USHAURI: Rais Samia aondoke madarakani kwa heshima kuliko Wananchi/Bunge kumwondoa

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,511
4,224
Upi mtazamo wako kwa yale yanayoendelea hapa nchini? Je, endapo itamlazimu kiongozi wa serikali kuondoka ipi itakuwa njia sahihi?

Ndani ya miaka hii miwili watanzania wameshuhudia na kupitia katika kipindi kigumu pengine kuwahi kutokea Tanzania. Ni kipindi ambacho huenda kinyozi wa saluni amefunga ofisi yake si chini ya mara 5 kwa wiki, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia kuibuka watu wanaoitwa chawa! Ni kipindi ambacho kimeua, kutesa na kudhulumu maelfu ya wananchi hususan wa daraja la chini kiuchumi kwa aidha tozo, miundombinu mibovu (ajali) huduma mbovu na sera mbovu za afya, na usimamizi mbovu wa huduma zitolewazo na serikali.Ni kipindi ambacho tumeshuhudia uzembe na ufisadi kurejea kwa kasi serikalini, ni kipindi ambacho watanzania wameshuhudia ulambaji wa asali pengine kuliko awamu yoyote ile, ni kipindi ambacho tumeshuhudia wanafunzi wakikaa chini bila madawati huku viongozi wakila maisha kwa ziara,semina za pongezi na hafla za anasa! N.k

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.

1. Uchumi wa Tanzania Umeporomoka. Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2. Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo. Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3. Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4. Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao. Tangu Rais Samia aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana. Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5. Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua. Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6. Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi. Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7. Kupanda kwa bei ya Mbolea. Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8. Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9. Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10. Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11. Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12. Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma. Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo. Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13: Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao. Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao. Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14. Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito, Maziwa, Bahari, Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama, Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15. Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16. Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17. Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18. Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19. Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20. Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21. Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22. Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23. Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
 
Toka umeanza kuandika pumba mwaka juzi unapuuzwa na kudharauliwa tuu..

Nyie si ndio mlisema hamalizi miaka 2 saizi deadline itakuwa ni lini?
20230327_131653.jpg
 
Muongo mkubwa wewe maana umeandika Mambo ya kiuopotoshaji tu hapa, kwanza ningependaa kuanza kukwambia kuwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ndio chaguo la watanzania katika kuwaongoza muhula wa pili.

Mh Rais amefanya juhudi kubwa Sana katika kuliongoza Taifa letu katikaa namna iliyoleta Tabasamu na matumaini kwa watanzania.

Mh Rais ameleta maendeleo katika kila secta na hivyo kugusa maisha ya watanzania,mfano katika suala la mbolea kupanda Bei mh Rais na serikali Yake alitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea Hali iliyoleta unafuu wa Bei sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu.

Katika Nishati ya mafuta pia mh Rais na serikali yake ilikuwa inatoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi hatua iliyoleta ahueni katika Bei ya mafuta hapa nchini na hivyo kushusha Bei kwa bidhàa zingine,na Ikumbukwe kuwa Bei ya mafuta haikupandishwa na serikali Bali ilitokana na kupanda katika soko la Dunia kulikokuwa kumesababishwa na Vita vya urruss na ukreini.

Suala la tozo pia serikali yetu inaungwa na kuungwa mkono na watanzania,hatuwezi kutegemea misaada kwa kila kitu hata kwa vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu,mannuufaa yake Tumeona Ni mengi Sana mfano ujenzi wa vituo vya Afya kila Kona,ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20,utoaji wa Elimu bure Hadi kidato Cha sita,ongezeko la mikopo kufukia biliioni 654 kwa Elimu ya juu na hivyo kusaidia watoto wa maskini kupata Elimu na kutimiza Ndoto zao za kielimu.

Suala la ajira serikali ya Rais Samia imetoa ajira za kutosha kabla zaidi ya elfu 42 zikiongozwa na secta ya Afya na Elimu,lakini pia kupitia uboreshaji wa secta binafsi na kuvutia wawekezaji nchini kulikotokana na juhudi za mh Rais kuimarisha diplomasia yetu ya Mambo ya nje kumepelekea kuongezeka kwa miradi mingi ya kiuwekezaji iliyotoa fursa za ajira kwa vijana na kuongeza mapato ya kikodi mpaka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi na hivyo kuvunja historia katika ukusanyaji wa mapato tangia Taifa letu lipate Uhuru,

Suala la demokrasia Hilo Sina haha ya kueleza Sana maana kila mtu anaona namna demokrasia ilivyoshamiri hapa nchini mpaka Sasa viongozi wote wa vyama vya siasa wanakaa meza moja na kubadili Mambo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Ukija katika suala la mikopo ,ningependaa kukujibu kuwa kukopa siyo dhambi Wala jinai katika masuala ya Uendeshaji Wa nchi na katika kuchochea maendeleo,kinachoangaliwa na ambacho kimekuwa kikizingatiwa na serikali ya Rais Samia Ni aina ya mkopo,masharti ya mkopo,muda wa kurejesha au kuanza kufanya marejesho ya mkopo, mahali au kazi inayokwenda kufanywa na mkopo husika,Rais Samia na serikali Yake amekuwa akizingatia hayo yote kwa maslahi mapana ya Taifa letu na amekuwa akitueleza wazi watanzania,lakini pia hali ya Deni letu la Taifa siyo mbaya na tunao bado uwezo wa kulipa,lakini pia ulipaji wetu umekuwa Ni mzuri ndio maana tunekuwa tukiaminiwa na Kuendelea kukopeshwa ,kwa uaminifu huo ndio maana unaona China mwaka Jana ilitusamehe takribani billioni 31 fedha ambazo zitawekezwa katika maeneo mengine yanayogusa maisha ya watanzania.

Suala la safari za Rais , ningependaa kukujibu kuwa Tanzania siyo kisiwa ,lazima watanzania Tushirikiane na wenzetu katika nyanja mbalimbali,Rais Samia katika safari zaie ambazo amezifanya nje ya nchi zimeleta tija kubwa Sana kwa Taifa letu,mfano Ni safari na ziara ya Rais Samia nchini kenye ambayo ilifungua ukurasa mpya wa kidiplomasia hatua iliyoongeza na kuchochea biashara kwa watanzania ,ambapo Tanzania tunaendelea kunufaika na soko la mazao yetu nchini Kenya ,hali iliyopelekea mkulima kupata Bei nzuri ya mazao na hivyo kufaidika na jasho lake, lakini pia safari na ziara ya mh Rais nchini chini tulishuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali katika secta mbalimbali ambazo zitachochea mapinduzi ya viwanda,ongezeko la ajira kwa vijana,ongezeko la mapato ya kikodi,n.k,lakini Ni katika ziara hiyo ambapo Tanzania tulisamehewa Deni la billion 31.

Ni katika ziara hizo za mh Rais tunashuhudia kwa Sasa Tanzania ikiwa kimbilio na chaguo namba moja la wawekezaji na watalii ,Hali itakayo saidia kupata pesa za kigeni,lakini pia ni katika kuitangaza nchi yetu na kuimarishwa kwa diplomasia yetu kulikofanyika kupitia Royal Tour iliyofanywa na kuongozwa na mh Rais tunashuhudia kuwa Tanzania Ni moja ya nchi tatu pekee katika katika Bara Zima la Afrika zitakazotembelewa na kupewaa heshima na makamu wa Rais wa marekani ,hii yote Ni kutokana na heshima kubwa na Taswira njema iliyojengwa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ndani ya muda mfupi aliokaa madarakani Kama Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama
 
Naunga mkono hoja kiufupi Hana anachokifanya kuwapunguzia wananchi adha ya maisha magumu kutwa kutafuta kiki kupitia matukio yanayovuta watu wengi.
 
Hii nchi mama imemshinda hana option nyingine zaidi ya mikopo. Acha tuone mwisho wake. Ninashinda sana vijijini huko kuna project huwa tunazifanya watu maisha magumu sana. Imagine mnavyofika pale vijini wananchi wanawafata wanaomba misaada hadi huruma. Kuna mama alinipa jogoo wa 5 wakubwa kwa 20k tu nilimpa hela nikamwambia kuku abaki nao.

Lawama zote zinakwenda kwa mama why yeye? Kuna watu wanahali ngumu sana. Wale wanaokula ugali wa shikamoo, machawa na wale walamba asali watakutukana sana leo. Umetupa jiwe gizani.
 
Upi mtazamo wako kwa yale yanayoendelea hapa nchini? Je, endapo itamlazimu kiongozi wa serikali kuondoka ipi itakuwa njia sahihi?

Ndani ya miaka hii miwili watanzania wameshuhudia na kupitia katika kipindi kigumu pengine kuwahi kutokea Tanzania. Ni kipindi ambacho huenda kinyozi wa saluni amefunga ofisi yake si chini ya mara 5 kwa wiki, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia kuibuka watu wanaoitwa chawa! Ni kipindi ambacho kimeua, kutesa na kudhulumu maelfu ya wananchi hususan wa daraja la chini kiuchumi kwa aidha tozo, miundombinu mibovu (ajali) huduma mbovu na sera mbovu za afya, na usimamizi mbovu wa huduma zitolewazo na serikali.Ni kipindi ambacho tumeshuhudia uzembe na ufisadi kurejea kwa kasi serikalini, ni kipindi ambacho watanzania wameshuhudia ulambaji wa asali pengine kuliko awamu yoyote ile, ni kipindi ambacho tumeshuhudia wanafunzi wakikaa chini bila madawati huku viongozi wakila maisha kwa ziara,semina za pongezi na hafla za anasa! N.k

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.

1. Uchumi wa Tanzania Umeporomoka. Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2. Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo. Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3. Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4. Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao. Tangu Rais Samia aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana. Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5. Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua. Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6. Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi. Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7. Kupanda kwa bei ya Mbolea. Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8. Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9. Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10. Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11. Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12. Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma. Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo. Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13: Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao. Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao. Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14. Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito, Maziwa, Bahari, Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama, Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15. Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16. Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17. Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18. Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19. Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20. Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21. Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22. Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23. Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

#15
Umeme sasa kuunganisha ni Laki 8 sio laki 3 mkuu
Rekebisha hapo pls
 
Back
Top Bottom