Vodacom rudisheni vifurushi vyetu siyo kuomba radhi wateja!

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
774
196
WanaJF,

Kutokana na usumbufu wa mawasiliano uliotokea tarehe 16/8/2013, Vodacom wameamua kuwaomba radhi wateja wao kwa kuwatumia ujumbe wa maneno unaosema, "Ndugu mteja,Tunapenda kukutaarifu kuwa huduma zetu zimerejea.Tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea tarehe 16/8/2013.Endelea kufurahia huduma za Vodacom."

Kuomba radhi wateja kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno peke yake hakutoshi! Vodacom wanatakiwa kutuambia ni vipi wataturudishia wateja wao vifurushi vya internet vya masaa tulivyokuwa tumevinunua na kupotea bila kutumika kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano! Bila kufanya hivyo Vodacom wataendelea kuonekana wezi! Waturudishie vifurushi vyetu ili tuendelee kufurahia huduma za Vodacom!
 
Naona hata intanet yao inasumbua haikamati,au ni kwangu tu,imenibidi kurudi airtell haraka sana.
 
Hao ni wezi wakubwa

Kama Rostam bado anahisa Vodacom, watanzania tutaendelea kuibiwa tu mpaka tutakapompata mkombozi wa kweli! Kumbuka kuna zile milioni 153 ambazo kundi la akina Rostam wanalipwa kila siku kutokana na mkataba tata wa Richmond! Tunatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kuhamia kwenye mitandao mingine.
 
Mi nashangaa kusoma msg za malalamiko kuhusu vodacom mbona mi nishahamia airtel mwez sasa kutikana na wiz wao.
 
TCRA yaani hawana msaada wowote
kuhusu haya mambo ya voda yaliyojiri.
 
wezi sana hao voda..mi siku hiyo nilitumiwa 10,000 haikuingia kwenye simu na mpaka leo haijarudi kwa aliyenitumia wala kuja kwangu..

msamaha wasaidia nn wakati watu tumepata hasara!!!!!!
 
Bado cjawaelewa hao vodacom coz wanaomba radhi wkt nimenunua umeme kwa m pesa leo asubuhi mpaka sasa hakuna units wala kurudishiwa salio langu.Na cjui nianzie wapi
 
aseee voda ni ------- ni mambulula wameniboa kidogo nitapike nyongo nimetamani kuchoma mitambo yao yote
 
wezi sana hao voda..mi siku hiyo nilitumiwa 10,000 haikuingia kwenye simu na mpaka leo haijarudi kwa aliyenitumia wala kuja kwangu..

msamaha wasaidia nn wakati watu tumepata hasara!!!!!!

Graca, Pole sana! Tuombe Mungu kama Vodacom wamo humu jamvini wasikie vilio vyetu!
 
KakaJambazi, kama hata wewe unakiri kuwa Vodacom ni majambazi wenye kutumia usanii wa hali ya juu,basi tumekwisha!

hahaa hahaa haha,nikiliona jina la KakaJambazi na michango yake huwa napata raha sana,amani kwako Jambazi
 
Back
Top Bottom