Vitunguu vs Viazi Ulaya

Vinahifadhika mpaka miezi mitano. Kwa mfano Karatu ikifika mwezi wa Kumi wanaweka ghalani mpaka mwezi wa pili mwaka unaofuata ndipo wanaviuza...............Ila ujaribu kutengeneza ghala linalopitisha hewa vizuri na liwe kavu lili visioze ingawa hupungua uzito kiasi (lakini kwa soko la Kenya ndiyo huzingatia uzito).......Nazitafuta picha zinazoonyesha ghala lilivyo zikipatikana nitakutumia kwa PM (na ghala lenyewe linatengenezwa kwa mabanzi, miti na kuezekwa kwa nyasi) na hii ni Karatu ndiyo wanafanya kwa sababu wana uzalishaji mkubwa.

Kuhusu huyo mkulima huyo yupo wilaya ya Iramba kiijiji cha Mwanga.............unapitia njia ya kinampanda na kupita barabara inayoenda Hydom..........Naiangalia namba yake nitakutumia PM

Nashukuru kwa Ushauri mkuu be blessed I will check with you once I encounter any hurdle
 
Asante. Labda pengine unataka kulima maeneo gani? na utatumia mvua au kumwagilia? na kama kumwagilia ni kwa kutumia pampu au matone?

Kitunguu kinaweza kulimwa sehemu ambapo hamna maji kabisa?? ukategemea mvua?
 
Kitunguu kinaweza kulimwa sehemu ambapo hamna maji kabisa?? ukategemea mvua?

Yap, kama nilivyoeleza kwa sehemu kubwa singida wanatumia mvua.......tena kama ni large scale huwa wanamwaga mbegu hawapandi kwa mstari na advantage yake ni kuwa hutumwagilii na matumizi ya mbolea ni kidogo sana lakini tatizo ni kuwa uzalishaji si mkubwa sana
 
Unaposema uzalishaji si mkubwa sana unamaanisha wanachopata kama gunia ngapi hivi kwa heka moja?

Nafikiria kufanya majaribio
 
Platozoom
Ni lazima kuotesha mbegu kwenye kitalu kwanza? huwezi kupanda moja kwa moja vikakubali?
 
Platozoom
Ni lazima kuotesha mbegu kwenye kitalu kwanza? huwezi kupanda moja kwa moja vikakubali?

Unaweza kumwaga mbegu bila kuweka kwenye kitalu lakini hiyo inafaa tu wakati wa masika. Maji ya kutosha na hutumii mbolea kwa wingi au bila kutumia mbolea kabisa kama sehemu ina rutuba. Kiangazi ni vizuri kupanda kwenye kitalu kwa sababu kila tone la maji lina thamani yake mkuu
 
Mkuu mi nna interest na ulimaji wa vitunguu. Kama inawezekana naomba uni PM details zaidi.
Thanks sana mkuu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Iwapo mvua itakataa kabisa kunyesha bado kitunguu kinaweza ku survive au inakuwa maafa tu?

Kitunguu kinahitaji maji lakini si kwa kiasi kikubwa........kwa mfano mwezi wa miezi miwili ya kwanza kinahitaji maji na mvua ikikatika kwa muda mrefu kweli hayo ni maafa kabisa..........ndio maana kitunguu (kama zao la mboga) hufaa sana kulimwa kama bustani au mfumo wa jaruba kwenye kiangazi.

Lakini ni vyema kama unaamua kulima kipindi cha masika at least uwe umechimba shimo ambalo utahifadhi maji ya mvua in case mvua imekata unayatumia................Au kama umelima karibu na mto ni rahisi kupata maji ..........unafukua mchanga na kupata maji na hapo unaweza ku-pump kirahisi (Wilaya ya Iramba kwa sehemu wanafanya hivi)
 
Mnanitia hasira mwaka jana si nililima bwana kumbe washenzi walisupply mbolea feki nikala mweleka
Ila najua one day yes nakomaa mwakani na Eka kumi Singida uko mpaka kieleweke
Kilimo ukiwa serious kinakutoa kuna jamaa wanataka vitunguu ambavyo vyaoteshwa kwa organic manure bado naendelea kuwasaka nkipata data zao ntamwaga apa ila nasikia inalipa sana
 
Nina mpango wa kulima kimojawapo lengo ni kulima heka 3 cha msingi nahitaji kujua zao lenye faida zaidi ya lingine,changamoto zake,soko pia muda nitakao utumia tangu kupanda mpaka kuvuna.
Mi nilifikiri unataka kutuambia faida ya vitu hivyo labda kwamba ni dawa? Wacha nifungue haraka, kumbe du! kilimo kwanza!
 
Kitunguu kinahitaji maji lakini si kwa kiasi kikubwa........kwa mfano mwezi wa miezi miwili ya kwanza kinahitaji maji na mvua ikikatika kwa muda mrefu kweli hayo ni maafa kabisa..........ndio maana kitunguu (kama zao la mboga) hufaa sana kulimwa kama bustani au mfumo wa jaruba kwenye kiangazi.

Lakini ni vyema kama unaamua kulima kipindi cha masika at least uwe umechimba shimo ambalo utahifadhi maji ya mvua in case mvua imekata unayatumia................Au kama umelima karibu na mto ni rahisi kupata maji ..........unafukua mchanga na kupata maji na hapo unaweza ku-pump kirahisi (Wilaya ya Iramba kwa sehemu wanafanya hivi)

Nikichimba kisima kikubwa si naweza kunyeshea moja kwa moja kutoka kisimani au gharama zitakuwa kubwa sana?
 
Kitunguu kinaweza kulimwa sehemu ambapo hamna maji kabisa?? ukategemea mvua?

kitunguu kinalimwa kwenye tuta kama la nyanya ili kiweze kufyonza maji + kupenya kirahisi, kinahitaji maji mengi ili kiweze kutengeneza tunda kubwa na lenye quality... kikikosa maji ya kutosha kinakufa njiani au kinatoa vitunguu vidogo vidogo kama pipi.

NB: Mara nyingi huwa tunakiweka kwenye kundi la horticulture na hufanywa kwa njia za umwagiliaji at least mara moja kila siku labda kama eneo lako mvua itakuwa inanyesha zaidi ya mara 4 kwa wiki
 
Mnanitia hasira mwaka jana si nililima bwana kumbe washenzi walisupply mbolea feki nikala mweleka
Ila najua one day yes nakomaa mwakani na Eka kumi Singida uko mpaka kieleweke
Kilimo ukiwa serious kinakutoa kuna jamaa wanataka vitunguu ambavyo vyaoteshwa kwa organic manure bado naendelea kuwasaka nkipata data zao ntamwaga apa ila nasikia inalipa sana

Pole sana Njowepo
 
Last edited by a moderator:
Asante mke wa Raisi!Tz kuna mambo yanakera watu wanaleta mbolea feki sasa wameamia kwenye dawa nazo feki alafu sijawai sikia mtu katimuliwa au kahukumiwa jela.
No way ni kukomaa tuu kivyangu maana serikali haina msaada kabisa kwa wakulima wa inchi hii.
Kwa fertile land na ukubwa wake Tz ilibidi tuwe exporter wa mazao ya chakula miti matunda maua issue ni infrastructure na viongozi kuendekeza 10% nyambafu
 
Nikichimba kisima kikubwa si naweza kunyeshea moja kwa moja kutoka kisimani au gharama zitakuwa kubwa sana?

Gharama kuwa kubwa inatokana na ukubwa wa shamba.........ni vizuri ulime kwa majaruba ili kutunza maji (kiangazi)
 
Mnanitia hasira mwaka jana si nililima bwana kumbe washenzi walisupply mbolea feki nikala mweleka
Ila najua one day yes nakomaa mwakani na Eka kumi Singida uko mpaka kieleweke
Kilimo ukiwa serious kinakutoa kuna jamaa wanataka vitunguu ambavyo vyaoteshwa kwa organic manure bado naendelea kuwasaka nkipata data zao ntamwaga apa ila nasikia inalipa sana

Mkuu fuatilia hiyo kitu utupe data sehemu nilipo mimi kuna organic manure nyingi sana ni rahisi kutumia organic manure kuliko kutumia mbolea za viwandani
 
Platoom naomba tuwasiliane PM nahitaji ushauri wa karibu zaidi. Mi nimeanza kama pilot test Moshi. Nalima heka 1 kipindi hiki ambacho sio cha msimu. Nilikua interested nikaona nijaribu kwanza na heka 1 ili nipate picha halisi ya gharama na experience. So far vinatokelezea poa sasa. Nimeanza august ndo nasonga songa mbolea ya mwisho.
I would love to get your report as u said umefanya study sana kwa hilo zao.
Am interested mkuu.
Tuwasiliane tafadhali

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom