Lakini kaka Paskali utabiri wa Lema ulitimia and Magufuli is gone na pengine wa ndugai huenda nao ukatimia, ingawa uli-categorize kama source ya utabiri wake ni shetani based on your views or visions.Wanabodi,
Japo siku zote Nabii huwa hakubaliki nyumbani, hili nalijua na litabezwa, na nimeisha lisemea humu
TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums
Hii ni thread ya maono ya unabii, na sio utabiri na sio trends reading, ni unasikia tuu sauti inakuambia jambo fulani bila kuambiwa sababu na huwezi kuuliza, hivyo nami naomba kuwaeleza tuu sauti niliosikia na naomba msiniulize kitu kwasababu sio mimi ni sauti!.
Leo nilikuwa naangalia jinsi Bunge la Marekani, the Congress linavyomshughulikia rais wa Marekani, Donald Trump, ambapo azimio la kumshitaki kwenye Bazara la Senate limepitishwa, japo kule Senate itakuwa ni ngumu kwa azimio hilo kupata ile theluthi 2 ya kumuondoa ila kumshitaki tuu rais ni hatua kubwa.
Kuna mchangiaji mmoja akasema hata Tanzania ikithibitishwa rais Magufuli amevunja katiba kwa kuzuia mikutano ya siasa kinyume cha katiba, anaweza kushtakiwa!.
Ndipo nikauliza ni Bunge lipi hilo la kumshitaki Rais Magufuli?, nikauliza kama ni Bunge hili hili la Mhe. Ndungai au ni Bunge lijalo?, na ndio mara ghafla nikasikia sauti from within, ikiniambia kuwa "Spika ajaye ni Mhe. Dr. Tulia Akson. Sauti hiyo ikaniambia japo Mhe. Ndungai, atakuwa anatamani sana kuendelea kuwa Spika, lakini Ndugai hatakuwa kwa sababu fulani, (japo sauti hiyo imenieleza hizo sababu za kwa nini Mhe. Ndungai hataendelea kuwa Spika Bunge lijalo, lakini sio lazima kusema kila unachosikia, kwa sababu sometimes sio kila unachosikia from within ni sauti kutoka kwa Mungu au ni maono, sauti nyingine ni sauti za shetani tuu na sio sauti za Mungu, kama zilivyo ndoto nyingine, ni ndoto za shetani kama ile "ndoto ya Lema", ukisikia sauti ukahisi inaweza isiwe sauti ya Mungu, au ukiota ndoto ya jambo la ajabu ajabu ukahisi jambo hilo sio la kheri, sio lazima uliseme). Mfano ni tangu August 14, 2014 nilielezwa rais ajaye wa Tanzania ni Magufuli, na nilielezwa sababu kwanini ni Magufuli, nami nikaeleza humu lakini sikuzisema.
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
Hili la kutokusema kila unachokisikia, nimelisisitiza hapa
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa? - JamiiForums
Jambo tangu baada ya Spika Sitta, trends za uspika zimeonyesha kiti cha Spika ni just one term only na term hiyo ikiisha, Naibu Spika ndio huwa Spika. Wakati wa Spika Sitta, Naibu Spika alikuwa Anna Makinda, japo Sitta alitamani kuendelea, aliwekwa pembeni, Naibu wake Anna Makinda akachaguliwa kuwa Spika. Wakati wa Spika Anna Makinda, Job Ndugai alikuwa Naibu Spika, baada ya Makinda kumaliza one term yake, Naibu wake Job Ndugai akawa Spika, hivyo trends zinaelekeza baada ya Spika Job Ndugai, automatically, Spika anayefuatia ni Naibu Spika Dr. Tulia Akson, ila hili sio bandiko la trends za uspika ni bandiko la " Voices from Within".
Hitimisho.
Hiki kinachofanywa na Bunge la Marekani kwa rais wao, jee kingeweza kufanywa na Bunge la Tanzania, suppose ni kweli rais Magufuli anakiuka Katiba?.
Hoja kama jee ni kweli rais Magufuli anakiuka katiba au laa, bado sio hoja kwasababu mamlaka peke yenye uwezo wa kutafsiri sheria kama kwa kuzuia mikutano ya siasa, rais Magufuli akiuka katiba ama laa ni Mahakama Kuu pekee, na so far hakuna mtu yoyote au chama chochote kilicho omba tafsiri ya kisheria ya uamuzi huo wa rais Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa kama unakiuka katiba au laa, lakini pia kwa vile Spika ajae kwa mujibu wa maono haya ni Dr. Tulia Akson, hata rais Magufuli akikiuka katiba, Bunge la Dr. Tulia, tena kwa kuzingatia litakuwa ni Bunge la chama kimoja CCM, litaweza kumwajibisha rais?.
Alhamisi Njema.
Paskali
All in All naamini wote Lema and You mna unique abilities, and that is unquestionable.