TCRA mmeridhika na wizi wa vifurushi unaofanywa na Vodacom? Kifurushi Cha 1.2GB kinaisha less than 24hrs for normal chatting?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Makampuni ya simu Uhuru na mamlaka mnazojitwalia za kuwaibia wananchi kwa kutukomoa au kurejesha fedha za hasara mlizopata kipindi Cha nyuma si sahihi.

Nimejiunga kifurushi cha wiki 1.2GB cha Vodacom jana saa sita kasoro usiku. Then nikazima data hadi saa nne asubuhi. Nimewasha data since saa nikawa naperuzi mitandao ya kijamii pamoja ikiwemo kutumia WhatsApp. Ilipofika saa tano usiku nikapata ujumbe kwamba nimebakiwa na MB300+, baada tu yakupokea ujumbe huo nikapokea ujumbe mwingine kifurushi chako kimekwisha. Naomba Vodacom watusaidie watumiaji wao wa internet.

1. Ni katika mazingira gani data 1GB zinaweza kuisha bila hata kudown file mtandaoni?

2. Ni kipi kimebadilika kabla ya utawala wa awamu iliyopita na utawala huu? Before ilikuwa ukijiunga kifushi Cha GB 1 unamaliza wiki nzima Kama huduma inavyojieleza. Leo kifurushi Cha wiki kinaisha less than a day

3. Nimeshtushwa na MB 300 kuisha ndani ya ten minutes, je alert sms mnazotuma zinafika kwa wakati kwa wateja au zinadelay? Unapomtumia mteja sms ya alert ya 300Mb zimebaki wakati huohuo inaingia sms zimeisha mnamaanisha Nini?

4. Baada ya kifurushi kuisha nilipiga simu kwa huduma kwa mteja, majibu yao ni kwamba, wanathibitisha kwamba sms ya mb300 na Sms kuisha kwa kifurushi zimetumwa kwa mda wa less than 15 mnts. Unawauliza sababu wanakwambia Kuna mafaili makubwa unadownload , seriously kwamba mteja awezi kujua amedownload kitu gani? Na kwa speed gani hiyo ya kutumia 300MB per 10Mnts?

Lakini hii siyo mara ya Kwanza, kila ukijiunga GB let say 2+ za ths 5000 unashtuka less than 3dys zimeisha. Mnapotukomoa sisi kwa kujua mamlaka zimewakalia kimya mnadhani tukifilisika vifurushi watanunua wakina Nani?

Waziri mwenye dhamana malalamiko haya ya Dakika na vifurushi yamekuwa mengi mitandaoni lakini hakuna hatua unayochukua wala kutoa anagalau ufafanuzi au kufanya utafiti na kutoa majibu endapo unaamini walalamikaji wanakosea, umekaa kimya kisa wewe na Watendaji wakubwa serikalini vocha na vifurushi mnanunuliwa na serikali.

Jaribuni kuvaa viatu vya wananchi wanaowalipa mishahara. Bila mawasiliano wengine hatuwezi kuingiza kipato, kuendelea kutudhibiti tusitumie mawasiliano kupata vipato vyetu nikudidimiza uchumi wa nchi.

Vodacom pesa mnazochukua za dhulma ipo siku ataingia mweu atawafilisi. Mmetufanya sisi Kama ndondocha ipo siku na ninyi pamoja na ukubwa wenu kama kampuni mtapoteza wateja. Wizi siyo kitu kizuri hasa mnapotuibia wanyonge wa nchi hii.

Nina hasira basi tu
 
Mkuu yote uliyoelezea ni sahihi, halafu hili janga si lako pekee bali ni la wote ila watu hawapigi tu kelele lakini maumivu wanayasikia kama si kuyaona!

Mie baada ya kuona hawarekebishi na waziri husika hana mpango, niling'oa hiyo line na kupachika Halo tel nikitumia voice na data.

Halo tel ingawa hawana kasi kama Voda, lakini hawana uhuni huo tena wana gharama nafuu kuliko Voda na pia ukiunga kifurushi cha data au voice kifurushi haki'expai' bali kina 'cease' na ukiunga kipya, kilicho cease kinasisimka na kusongeshwa kwa kuunganishwa na kipya ulichojiunga.
 
"2. Ni kipi kimebadilika kabla ya utawala wa awamu iliyopita na utawala huu?"

Upuuzi wako uko hapo kwny hio statement,voda upigaji wa vifurushi wanafanya tangu miaka mingi iliyopita na mpk sasa kazi ya upigaji inaendelea vyema.
 
Waziri na tcra wako busy kuangalia raia wanaofanya makosa mitandaoni kuibiwa kwa wananchi wala hawajali,malalamiko ya kuibiwa na voda na kampuni zingine za simu yamekua mengi lakini usikii wahusika serikalini kuongelea hii kitu!!
Waziri yupo bize na kuchamba
 
Kumbe ndio wizi huu,mimi nimeshindwa kabisa kuelewa mara mbili nanunua kifurushi cha week Gb 1 lakini ndani ya 24hrs natumiwa sms umemaliza kifurushi chako,wakati huo mchana wote nimezima simu,sina Instagram,siangalii youtube,sidownload apps na files,natumia JF na Twitter tu.
vodacom acheni wizi
 
Back
Top Bottom