenzao kuwajulisha wenye mali! Vulugu zimeanza baada ya polisi kuwaachia watuhumiwa jioni hii na kumkamata m/kiti wa soko na kumsweka ndani, hapo ndipo peoples power ilipoanza, polisi wamelazimika kuita FFU kutoka Iringa na Njombe, hivi ninavyo andika post hii mabomu ya machozi yanapigwa hovyo na watu wanakimbia hovyo. Chanzo cha habari- wananchi Makambako.
Hawa askari wetu vipi,mbona wao ndio waliosababisha vurugu zote hizi kwa kuwaachia watuhumiwa?Ni kweli wao wana mabomu na wananchi hawana kitu.Hivi nyie maaskari mnawafundisha nini watanzania,mnataka kusema hii ndiyo nja mwafaka ya kuleta amani katika nchi?Wafanyabiashara wameibiwa mali zao na ninyi bila huruma mnacheka na wezi,mnadhani ni rahisi kuwanyamazisha wafanyabiashara kwa mabomu ya machozi?ole wenu mnaotetea watuhumiwa,ipo siku nanyi nguvu ya umma utawashukia msijue cha kufanya.