Vuguvugu la "occupy" linasambaa

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
16 Oktoba 2011 09:57 Maandamano duniani kote ya kupinga kile waandamanaji wanakiona kama uroho nausimamizi mbaya wa uchumi duniani yameingiasiku ya pili. Katika miji kadhaa - kutoka Auckland hadi Toronto - waandamanaji walikesha katika mahema kushinikiza wanasiasa wachukue hatua.

Haijawa wazi iwapo maandamano yanaanza kushikamana na kuwa kitu kikubwa. Mjini London, msemaji alisema lengo ni kuiga mambo yanayotokea mjini New York, katika mtaa wa masoko ya fedha, ambako maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana kwa wiki
kadhaa. Mjini London waandamanaji wamelala nje ya kanisa kuu la Saint Paul, katikati ya jiji, baada ya kuondoshwa jana nje ya Soko la Hisa.

Watu kama 500 walibaki, na wengi wao walilala kwenye mahema kama 70, wengine walikaa juu ya ngazi nje ya kanisa. Wana kauli moja - wamekerwa na serikali ya mseto ya Uingereza kubana matumizi, na wamehamaki kuwa mabenki yanasaidiwa. Biramu moja linasema "mwisho umefika".

Wanalalamika kuwa demokrasi haifanyi kazi na wanasema watabaki hapo wakiwa ni sehemu ya vuguvugu la dunia. Baadhi yao wanasema wanaweza kubaki hapo hadi Disemba.

Source:BBC
 
dah! kuna moja leo imeniacha hoi....jamaa walijipanga nje ya stanbic bank wakitaka ku withdraw pesa zao zote......
lucky me niko huku kwetu kasulu i dont have to worry about a ****ed up world economy!
 
Yaani wewe hapo uko huko vijijini Kasulu na ndipo ukatutangulia kusikia ya mijini sio? Wakati mwingine unapounda uongo ni bora uwekeze walau muda wa kufikiri.

dah! kuna moja leo imeniacha hoi....jamaa walijipanga nje ya stanbic bank wakitaka ku withdraw pesa zao zote......
lucky me niko huku kwetu kasulu i dont have to worry about a ****ed up world economy!
 
tu-i copy nini! Maana ndo kilichobaki.

Mkuu, siyo ku-kopi (copy), ni occupy, yaani miliki au chukua, hili ni vuguvugu ambalo limeanza kuenea sasa dunia yote ya nchi tajiri sana na zilizoendelea kiviwanda. Ni kwamba wananchi wanaandamana kupinga sera za kifedha (kiuchumi, zinazopendelea mabenki) za nchi zao na kutowajali wananchi wa kawaida ambao wanaathirika kiuchumi kutokana na sera hizo. Lengo la waandamanaji ni kuzitaka serikali zao ku-review sera hizo ili ziwe fair kwa pande zote, wananchi na mabenki. Vuguvugu hilo limepewa jina la Occupy...... halafu unataja jina la mji mnakoandamana. Mfano Occupy Tokyo.
 
Hivi bongo hakuna corporations?Ama zenyewe si greedy?

Mkuu
Vyombo vya fedha na mabenki yapo Tanzania. Tena yanawakomoa wateja. Unauliza uroho wa corporations wakati huo ndio mfumo kwao?
Hili la uroho wa fedha haliko kwa mabenki tu. Tz tunaadhibiwa na tunaathiriwa na "ufisadi" pia. Kigenge cha wezi wanaojichukulia fedha za umma huwa wanaonekana ndio wajanja na wameula kimaisha.

Ukiweka fedha zako chache benki, siku umekumbuka kuwa uliweka 50,000 elfu zako ,ukienda kutaka kuzichukua unaambiwa;
"doooh, ulikuwa wapi? Tunakutafuta siku nyingi, una deni la 20,000 kama ada ya akaunti"

Yaani 50,000 elfu yako imekwenda na maji na deni juu! Unapandwa na hasira lakini unapokumbuka kuwa TZ ni kisiwa cha "amani na utulivu", unageuka kuelekea mlangoni na kwenda kulalamika nyumbani.

Sera za IMF na World bank zilipoletwa miaka ile, wanasiasa, viongozi wetu walituambia tukaze mikanda na tuchangie huduma za jamii.
Wao wanajiengezea kima cha mishahara na masurufu, marupurupu.

Kasumba ya tukaze mikanda na utamaduni wa kutoa na kupokea rushwa umetufanya tuone kila kitu ni sawa tu.

watanzania tumeacha kujifikiria kama jamii, tunachofanya ni kila mtu kuchumia tumbo lake hata kama ni kuwaumiza watanzania wenzake.
Hata wale walio waelewa wa mambo badala ya kuuamsha umma na kuchukua hatua , ili kushibisha" tumbo" wanakimbilia kwenye "kula" aka siasa.
 
16 Oktoba 2011 09:57 Maandamano duniani kote ya kupinga kile
waandamanaji wanakiona kama uroho na
usimamizi mbaya wa uchumi duniani yameingia
siku ya pili. Katika miji kadhaa - kutoka Auckland hadi
Toronto - waandamanaji walikesha katika
mahema kushinikiza wanasiasa wachukue
hatua. Haijawa wazi iwapo maandamano yanaanza
kushikamana na kuwa kitu kikubwa. Mjini London, msemaji alisema lengo ni kuiga
mambo yanayotokea mjini New York, katika
mtaa wa masoko ya fedha, ambako maelfu ya
watu wamekuwa wakiandamana kwa wiki
kadhaa. Mjini London waandamanaji wamelala nje ya
kanisa kuu la Saint Paul, katikati ya jiji, baada ya
kuondoshwa jana nje ya Soko la Hisa. Watu kama 500 walibaki, na wengi wao walilala
kwenye mahema kama 70, wengine walikaa juu
ya ngazi nje ya kanisa. Wana kauli moja - wamekerwa na serikali ya
mseto ya Uingereza kubana matumizi, na
wamehamaki kuwa mabenki yanasaidiwa. Biramu moja linasema "mwisho umefika". Wanalalamika kuwa demokrasi haifanyi kazi na
wanasema watabaki hapo wakiwa ni sehemu
ya vuguvugu la dunia. Baadhi yao wanasema wanaweza kubaki hapo
hadi Disemba.
Source:BBC

Hv sisi tunasubiri nini wakuu? kama hata uingereza wamestuka sisi tuna nini mpaka tuwe wavumilivu namna hii?
 
Nadhani viongozi wetu washatulazimishia kufikiri kuwa shida na umasikini ni tamaduni zetu.
 
Hv sisi tunasubiri nini wakuu? kama hata uingereza wamestuka sisi tuna nini mpaka tuwe wavumilivu namna hii?

Kwa ubongo wa panzi,watu kama faizafoxy,omr,makupa unategemea nini?
Amin nakwambia, mambo yakibadilika wakina nape wataikimbia nchi,kukwepa malipo ya uwongo wao.
 
Neno democracy limetokana na maneno mawili.Yaani Demon na crasia.Maana ya demon unaijua na crasia ni neno la kilatini lenye maana ya authority.Kwa hiyo democrasia au democracy maana yake ni utawala wa mapepo.Sijui kama unaona jinsi tulivyoingizwa mkenge.Sasa katika utawala wa mapepo unategemea nini.Obviously kilio na kusaga meno.Na bado,matumbo yatauma kwa dhiki zilizopo mbele yetu.
16 Oktoba 2011 09:57 Maandamano duniani kote ya kupinga kile waandamanaji wanakiona kama uroho nausimamizi mbaya wa uchumi duniani yameingiasiku ya pili. Katika miji kadhaa - kutoka Auckland hadi Toronto - waandamanaji walikesha katika mahema kushinikiza wanasiasa wachukue hatua.

Haijawa wazi iwapo maandamano yanaanza kushikamana na kuwa kitu kikubwa. Mjini London, msemaji alisema lengo ni kuiga mambo yanayotokea mjini New York, katika mtaa wa masoko ya fedha, ambako maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana kwa wiki
kadhaa. Mjini London waandamanaji wamelala nje ya kanisa kuu la Saint Paul, katikati ya jiji, baada ya kuondoshwa jana nje ya Soko la Hisa.

Watu kama 500 walibaki, na wengi wao walilala kwenye mahema kama 70, wengine walikaa juu ya ngazi nje ya kanisa. Wana kauli moja - wamekerwa na serikali ya mseto ya Uingereza kubana matumizi, na wamehamaki kuwa mabenki yanasaidiwa. Biramu moja linasema "mwisho umefika".

Wanalalamika kuwa demokrasi haifanyi kazi na wanasema watabaki hapo wakiwa ni sehemu ya vuguvugu la dunia. Baadhi yao wanasema wanaweza kubaki hapo hadi Disemba.

Source:BBC
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Licha ya Mabenki kuna wizi mkubwa sana unafanywa na makampuni ya simu hapa Tanzania kwa wateja lakini serikalia kupitia TCRA na Umma wote umetiwa maji na kutota!
 
Mkuu, siyo ku-kopi (copy), ni occupy, yaani miliki au chukua, hili ni vuguvugu ambalo limeanza kuenea sasa dunia yote ya nchi tajiri sana na zilizoendelea kiviwanda. Ni kwamba wananchi wanaandamana kupinga sera za kifedha (kiuchumi, zinazopendelea mabenki) za nchi zao na kutowajali wananchi wa kawaida ambao wanaathirika kiuchumi kutokana na sera hizo. Lengo la waandamanaji ni kuzitaka serikali zao ku-review sera hizo ili ziwe fair kwa pande zote, wananchi na mabenki. Vuguvugu hilo limepewa jina la Occupy...... halafu unataja jina la mji mnakoandamana. Mfano Occupy Tokyo.

Hapo ndipo Nyerere anapokuwa nabii/professor; Thanks Magoba!
 
Mkuu
Vyombo vya fedha na mabenki yapo Tanzania. Tena yanawakomoa wateja. Unauliza uroho wa corporations wakati huo ndio mfumo kwao?
Hili la uroho wa fedha haliko kwa mabenki tu. Tz tunaadhibiwa na tunaathiriwa na "ufisadi" pia. Kigenge cha wezi wanaojichukulia fedha za umma huwa wanaonekana ndio wajanja na wameula kimaisha.

Ukiweka fedha zako chache benki, siku umekumbuka kuwa uliweka 50,000 elfu zako ,ukienda kutaka kuzichukua unaambiwa;
"doooh, ulikuwa wapi? Tunakutafuta siku nyingi, una deni la 20,000 kama ada ya akaunti"

Yaani 50,000 elfu yako imekwenda na maji na deni juu! Unapandwa na hasira lakini unapokumbuka kuwa TZ ni kisiwa cha "amani na utulivu", unageuka kuelekea mlangoni na kwenda kulalamika nyumbani.

Sera za IMF na World bank zilipoletwa miaka ile, wanasiasa, viongozi wetu walituambia tukaze mikanda na tuchangie huduma za jamii.
Wao wanajiengezea kima cha mishahara na masurufu, marupurupu.

Kasumba ya tukaze mikanda na utamaduni wa kutoa na kupokea rushwa umetufanya tuone kila kitu ni sawa tu.

watanzania tumeacha kujifikiria kama jamii, tunachofanya ni kila mtu kuchumia tumbo lake hata kama ni kuwaumiza watanzania wenzake.
Hata wale walio waelewa wa mambo badala ya kuuamsha umma na kuchukua hatua , ili kushibisha" tumbo" wanakimbilia kwenye "kula" aka siasa.

Tena yanawakomoa sana kwa kuwatoza riba kubwa kupita kiasi. Sasa hivi nchi nyingi za Magharibi, kama unachukua mkopo kwa fixed rate basi watakupa kati ya 3% mpaka 4% kwa miaka mitano na kama ni variable rate unaweza kupata kati ya 2.5% mpaka 3% lakini nchini kwetu sasa hivi riba ya mkobo kutoka katika mabenk yaliyopo nchini kama sikosei iko juu ya 12% huu ni wizi wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom